Tupo kwenye vita kali sana ya kiuchumi na Kenya

Tupo kwenye vita kali sana ya kiuchumi na Kenya

Hakuna maneno ya kuandikwa yakatoshea kuelezea usumbufu alioupata. Kuna interviews zake YouTube anaelezea, alipokea hadi meseji za vitisho
No, namaanisha sema, mfano VIONGOZI WETU NI.......
SERA ZETU NI........
Ndo maana wawekezaji wanakimbia.
 
Umesahau na uchama. Hakuna sera za taifa kuna sera za chama halafu sera za chama zipo nyingiii, kila kiongozi anajichagulia tu ipi ina manufaa kwa wakati husika.
Sera ya Taifa ipo na wananchi walishirikishwa kama Chadema mnataka kutunga sera yenu na kuita ya Taifa shindeni uchaguzi kwanza.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Huu ni uongo mwingine
Kwenye manufacturing wanaangalia cost of production kama kipaumbele

Mexico inavutia viwanda vingi kuliko marekani kwa sababu wana cost of production ndogo
Unapotosha. Mexico wanavutia kwa cheap labor intensive investment tu peke yake. Yaani uwekezaji unaohitaji cheap unskilled labor. Na hiyo cheap labor wana export kwa wingi sana Marekani kwenye mashamba ya matunda na mboga. Marekani ni wa kwanza duniani kwa kuvutia uwekezaji unaohitaji mitaji na teknolojia kubwa.
 
Huu ni uongo mwingine
Kwenye manufacturing wanaangalia cost of production kama kipaumbele

Mexico inavutia viwanda vingi kuliko marekani kwa sababu wana cost of production ndogo
Acha kuongea vitu ambavyo huvunji. Kwenye uwekezaji huo kikubwa zaidi kinachosngaliwa ni ROI, halafu fahamu Dangote wanajenga refinery ya kudumu hata miaka 100, mafuta yenu ya Uganda tu yataisha ndani ya miaka 20, Kenya nao wana mafuta na wataanza kuyachimba.
 
Sera ya Taifa ipo na wananchi walishirikishwa kama Chadema mnataka kutunga sera yenu na kuita ya Taifa shindeni uchaguzi kwanza.
Sera ya taifa inaathiriwa vipi na ilani ya chama tawala?

Epuka mahitimisho usiyo na uhakika nayo, unless unataka kuyatumia kama kichaka cha kukwepa hoja. Mfano hilo la chadema.
 
Sera ya taifa inaathiriwa vipi na ilani ya chama tawala?

Epuka mahitimisho usiyo na uhakika nayo, unless unataka kuyatumia kama kichaka cha kukwepa hoja. Mfano hilo la chadema.
Unalalamika nini hapa?
 
Tena ndani ya nchi yake.
Screenshot_20260708_113556_Chrome.jpg
 
Unalalamika nini hapa?
Hakuna malalamiko, jikite kwenye hoja. Sera ya taifa inaathiriwa vipi na ilani ya chama tawala?

Epuka kuhama hoja kwa kuwepa kwepa na kuingiza yasiyohusika itapendeza zaidi.
 
Umesahau na uchama. Hakuna sera za taifa kuna sera za chama halafu sera za chama zipo nyingiii, kila kiongozi anajichagulia tu ipi ina manufaa kwa wakati husika.
Watu wanapayuka tu kuhusu Kenya na Dangote ila hawafahamu jinsi mazingira ya biashara yalivyo magumu Tanzania kuanzia urasimu uliopitiliza, miondombinu duni, ukosefu wa wafanyakazi wenye weledi na usumbufu wa wanasiasa wa chama tawala wanaodai michango na kuja kujidai kwenye uwekezaji binafsi.
 
Niliwaza hivi pia, ila Wadau wanasema hiyo si factor, factor ni gharama za uzalishaji.
Vyote hivyo vinapigiwa hesabu kwenye uwekezaji kisha vinafanyiwa comparison kwenye cost benefit analysis.
Kwa mfano muwekezaji anajiuliza maswali yafuatayo:
1.Gharama za uzalishaji ni kubwa lakini je nikimudu hizo gharama za uzalishaji nikaanza uzalishaji soko lipo?
2.Na kama soko lipo je bei nitakayouza itamudu kurudisha gharama za uzalishaji na kupata faida?
3.Je wakati huo nimeshaanza kuzalisha na kuuza nikipata changamoto yoyote itatatuliwa kwa wakati au hadi nitoe rushwa tena ndio uzalishaji uendelee?hapa Kenya wametupiga gepu
4.Je nikihitaji wafanyakazi professional kwa haraka bila uzalishaji kusimamishwa nitawapata kwa haraka au hadi nikatafute watu ulaya niwalete?hapa ndipo Kenya wanapotupiga gepu
5.Je kuna malighafi zilizo tayari kwa matumizi au hata mpango tu wa miaka michache mbeleni kwamba kutakuwa na projects za kuandaa malighafi?jibu hapana
 
Hata yeye mkuu si amesema hapo wanavutia uwekezaji mkubwa kwenye viwanda ? Hajasema uwekezaji wa aina zote
Kasema viwanda vingi kuliko Marekani. Viwanda gani? Mexico wanavutia kwa viwanda vya cheap unskilled labor tu. Tena siyo peke yako. Wanashindana na China, Vietnam, Pakistan, etc.
 
