Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Bukoba Mjini pana misikiti mingi kuliko mahitaji ya waumini. Mingine hata kuifanyia usafi ni tatizo. Majani hadi mlangoni

Ni heri sasa kujikita katika kujali mahitaji ya kimwili ya waumini kuliko kuendeleza mashindano ya kujenga misikiti.
 
Kujivika miwani ya mbao kwa kutokuliona tatizo sio suluhisho la tatizo. Tangu uhuru hadi sasa hatuna chuo kikuu cha maana kilicho sawasawa, tangu uhuru hadi sasa hatuna japo Maternity Hospital hata moja inayo elewaka walau kuwasaidia wakinamama wa wakiislamu. Hatuna mifumo yoyote ya kuwasaidia waumini kiuchumi, kiasi kwamba mtu akisaidiwa na kanisa inakuwa vyepesi kwake kuritadi.
Na mkijenga hospitaal yakhe, zisiwe ni kuahudumia waislamu kama ulivyoandika hapo juu! Mfanye kama wenzenu Wakristo, hakuna ubaguzi. Na mashule hivyo hivyo.

Chuo kikuu cha Morogoro kimekuwa madrasa tul islam ubaguzi tele.
 
Wanaojenga misikiti sio hawa wazawa titii ni waarabu wa nje toka nchi za kiislam. Wazawa wanajenga ya matope huko vijijini na wa mijini wanajenga vijengo vidogovidogo vya kawaida tu, ila vimisikiti vingi vimejengwa kando ya barabara kuu maeneo ya vijijini, hivi vimisikiti vingi kila baada ya kilometa chache maporini havina waumini wa kusali. Ni misaada toka nje, misikiti mingi hata kwenye maeneo ambayo hayana waislamu wengi wana bahati nchi ni ya amani na uhuru wa kuabudu hakuna wa kuibomoa hiyo misikiti iliyojengwa kando ya barabara kuu huko maporini vijijini. Hivi katika nchi za kiislam inawezekana vipi makanisa yakajengwa kwa wingi porini na yakabaki salama? Nchi ya amani na uhuru wa kuabudu hii
 
Ukifunga ramadhani yote una pepo kama utakutana na tulqadir
Ukijenga msikuti una pepo
 
Maendeleo ni muhimu katika jamii za Kiislamu.
Uislamu na mendeleo ndiko kutakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu.

Kiwango cha maendeleo duni katika maeneo ya Wailslamu hapa nchini kinaonyeshwa kwa kutumia mifano iliyo hai. Maeneo mengi ya Waislamu kuna tatizo kubwa la kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Hili linawafanya wasio waislamu kuulaumu Uislamu kuwa ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa maendeleo katika maeneo husika.

Inajadiliwa, sio kwamba uislamu hauna mbinu wala elimu za kiuchumi laa, ispokuwa waislamu wenyewe wameacha kufuata misingi iliyoasisiwa na Mtume wetu Muhammada (s.a.w). Kwamba uislamu daima umekuza shughuli za kiuchumi, na biashara na kipindi cha nyuma uislamu ulikuwa unachukuliwa kuwa njia bora ya kupata riziki ya mtu. Zaidi ya hayo, dhana ya maendeleo katika Uislamu ni mchakato muhimu, ambao unaboresha ustawi wa binadamu katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na akhera. Vielelezo vya MAKKA na MADINA vinawasilishwa kama mojawapo ya njia za maendeleo katika Uislamu wetu.

Waislamu kutoka mtaa mmoja wanakutana mara 5 kwa siku (sala tano), waislamu wa kitongoji kimoja wanakutana mara 1 kwa wiki (Sala ya Ijumaa), waislamu wa mkoa mmoja wanakutana mara mbili kwa mwaka (Sala za Eid), waislamu kote duniani tena walio matajiri wanakutana mara moja kwa mwaka (Hija).

Mlolongo huo alituachia Mwenyezi Mungu s.w kupitia Mtume wetu Muhammada (s.a.w), Lakini kukutana kwetu huko hakutakua na manufaa yoyote ikiwa bado kutakuwa na ukosefu wa maendeleo kwa watu wetu.

