Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Mada nzuri sana,mikoa au maeneo yenye waislam wengi kuna hali duni za maisha hali iyo maranyingi huwa inazaa vibaka,singeli,vigodoro na wazazi kupuuzia malezi na elimu kwa watoto wao.
 
Haya mambo tukisema sisi tusiokiwa waislam tunashambuliwa na kutukanwa.

Sasa hatimaye ninyi wenyewe mnauona ukweli ambao tumekuwa tukiusema mara nyingi.
Una uhakika gani, hao ni Waislamu, huku kukiwa na muendelezo wa watu maalumu, wanaotafuta kuidhoovisha Tanzania kupitia imani.

Kila siku kuda mada ya dini ukristo kuuhoji uislamu.
Na mimi baadae nitauliza swali, waliomtesa yesu, kwanini walimvua nguo na kumvisha kile kinguo.
 
Nia ya mtoa mada ni nzuri ila binafsi nilifarakiana nayo baada ya kuona jambo haswa ni la kiislam na la waislam yeye kaona pakulileta ni jf, utafikiri huku kuna chombo cha kuratibu issues za Muslims... Huku ni kama una jambo la kudarasisha au kuuliza japo pia siafiki sana maana mwisho huwa ni matusi na makufuru siku zote duuh....akiwa naimani kuwa tutajadili apate majibu wakati mpaka sasa ukute over 60% ya waliochangia hii mada hata si waislam.... Maoni yangu lakini..

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Lengo ni ujumbe ufike, kama kuna msikiti unaosimamia basi bambo yanatakiwa kubadilika au kuwashauri wasimamizi wa mambo hayo ukiwa nao karibu.
 
Una uhakika gani, hao ni Waislamu, huku kukiwa na muendelezo wa watu maalumu, wanaotafuta kuidhoovisha Tanzania kupitia imani.

Kila siku kuda mada ya dini ukristo kuuhoji uislamu.
Na mimi baadae nitauliza swali, waliomtesa yesu, kwanini walimvua nguo na kumvisha kile kinguo.
Mkuu, matatizo yaliyo jadiliwa kwenye mada, yapo au hayapo? kiuhalisia kabisa
 
Maendeleo ni muhimu katika jamii za Kiislamu.
Uislamu na mendeleo ndiko kutakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu.

Kiwango cha maendeleo duni katika maeneo ya Wailslamu hapa nchini kinaonyeshwa kwa kutumia mifano iliyo hai. Maeneo mengi ya Waislamu kuna tatizo kubwa la kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Hili linawafanya wasio waislamu kuulaumu Uislamu kuwa ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa maendeleo katika maeneo husika.

Inajadiliwa, sio kwamba uislamu hauna mbinu wala elimu za kiuchumi laa, ispokuwa waislamu wenyewe wameacha kufuata misingi iliyoasisiwa na Mtume wetu Muhammada (s.a.w). Kwamba uislamu daima umekuza shughuli za kiuchumi, na biashara na kipindi cha nyuma uislamu ulikuwa unachukuliwa kuwa njia bora ya kupata riziki ya mtu. Zaidi ya hayo, dhana ya maendeleo katika Uislamu ni mchakato muhimu, ambao unaboresha ustawi wa binadamu katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na akhera. Vielelezo vya MAKKA na MADINA vinawasilishwa kama mojawapo ya njia za maendeleo katika Uislamu wetu.

Waislamu kutoka mtaa mmoja wanakutana mara 5 kwa siku (sala tano), waislamu wa kitongoji kimoja wanakutana mara 1 kwa wiki (Sala ya Ijumaa), waislamu wa mkoa mmoja wanakutana mara mbili kwa mwaka (Sala za Eid), waislamu kote duniani tena walio matajiri wanakutana mara moja kwa mwaka (Hija).

Mlolongo huo alituachia Mwenyezi Mungu s.w kupitia Mtume wetu Muhammada (s.a.w), Lakini kukutana kwetu huko hakutakua na manufaa yoyote ikiwa bado kutakuwa na ukosefu wa maendeleo kwa watu wetu.

Lengo la watu kukutana sio kuswali na kuondoka tu, watu wanatakiwa kujadili, kufahamiana, na kupanga mikakati ya kusonga mbele zaidi kielimu, kiuchumi, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. Nasio kuishia kuswali na kuondoka hata bila kupeana mikono.

Wenzetu wamechukua mfumo huo wa kukutana, leo utaona kuna jumuiya nyingi za Kikristo zinakutana kila wiki asubuhi mapema, leo utaona kuna umoja wa kimataifa (mataifa yote yanakutana) asili yake hii ni Uislamu. Lengo la kukutana misikitini ni kufanya vikao vya kheri kwa umoja wenu msonge mbele kimaendeleo.

Ifake wakati sasa misikiti iyanze kuhudumia watu na kuwafanyia watu mambo yaliyo mema, nasio watu siku zote kuihudumia misikiti. Moyo wa mtu umeumbwa kukipenda na kukithamini kile kitu kinachomjali, na moyo umeumbwa kukichukia na kukidharau kile kitu kisichomjali.