Watu wanapayuka tu kuhusu Kenya na Dangote ila hawafahamu jinsi mazingira ya biashara yalivyo magumu Tanzania kuanzia urasimu uliopitiliza, miondombinu duni, ukosefu wa wafanyakazi wenye weledi na usumbufu wa wanasiasa wa chama tawala wanaodai michango na kuja kujidai kwenye uwekezaji binafsi.
Stroke hajajibu hoja, kaja na kichaka cha nyie chadema mje na sera yenu. Uchama umetukaa, hatuwezi tena kukaa tukajadili jambo lenye manufaa bila vita ya kichama. Sijui tumlaumu Nyerere au nani.
 
Ukifuatilia matukio mawili utagundua tupo kwenye vita kali sana ya kiuchumi na kenya
  1. Dangote refinery in mombasa
  2. Rwanda kuanza kutumia bandari ya mombasa kushafirisha mafuta
Soma pia Dangote aichagua Kenya badala Tanzania kuanzisha kiwanda kikubwa cha kusafishia mafuta
Kenya ni mshindani wetu wa fursa miaka yote, tatizo letu sisi ni nchi ya rushwa sana kuliko Kenya, sisemi kuwa Kenya hamna rushwa hapana, nchi zote za watu weusi maslahi ya mtu binafsi yanatangulia kuliko nchi.
Embu tujiulize swali moja, Dangote alishakubali kujenga kiwanda Tanzania na Kenya ilikubali bila taabu, na zingatia kuwa Kenya yenyewe iliona kuwa ili mafuta yawe rahisi basi kiwanda kijengwe Tanga!! Kwa kuwa waliona itakuwa suluhu ya matatizo ya mafuta kwa maana ya gharama za usafishaji wa crude oil.

Miradi mingi ya uwekezaji wa muda mrefu huathiriwa sana na rushwa, kwa kuwa watu walioko madarakani siku zote wanatengeneza mianya ya kumiliki uchumi kwa muda mrefu ili kuhakikishia vizazi vyao usitawi wa kudumu.
Wakati Dangote anajenga kiwanda cha simenti kule Mtwara tulihakikishiwa kuwa bei ya cement itashuka, jiulize kwa nini mpaka leo bado bei inapanda badala ya kushuka?? Tamaa ya watoza kodi ambao siku zote hutaka kupata zaidi kwa wananchi.

Lakini kumbuka changomoto alizokutana nazo Dangote wakati wa kujenga kiwanda na kuanza uzalishaji wa saruji kule Mtwara!! Ashukuriwe John Pombe(RIP) Kwa kuingilia kati na kuondoa makando kando ya rushwa.
Vita yetu ya uchumi ni ubinafsi wa maamuzi yetu wenyewe, Mazingira mazuri ya kuwekeza huvutia wawekezaji, je sasa hivi tunayo mazingira hayo??
Haya matishio ya maandamano yasiposhughulikiwa na serikali yatafukuza wawekezaji wengi, kiburi cha watawala ndio tatizo tulilonalo sasa.
 
Sera ya Taifa ipo na wananchi walishirikishwa kama Chadema mnataka kutunga sera yenu na kuita ya Taifa shindeni uchaguzi kwanza.
Mngekuwa na sera ya Taifa msingehangaika hata kwa mambo madogo tu kama ya ujenzi wa barabara. CCM haikuwahi kuwaza kama kuna siku Dar es Salaam itahitaji mwendokasi au treni za mjini ndio maana inabomoa barabara za lami kila mahali ili wajenge mwendokasi na kusababisha upotevu wa mabilioni ya walipa kodi usumbufu mkubwa.
 
Vyote hivyo vinapigiwa hesabu kwenye uwekezaji kisha vinafanyiwa comparison kwenye cost benefit analysis.
Kwa mfano muwekezaji anajiuliza maswali yafuatayo:
1.Gharama za uzalishaji ni kubwa lakini je nikimudu hizo gharama za uzalishaji nikaanza uzalishaji soko lipo?
2.Na kama soko lipo je bei nitakayouza itamudu kurudisha gharama za uzalishaji na kupata faida?
3.Je wakati huo nimeshaanza kuzalisha na kuuza nikipata changamoto yoyote itatatuliwa kwa wakati au hadi nitoe rushwa tena ndio uzalishaji uendelee?hapa Kenya wametupiga gepu
4.Je nikihitaji wafanyakazi professional kwa haraka bila uzalishaji kusimamishwa nitawapata kwa haraka au hadi nikatafute watu ulaya niwalete?hapa ndipo Kenya wanapotupiga gepu
5.Je kuna malighafi zilizo tayari kwa matumizi au hata mpango tu wa miaka michache mbeleni kwamba kutakuwa na projects za kuandaa malighafi?jibu hapana
Ok, una hoja. Dennis Robert Shughuru and Strong ladg and Yoda
 
CCM ni Wajinga Imagine walikubali mkataba wa DP World wakakataa refinery ya Dangote, na details za mradi wa refinery zikiwa zimefichwa hatujui faida kiasi gani tungepata au tungekosa, ndio maana watu wanataka mabadiliko
 
Tuko kwenye vita lakini Mungu katupendelea sana Tanzania.
Kila siku najiuliza kwa nini Tanzania ni masikini?
Kwa ardhi yetu yenye rutuba inatosha kutufanya matajiri
Sasa kuna mtu kakutaza kulima? Nenda kalime upate utajiri.
 
Back
Top Bottom