Tupike pamoja wali nazi, maharage nazi na miguu ya kuku

Tupike pamoja wali nazi, maharage nazi na miguu ya kuku

Mie huwa muda wa kula siupi uzito sijajua kwanini.
Naweza amka saa 9 usiku nikapika ugali na kula.
Ila nikilala hapoooo nitakuja kuamshwa na winch😊
Pambana kupunguza kitambi mkuu, kula wanga usiku na kulala kupita kiasi na unywaji wa bia, Hiyo ni formula mbaya ya maisha na ni kikwazo cha kufikia malengo yako.

Sijajua BMI yako Ila bado unaweza kuwa overweight maana lifestyle Yako ni mbaya.
 
Pambana kupunguza kitambi mkuu, kula wanga usiku na kulala kupita kiasi na unywaji wa bia, Hiyo ni formula mbaya ya maisha na ni kikwazo cha kufikia malengo yako.

Sijajua BMI yako Ila bado unaweza kuwa overweight maana lifestyle Yako ni mbaya.
BMI yangu target yangu ni kg 72.
Bado 3 tu nifike mwisho
 
BMI yangu target yangu ni kg 72.
Bado 3 tu nifike mwisho
Kula matunda tu usiku hata Kwa week mara 3, jipe mazoezi ya kutokula chips week 2, punguza kula wanga mwingi usiku, Jipe muda wa mazoezi asubuhi(Abbs 10×2, jumps 12×4 pumzika 1mn kila zoezi Kama una kamba ni vizuri) fanya hivi kila siku Kwa muda wa week 2 alafu nenda kapime Tena.
 
Kula matunda tu usiku hata Kwa week mara 3, jipe mazoezi ya kutokula chips week 2, punguza kula wanga mwingi usiku, Jipe muda wa mazoezi asubuhi(Abbs 10×2, jumps 12×4 pumzika 1mn kila zoezi Kama una kamba ni vizuri) fanya hivi kila siku Kwa muda wa week 2 alafu nenda kapime Tena.
Sawa boss wangu.
Nitafanya hivo.
Nashukuru sana kaka Lighton
🙏🙏🙏🙏🙏
 
Leo siku ya Ijumaa niliamka nikiwa nina hamu ya kula kitu kichachu chachu japo sina 🦎 wala nini.

Asubuhi huwa naamka na hii detox special kwa ajili ya kupunguza uzito.
Imenipunguza toka huko niliko mpaka sahv kwenye kg 75.
View attachment 3336542View attachment 3336543View attachment 3336544
Huwa nina program hiyo kwani hukata uzito balaa na huwa nakuwa nayo makini katika unywaji kwani nataka nibaki na kilo zangu za ujana na nyash! yangu ibakie vilevile pia.

Mchana nikajiendea zangu sehemu wanauza miguu ya kuku na vishombo shombo kadhaa.
View attachment 3336545

Nikafika nyumbani nikaiandaa vyema na kutia viungo kisha nikaifunika na kuiacha masaa 2 ili ichanyanyikiwe😂

Hapo maharage yangu yalikuwa jikoni na tayari nimeshayaunga na tui bubu tu.
Huwa sie wanawake wa pwani nazi sio shida zetu, ndio maana tunatumia tui bubu tu katika kupikia vyakula.
View attachment 3336547
Lile tui la pili huwa napenda sana kuliogea au kunawia uso na huku kwa bibi kwani huleta mvuto na mnato zaidi.

Na hapo nilikuwa nishauchambua mchele wangu na kutoa vitaka vyote na virangirangi vya jarubani.
Kisha nikakuna nazi ingine na kupika wali mtamu wa nazi wenye ukoko ukoko.
Mie napenda sana ukoko hasa ukiwa wa wali, uji au ukoko wa ugali.
View attachment 3336548
Na baada ya kuivisha wali nazi na harage nazi, nikaanza kukarangiza miguu yangu ya kuku☺️
Nilikatia katia kila kitu jikoni kisha nikaimwagia miguu humohumo, nikaipika ikaiva nikatia limau na kapilipili huku nadokoa mpaka ikakaribia kuisha jikoni.
View attachment 3336549

Na baada ya hapo nikakata kata kachumbari na kutenga mezani kisha nikaupiga mwingi.

Karibuni sana warembo wenzangu na wakaka wote wa Jamii Forums na visitors wote.
View attachment 3336550
Nyie watoto wa ushuani wenzenu huku uswazi miguu ya kwioo ni mboga tamu sana hasa uipatie kindimu na kipilipili cha kutupia👌

Hapa nilipo nashushia na Castle lite ya baridi mixer kvant ili nipate nguvu za kwenda Club kusakata muziki vizuri maana leo weekend imeanza
View attachment 3336556

Cheers!!!!!🥂🍻🥂🍻🥂🎵🎵🎵
Mie kupika ni moja kati ya hobby zangu,nikiona uzi wa mapishi naufungua mbiombio.Nimeusoma huu uzi wako nikafurahi sana,hasa unapoogea tui la nazi kwa bibi,japo naomba uwe makini maana usijepeleka maambukizo kwa bibi maana babu atakosa chakula chake.
Miguu ya kuku mimi ilishanishinda kula kabisa hivyo huwa sihangaiki navyo,maharage ni mboga yangu muhimu sana kwenye kila msosi ni lazima maharage yawepo na ndio mboga ninayotumia bajeti kubwa kutoa nyama.Asante
 
Back
Top Bottom