Lengo la watu kukutana sio kuswali na kuondoka tu, watu wanatakiwa kujadili, kufahamiana, na kupanga mikakati ya kusonga mbele zaidi kielimu, kiuchumi, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. Nasio kuishia kuswali na kuondoka hata bila kupeana mikono.

Wenzetu wamechukua mfumo huo wa kukutana, leo utaona kuna jumuiya nyingi za Kikristo zinakutana kila wiki asubuhi mapema, leo utaona kuna umoja wa kimataifa (mataifa yote yanakutana) asili yake hii ni Uislamu. Lengo la kukutana misikitini ni kufanya vikao vya kheri kwa umoja wenu msonge mbele kimaendeleo.

Ifake wakati sasa misikiti iyanze kuhudumia watu na kuwafanyia watu mambo yaliyo mema, nasio watu siku zote kuihudumia misikiti. Moyo wa mtu umeumbwa kukipenda na kukithamini kile kitu kinachomjali, na moyo umeumbwa kukichukia na kukidharau kile kitu kisichomjali.

Misikiti mingi haina hata orodha (Record Keeping Books) ya kuwatambua waumini wake, idadi yao na shughuli zao. Misikiti mingi haina vipaombele katika swala la maendeleo, misikiti mingi haina orodha ya wajane, haina orodha ya mayatima, haina orodha ya wanafunzi walio kwama Masomo kwa ukata wa pesa, haina orodha ya wagonjwa, imekuwa ni sehemu ya kuswalia tu na kuondoka.
Msikiti ni kituo cha Kiislamu kinachotakiwa kuzalisha usasa wa kijamii na kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata sheria za MUNGU. Panapokuwa na dhiki inaashiria kwamba malengo ya Uislamu hayawezi kutimizwa, kwasababu watu hawajiwezi kwa kutofautiana kijamii na kiuchumi, rushwa na ukosefu wa haki. Haina faida kujenga msikiti ilihali wake za Masheikh wanazalishwa na Madaktari wa kiume, haina faida ya kujenga msikiti ilihali kuna kundi kubwa la vijana wa kiislamu wanakwama masomo kwa ukata wa pesa, haina faida ya kujenga msikiti ilihali wanawake wa kiislamu wanadhalilishwa kwenye mikopo ya Riba. Na mambo mengine ya kuudhi yanayoofanyika dhidi ya watu wetu.

Tusisahau kwamba ni kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo yalisaidia jamii za Kiislamu kujenga ustaarabu wenye mafanikio makubwa na mafanikio yaliyoonyeshwa katika kukusanya rasilimali na kuunda fursa, na ambayo ilizisaidia jamii kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi hadi karne ya kumi na tisa.

Turudi katika misingi na kanuni zetu. Muislamu kupewa msaada na Kanisa inatia aibu ilihali misikiti ipo.

frauenindermoschee.jpg

BAKIIF ISLAMIC
Kimara, Dar es salaam
Tatizo kubwa la Uislamu tangu karne za giza ni kutaka kushindana na Ukristo. Hii imefanya Uislamu kukosa dira na sababu nzuri za kufanya mambo ya msingi katika jamii.

Utaona kabisa waislamu wanafanya juu chini na kutumia mabilioni ilimradi tu wanajipenyeza kwenye ngome za wakristo! Kujenga misikiti mita mbili kutoka barabara kuu ili tu watu waone kwamba miskiti imejaa njia yote.

Mpeleke huduma ndani vijijini wapo wengi wasio na maji, shule, nk acheni mashindano yasiyo na tija kwa umma.
 
