Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
Maendeleo ni muhimu katika jamii za Kiislamu.
Uislamu na maendeleo ndiko kutakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu.

Kiwango cha maendeleo duni katika maeneo ya Wailslamu hapa nchini kinaonyeshwa kwa kutumia mifano iliyo hai. Maeneo mengi ya Waislamu kuna tatizo kubwa la kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Hili linawafanya wasio waislamu kuulaumu Uislamu kuwa ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa maendeleo katika maeneo husika.

Inajadiliwa, sio kwamba uislamu hauna mbinu wala elimu za kiuchumi laa, ispokuwa waislamu wenyewe wameacha kufuata misingi iliyoasisiwa na Mtume wetu Muhammada (s.a.w). Kwamba uislamu daima umekuza shughuli za kiuchumi, na biashara na kipindi cha nyuma uislamu ulikuwa unachukuliwa kuwa njia bora ya kupata riziki ya mtu. Zaidi ya hayo, dhana ya maendeleo katika Uislamu ni mchakato muhimu, ambao unaboresha ustawi wa binadamu katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na akhera. Vielelezo vya MAKKA na MADINA vinawasilishwa kama mojawapo ya njia za maendeleo katika Uislamu wetu.

Waislamu kutoka mtaa mmoja wanakutana mara 5 kwa siku (sala tano), waislamu wa kitongoji kimoja wanakutana mara 1 kwa wiki (Sala ya Ijumaa), waislamu wa mkoa mmoja wanakutana mara mbili kwa mwaka (Sala za Eid), waislamu kote duniani tena walio matajiri wanakutana mara moja kwa mwaka (Hija).

Mlolongo huo alituachia Mwenyezi Mungu s.w kupitia Mtume wetu Muhammada (s.a.w), Lakini kukutana kwetu huko hakutakua na manufaa yoyote ikiwa bado kutakuwa na ukosefu wa maendeleo kwa watu wetu.

Lengo la watu kukutana sio kuswali na kuondoka tu, watu wanatakiwa kujadili, kufahamiana, na kupanga mikakati ya kusonga mbele zaidi kielimu, kiuchumi, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. Nasio kuishia kuswali na kuondoka hata bila kupeana mikono.

Wenzetu wamechukua mfumo huo wa kukutana, leo utaona kuna jumuiya nyingi za Kikristo zinakutana kila wiki asubuhi mapema, leo utaona kuna umoja wa kimataifa (mataifa yote yanakutana) asili yake hii ni Uislamu. Lengo la kukutana misikitini ni kufanya vikao vya kheri kwa umoja wenu msonge mbele kimaendeleo.

Ifake wakati sasa misikiti iyanze kuhudumia watu na kuwafanyia watu mambo yaliyo mema, nasio watu siku zote kuihudumia misikiti. Moyo wa mtu umeumbwa kukipenda na kukithamini kile kitu kinachomjali, na moyo umeumbwa kukichukia na kukidharau kile kitu kisichomjali.

Misikiti mingi haina hata orodha (Record Keeping Books) ya kuwatambua waumini wake, idadi yao na shughuli zao. Misikiti mingi haina vipaombele katika swala la maendeleo, misikiti mingi haina orodha ya wajane, haina orodha ya mayatima, haina orodha ya wanafunzi walio kwama Masomo kwa ukata wa pesa, haina orodha ya wagonjwa, imekuwa ni sehemu ya kuswalia tu na kuondoka.
Msikiti ni kituo cha Kiislamu kinachotakiwa kuzalisha usasa wa kijamii na kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata sheria za MUNGU. Panapokuwa na dhiki inaashiria kwamba malengo ya Uislamu hayawezi kutimizwa, kwasababu watu hawajiwezi kwa kutofautiana kijamii na kiuchumi, rushwa na ukosefu wa haki. Haina faida kujenga msikiti ilihali wake za Masheikh wanazalishwa na Madaktari wa kiume, haina faida ya kujenga msikiti ilihali kuna kundi kubwa la vijana wa kiislamu wanakwama masomo kwa ukata wa pesa, haina faida ya kujenga msikiti ilihali wanawake wa kiislamu wanadhalilishwa kwenye mikopo ya Riba. Na mambo mengine ya kuudhi yanayoofanyika dhidi ya watu wetu.

