Leo siku ya Ijumaa niliamka nikiwa nina hamu ya kula kitu kichachu chachu japo sina π¦ wala nini.
Asubuhi huwa naamka na hii detox special kwa ajili ya kupunguza uzito.
Imenipunguza toka huko niliko mpaka sahv kwenye kg 75.
View attachment 3336542View attachment 3336543View attachment 3336544
Huwa nina program hiyo kwani hukata uzito balaa na huwa nakuwa nayo makini katika unywaji kwani nataka nibaki na kilo zangu za ujana na nyash! yangu ibakie vilevile pia.
Mchana nikajiendea zangu sehemu wanauza miguu ya kuku na vishombo shombo kadhaa.
View attachment 3336545
Nikafika nyumbani nikaiandaa vyema na kutia viungo kisha nikaifunika na kuiacha masaa 2 ili ichanyanyikiweπ
Hapo maharage yangu yalikuwa jikoni na tayari nimeshayaunga na tui bubu tu.
Huwa sie wanawake wa pwani nazi sio shida zetu, ndio maana tunatumia tui bubu tu katika kupikia vyakula.
View attachment 3336547
Lile tui la pili huwa napenda sana kuliogea au kunawia uso na huku kwa bibi kwani huleta mvuto na mnato zaidi.
Na hapo nilikuwa nishauchambua mchele wangu na kutoa vitaka vyote na virangirangi vya jarubani.
Kisha nikakuna nazi ingine na kupika wali mtamu wa nazi wenye ukoko ukoko.
Mie napenda sana ukoko hasa ukiwa wa wali, uji au ukoko wa ugali.
View attachment 3336548
Na baada ya kuivisha wali nazi na harage nazi, nikaanza kukarangiza miguu yangu ya kukuβΊοΈ
Nilikatia katia kila kitu jikoni kisha nikaimwagia miguu humohumo, nikaipika ikaiva nikatia limau na kapilipili huku nadokoa mpaka ikakaribia kuisha jikoni.
View attachment 3336549
Na baada ya hapo nikakata kata kachumbari na kutenga mezani kisha nikaupiga mwingi.
Karibuni sana warembo wenzangu na wakaka wote wa Jamii Forums na visitors wote.
View attachment 3336550
Nyie watoto wa ushuani wenzenu huku uswazi miguu ya kwioo ni mboga tamu sana hasa uipatie kindimu na kipilipili cha kutupiaπ
Hapa nilipo nashushia na Castle lite ya baridi mixer kvant ili nipate nguvu za kwenda Club kusakata muziki vizuri maana leo weekend imeanza
View attachment 3336556
Cheers!!!!!π₯π»π₯π»π₯π΅π΅π΅