Kujivika miwani ya mbao kwa kutokuliona tatizo sio suluhisho la tatizo. Tangu uhuru hadi sasa hatuna chuo kikuu cha maana kilicho sawasawa, tangu uhuru hadi sasa hatuna japo Maternity Hospital hata moja inayo elewaka walau kuwasaidia wakinamama wa wakiislamu. Hatuna mifumo yoyote ya kuwasaidia waumini kiuchumi, kiasi kwamba mtu akisaidiwa na kanisa inakuwa vyepesi kwake kuritadi.
Wasiowaislam wanajenga hospital za kuhudumia watu wote wewe unasema za kuhudumia waislam...Hamuwezi kufanikiwa kwa mawazo hayo

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Mambo yanayowangusha waislam kwenye maendeleo ya kaya zao ni:
1 polygamy: ni ngumu kiendelea kama huna mahusiano stable ya familia hii onazaa la watoto ambao hawana misingi imara ya kifamilia kwa hiyo kukosa uelekeo sahihii.pia resources nyingi hutumika kwenye recurrent expenditure za kuwa na kuhudumja wake

2. Msisistizo mdogo kwenye secular education.
3.kuamini sana kwenye ushirikiana
 
Msikiti ndio kituo Cha uislam,ndio msingi wa kuhuisha uislam
Tatizo ni kuwa uislam halisi umeachwa, pasipo kusimamisha utawala wa kiislam hayo uongeayo ni ndoto
Simamisha uislam msikiti isimame
 
Umetoa bonge LA point Ila afrika tumekuwa mbuzi Sana siku hizi , mwarabu au mzungu akisema hiki mbio tunafuata ....dini bila maendeleo ni borderline cult tu , waislamu tujengane ,tuanzishe mbinu za kuzalisha utajiri au ajira kwa vijana kwa ss miskiti imetosha
 
Washamba hao point yao watakuja na MWENGE catholic na hospital ya Muhimbili kama unabisha ndo defensive mechanism yao ...Wakati ni wajinga wanawachangia mapandre na maaskofu then wao ndo wamiliki wa izo shule na vyuo
Hawa ndio aina ya waislam mtoa mada anaowazungumzia....Umesaidia kuprove hoja ya mtoa mada ambaye ni mwislam mwenzako.

Mimi nitakutajia Vyuo vikuu vya Wakristo hapa Tz.

1. St Augustine University
2. Tumaini University
3. St John's University
4. University of Arusha
5. St Joseph University

Na Kwenye vyuo hivi, KUNA WAISLAM KIBAO wanasoma na wamesoma humo.

Ukiachana na MUM cha Morogoro, Waislam mna chuo kikuu kingine?
 
Ivyo vyuo hapo vyote takataka kama vyuo vya kata hamna cha maana..siwezi kusoma.

Unaongelea vyuo wangapi wanafaulu wanashindwa kulipa ada..Hapa ni ishu za kusaidiana tunajua majority wengi ni maskini sasa utakwamua vip .

Ivyo kweny list narudia ni takataka Tena havina kitu kabisa..
 
Una uhakika gani, hao ni Waislamu, huku kukiwa na muendelezo wa watu maalumu, wanaotafuta kuidhoovisha Tanzania kupitia imani.

Kila siku kuda mada ya dini ukristo kuuhoji uislamu.
Na mimi baadae nitauliza swali, waliomtesa yesu, kwanini walimvua nguo na kumvisha kile kinguo.
Wewe umeshapanic.... Mada inahusu maendeleo na Waislam wewe unakuja na habari za Yesu.

Nyie ndio wale mnaozungumziwa na mtoa mada(mwislam mwenzenu)
 
Umenisemea Allah anisamehe mwanangu baba ake amempeleka seminary ya masista maana hakuna shule nzuri ya kiislamu ya wasichana,ni mtihani mtupuu

Binafsi shule ya msingi alikuwepo dada mmoja muislam anaitwa mwajuma Rashid Mbonde. Alikuwa kichwa kweli kweli.. la saba alifaulu na kupangiwa kuanza form one katika shule ya vipaji kilakala.. ila wazazi wake walimpeleka shule ya masista st francis mbeya. Na alipofika st francis na uislamu wake bado form 4 alifaulu kwa div 1 pts 8 na A level akaenda Marian galz.

Sasa hivi ni daktari huyo dada.