Tusisahau kwamba ni kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo yalisaidia jamii za Kiislamu kujenga ustaarabu wenye mafanikio makubwa na mafanikio yaliyoonyeshwa katika kukusanya rasilimali na kuunda fursa, na ambayo ilizisaidia jamii kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi hadi karne ya kumi na tisa.

Turudi katika misingi na kanuni zetu. Muislamu kupewa msaada na Kanisa inatia aibu ilihali misikiti ipo.

frauenindermoschee.jpg



BAKIIF ISLAMIC
Kimara, Dar es salaam
 
Nani wa kumfunga paka kengele, ikiwa kiongozi mkuu wa nchi naye anaomba msaada wa kujengewa msikiti nchini mwake.

Bajeti ya ujenzi wa msikiti wa ghorofa mbili inatosha kujenga dispensary.

Ndani ya mtaa wetu pana misikiti minne mikubwa, ila huduma za afya mpaka ukimbilie mnazi mmoja
 
Nani wa kumfunga paka kengele, ikiwa kiongozi mkuu wa nchi naye anaomba msaada wa kujengewa msikiti nchini mwake.

Bajeti ya ujenzi wa msikiti wa ghorofa mbili inatosha kujenga dispensary.

Ndani ya mtaa wetu pana misikiti minne mikubwa, ila huduma za afya mpaka ukimbilie mnazi mmoja
Kuna mambo yanafanyiwa manipulation haswa kwa wanaofuatilia kwa mfano mambo kama ya kiuchumi yameelezwa hata umuhimu wa kutafuta elimu kwamba ni faradhi(kwa mwanamke na mwanaume) ila haya mambo watu wanayaacha kabisa wanafuata sehemu ndogo wanayoona nyepesi .

Kiufupi watu hawafuati uislamu wanafanya manipulation na kusoma elimu stahiki.. Alhamdulliah nimesoma taasisi mbili tofauti na zote mpaka sasa walianza na nursery schools mpaka dispensary pamoja na mradi wa kusomesha mayatima.
 
Nadhani umetumwa wewe. Uislamu unajitosheleza. Una watu wana elimu nzuri na ya kutosha.
Kujivika miwani ya mbao kwa kutokuliona tatizo sio suluhisho la tatizo. Tangu uhuru hadi sasa hatuna chuo kikuu cha maana kilicho sawasawa, tangu uhuru hadi sasa hatuna japo Maternity Hospital hata moja inayo elewaka walau kuwasaidia wakinamama wa wakiislamu. Hatuna mifumo yoyote ya kuwasaidia waumini kiuchumi, kiasi kwamba mtu akisaidiwa na kanisa inakuwa vyepesi kwake kuritadi.
 
Hii pia iende kwa wakristu,Mimi nimekuona Sana unakuta michango mingi ya ujenzi wa jengo la billions,wkt jengo lililopo linatosha kabisa hiyo pesa kwanin isitumike kuinua vipato vya watu humo humo wale wenyebiashara wawezeshwe kwa kufatiliwa kuona maendeleo yao ili kila mtu awe Sasa na uwezo km alikuwa anatoa Mia mbili aweze kutoa elfu moja na kulisha familia yake
 
Kujivika miwani ya mbao kwa kutokuliona tatizo sio suluhisho la tatizo. Tangu uhuru hadi sasa hatuna chuo kikuu cha maana kilicho sawasawa, tangu uhuru hadi sasa hatuna japo Maternity Hospital hata moja inayo elewaka walau kuwasaidia wakinamama wa wakiislamu. Hatuna mifumo yoyote ya kiuchumi, kiasi kwamba mtu akisaidia na kanisa inakuwa vyepesi kwake kuritadi.
Hakuna mtu anayeiingia ukirisito kwa kupewa msaada. Morogoro tuna chuo na shule nyingi tu. Na hospital zipo nyingi tu. Sijajua lengo lako nini. Uislamu unaongoza kwa maendeleo mengi nchini
 
Back
Top Bottom