Misikiti mingi haina hata orodha (Record Keeping Books) ya kuwatambua waumini wake, idadi yao na shughuli zao. Misikiti mingi haina vipaombele katika swala la maendeleo, misikiti mingi haina orodha ya wajane, haina orodha ya mayatima, haina orodha ya wanafunzi walio kwama Masomo kwa ukata wa pesa, haina orodha ya wagonjwa, imekuwa ni sehemu ya kuswalia tu na kuondoka.
Msikiti ni kituo cha Kiislamu kinachotakiwa kuzalisha usasa wa kijamii na kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata sheria za MUNGU. Panapokuwa na dhiki inaashiria kwamba malengo ya Uislamu hayawezi kutimizwa, kwasababu watu hawajiwezi kwa kutofautiana kijamii na kiuchumi, rushwa na ukosefu wa haki. Haina faida kujenga msikiti ilihali wake za Masheikh wanazalishwa na Madaktari wa kiume, haina faida ya kujenga msikiti ilihali kuna kundi kubwa la vijana wa kiislamu wanakwama masomo kwa ukata wa pesa, haina faida ya kujenga msikiti ilihali wanawake wa kiislamu wanadhalilishwa kwenye mikopo ya Riba. Na mambo mengine ya kuudhi yanayoofanyika dhidi ya watu wetu.

Tusisahau kwamba ni kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo yalisaidia jamii za Kiislamu kujenga ustaarabu wenye mafanikio makubwa na mafanikio yaliyoonyeshwa katika kukusanya rasilimali na kuunda fursa, na ambayo ilizisaidia jamii kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi hadi karne ya kumi na tisa.

Turudi katika misingi na kanuni zetu. Muislamu kupewa msaada na Kanisa inatia aibu ilihali misikiti ipo.

frauenindermoschee.jpg

BAKIIF ISLAMIC
Kimara, Dar es salaam
Kujenga misikiti ni dili. Kuna kitu kitaopatikana kutoka kwa mfdhili ambachoanaye initiate kujenga huo msikiti atapata, tena siyo kidogo. WE acha habari hiyo!
 
هَكِكَ هُو نِ اُشَورِ مزُرِ كويتُ سِسِ وَيِسلَمُ
 
Mkuu, matatizo yaliyo jadiliwa kwenye mada, yapo au hayapo? kiuhalisia kabisa
Msikiti ndo kituo cha waislam kuwakutanisha hapo kwenye mambo yote ya ibada na mambo mengine ya kijamii.
hapo tunapata picha kua kumbe msikiti tayari ni kituo muhimu sana kwa waislam kukutana na kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii yao.
 
Acha tujenge misikiti kwanza , maendeleo ya kumjua Allah ndo kila kitu Mali hazina maana.
Yah huku tukijisifia utajiri wa waislam kadhaa tena waarabu walioshikilia record ya utajiri ndani ya nchi huku sisi wengine hata kula yetu ya kesho hatuna uhakika nayo sembuse ya leo.
 
Yani mimi mnaniacha hoi mwaka jana mwishoni nilitembelea Dar es salaam eti pale Kawe kuanzia ukwamani I think mpaka kwenye mnara wa Clouds kuna misikiti mitatu mikubwa, yani mikubwa kweli... sasa nikajiuliza kwamba wanawaumini wengi wasingetosha kwa msikiti mmoja? Yani ni walking distance kabisa... nikajisemea si angalau basi hata huo msikiti mmoja wangejenga zahanati? Nilitafakari sana mwishoni nikainua macho yangu juu nikafanya ishara ya msalama nikamwambia Mungu NINAKUSHUKURU KWA KUNIFANYA NIWE MKRISTO, NI KWA NEEMA TU AMBAYO SI KILA MTU UMEMJALIA
 
Yah huku tukijisifia utajiri wa waislam kadhaa tena waarabu walioshikilia record ya utajiri ndani ya nchi huku sisi wengine hata kula yetu ya kesho hatuna uhakika nayo sembuse ya leo.

Shukuru kwa kila Jambo

Msitamani Mali Ambazo mnakufa na kuziacha
 
Hakuna mtu anayeiingia ukirisito kwa kupewa msaada. Morogoro tuna chuo na shule nyingi tu. Na hospital zipo nyingi tu. Sijajua lengo lako nini. Uislamu unaongoza kwa maendeleo mengi nchini
Sijui unapinga ni na kwa sababu gani maana mwenzio aliyoyasema siyo kwamba hayaoni anayaona wewe unataja maendeleo ya hapo Morogoro ina maana waislam wapo Morogoro tu?
 
BAKIIF Islamic hata huku kwenye ukristo hasa PENTECOSTALS kazi yetu kubwa kilasiku tunawaza kufungua makanisa na kufungulia mziki Kwa fujo ....ufike muda walokole nao wajenge hospital,shule na huduma zingine za jamii kama ilivyo Kwa katoliki na kkkt
Hao ktk bold wanatoa sana sadaka na michango mbalimbali but ninyi huwa mnawacheka kwamba ni wajinga wanapelekea hela mapadre na wachungaji.

Mkiiga kwao mkubali kuwa watoaji.
 
Back
Top Bottom