Wazazi wake japo ni waislamu waliamua kumsomesha shule za masista sababu hakuna shule za waislamu zilizo vizuri ki academic
 
Ivyo vyuo hapo vyote takataka kama vyuo vya kata hamna cha maana..siwezi kusoma.

Unaongelea vyuo wangapi wanafaulu wanashindwa kulipa ada..Hapa ni ishu za kusaidiana tunajua majority wengi ni maskini sasa utakwamua vip .

Ivyo kweny list narudia ni takataka Tena havina kitu kabisa..
Hahaha... Wewe Huwezi kusoma wakati humo kwenye hivyo vyuo Waislam wenzako wamejazana kibao!!!

Na kwenye list yangu nilisahau kutaja chuo kikuu cha sita.

6. Sebastian Kolowa Memorial University

Na nimekuuliza swali naona unajifanya hulioni, ukitoa MUM morogoro (ambacho mlipewa na Mkatoliki Mkapa), Waislam Mna chuo gani kingine hapa Tanzania?
 
Maendeleo ni muhimu katika jamii za Kiislamu.
Uislamu na mendeleo ndiko kutakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu.

Kiwango cha maendeleo duni katika maeneo ya Wailslamu hapa nchini kinaonyeshwa kwa kutumia mifano iliyo hai. Maeneo mengi ya Waislamu kuna tatizo kubwa la kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Hili linawafanya wasio waislamu kuulaumu Uislamu kuwa ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa maendeleo katika maeneo husika.

Inajadiliwa, sio kwamba uislamu hauna mbinu wala elimu za kiuchumi laa, ispokuwa waislamu wenyewe wameacha kufuata misingi iliyoasisiwa na Mtume wetu Muhammada (s.a.w). Kwamba uislamu daima umekuza shughuli za kiuchumi, na biashara na kipindi cha nyuma uislamu ulikuwa unachukuliwa kuwa njia bora ya kupata riziki ya mtu. Zaidi ya hayo, dhana ya maendeleo katika Uislamu ni mchakato muhimu, ambao unaboresha ustawi wa binadamu katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na akhera. Vielelezo vya MAKKA na MADINA vinawasilishwa kama mojawapo ya njia za maendeleo katika Uislamu wetu.

Waislamu kutoka mtaa mmoja wanakutana mara 5 kwa siku (sala tano), waislamu wa kitongoji kimoja wanakutana mara 1 kwa wiki (Sala ya Ijumaa), waislamu wa mkoa mmoja wanakutana mara mbili kwa mwaka (Sala za Eid), waislamu kote duniani tena walio matajiri wanakutana mara moja kwa mwaka (Hija).

Mlolongo huo alituachia Mwenyezi Mungu s.w kupitia Mtume wetu Muhammada (s.a.w), Lakini kukutana kwetu huko hakutakua na manufaa yoyote ikiwa bado kutakuwa na ukosefu wa maendeleo kwa watu wetu.

Lengo la watu kukutana sio kuswali na kuondoka tu, watu wanatakiwa kujadili, kufahamiana, na kupanga mikakati ya kusonga mbele zaidi kielimu, kiuchumi, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. Nasio kuishia kuswali na kuondoka hata bila kupeana mikono.

Wenzetu wamechukua mfumo huo wa kukutana, leo utaona kuna jumuiya nyingi za Kikristo zinakutana kila wiki asubuhi mapema, leo utaona kuna umoja wa kimataifa (mataifa yote yanakutana) asili yake hii ni Uislamu. Lengo la kukutana misikitini ni kufanya vikao vya kheri kwa umoja wenu msonge mbele kimaendeleo.

Ifake wakati sasa misikiti iyanze kuhudumia watu na kuwafanyia watu mambo yaliyo mema, nasio watu siku zote kuihudumia misikiti. Moyo wa mtu umeumbwa kukipenda na kukithamini kile kitu kinachomjali, na moyo umeumbwa kukichukia na kukidharau kile kitu kisichomjali.

Misikiti mingi haina hata orodha (Record Keeping Books) ya kuwatambua waumini wake, idadi yao na shughuli zao. Misikiti mingi haina vipaombele katika swala la maendeleo, misikiti mingi haina orodha ya wajane, haina orodha ya mayatima, haina orodha ya wanafunzi walio kwama Masomo kwa ukata wa pesa, haina orodha ya wagonjwa, imekuwa ni sehemu ya kuswalia tu na kuondoka.
Msikiti ni kituo cha Kiislamu kinachotakiwa kuzalisha usasa wa kijamii na kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata sheria za MUNGU. Panapokuwa na dhiki inaashiria kwamba malengo ya Uislamu hayawezi kutimizwa, kwasababu watu hawajiwezi kwa kutofautiana kijamii na kiuchumi, rushwa na ukosefu wa haki. Haina faida kujenga msikiti ilihali wake za Masheikh wanazalishwa na Madaktari wa kiume, haina faida ya kujenga msikiti ilihali kuna kundi kubwa la vijana wa kiislamu wanakwama masomo kwa ukata wa pesa, haina faida ya kujenga msikiti ilihali wanawake wa kiislamu wanadhalilishwa kwenye mikopo ya Riba. Na mambo mengine ya kuudhi yanayoofanyika dhidi ya watu wetu.

Tusisahau kwamba ni kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo yalisaidia jamii za Kiislamu kujenga ustaarabu wenye mafanikio makubwa na mafanikio yaliyoonyeshwa katika kukusanya rasilimali na kuunda fursa, na ambayo ilizisaidia jamii kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi hadi karne ya kumi na tisa.

Turudi katika misingi na kanuni zetu. Muislamu kupewa msaada na Kanisa inatia aibu ilihali misikiti ipo.

frauenindermoschee.jpg

BAKIIF ISLAMIC
Kimara, Dar es salaam
Pamoja na maoni au Ushauri mzuri tegemea zaidi matusi na kebehi kutoka kwa Waislam
 
Hahaha... Wewe Huwezi kusoma wakati humo kwenye hivyo vyuo Waislam wenzako wamejazana kibao!!!

Na nimekuuliza swali naona unajifanya hulioni, ukitoa MUM morogoro (ambacho mlipewa na Mkatoliki Mkapa), Waislam Mna chuo gani kingine hapa Tanzania?
Wataka vyuo vya dini ili iweje Zanzibar hakuna..Mbona ivyo watu wanasoma mchanganyiko !! Kwani ivyo vyuo watu wanasoma bure?

Izo ni takataka kwa watu wanaopenda kitongo ila vyuo vikubwa vinajulikana sio izo takataka mara ohh kaanzisha mkapa ..Hata Bakwata kaanzisha Nyerere.

Izo ni biashara za watu maana wanapokea ada na figisu kibao watoto jawadisco ili waendelee kula ada.

Izo ni takataka kabisa ...ni milimi ya michango yenu walala hoi mnatao then watu wanafanya biashara
 
Swali langu ni rahisi sana... Acha Blah blah jibu nilichokuuliza.

Wakristo wana Vyuo vikuu visivyopungua SITA hapa Tanzania(nimeviorodhesha hapo juu)

Sasa turudi kwa waislam, Ukitoa chuo kikuu cha morogoro (MUM) Mlichopewa na Rais Mkatoliki Mkapa, Ninyi Waislam mna vyuo vikuu vingapi?
 
Wataka vyuo vya dini ili iweje Zanzibar hakuna..Mbona ivyo watu wanasoma mchanganyiko !! Kwani ivyo vyuo watu wanasoma bure?

Izo ni takataka kwa watu wanaopenda kitongo ila vyuo vikubwa vinajulikana sio izo takataka mara ohh kaanzisha mkapa ..Hata Bakwata kaanzisha Nyerere.

Izo ni biashara za watu maana wanapokea ada na figisu kibao watoto jawadisco ili waendelee kula ada.

Izo ni takataka kabisa ...ni milimi ya michango yenu walala hoi mnatao then watu wanafanya biashara
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hawa ndio waislam mtoa mada anao wazungumzia.

Kwa mentality hii, Waislam mna kazi kwelikweli kujikwamua kutoka hapo mlipo
 
Back
Top Bottom