Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Kujivika miwani ya mbao kwa kutokuliona tatizo sio suluhisho la tatizo. Tangu uhuru hadi sasa hatuna chuo kikuu cha maana kilicho sawasawa, tangu uhuru hadi sasa hatuna japo Maternity Hospital hata moja inayo elewaka walau kuwasaidia wakinamama wa wakiislamu. Hatuna mifumo yoyote ya kuwasaidia waumini kiuchumi, kiasi kwamba mtu akisaidiwa na kanisa inakuwa vyepesi kwake kuritadi.
Shida yenu inaanziaga hapo."Kuwasaidia akina mama wa kiisilamu" na si humanity.Hata taasisi nyingi mnazozianzisha huwa zinafail hapo.Ubaguzi ubaguzi ubaguzi
 
Nadhani umetumwa wewe. Uislamu unajitosheleza. Una watu wana elimu nzuri na ya kutosha.
Ametumwa na nani?

Yeye maelezo yake yamewekwa kwa mtindo wa hoja. Unapojibu, jibu kwa hoja ili kuendeleza mjadala chanya.

Unaposema Uislam umejitosheleza, sidhani kama yeye kuna mahali amesema haujajitosheleza, points zake hazijajikita kwenye Uislam, bali kwa waislam, kwa namna wanayo handle mambo.

Ni kweli waislam wenye elimu wako wengi sana, hata nchi hii peke yake, ukitaja matajiri, orodha itajaa waislam, ila impact yao ni ipi?
 
Kujivika miwani ya mbao kwa kutokuliona tatizo sio suluhisho la tatizo. Tangu uhuru hadi sasa hatuna chuo kikuu cha maana kilicho sawasawa, tangu uhuru hadi sasa hatuna japo Maternity Hospital hata moja inayo elewaka walau kuwasaidia wakinamama wa wakiislamu. Hatuna mifumo yoyote ya kuwasaidia waumini kiuchumi, kiasi kwamba mtu akisaidiwa na kanisa inakuwa vyepesi kwake kuritadi.
Talaka imepewa kipaumbele utadhani kitu cha maana.

Yaani msisitizo umewekwa kwenye talaka mpaka mabaraza ya kutetea Talaka <wajumbe wanaume tupu, huku wahanga wakubwa wakiwa wanawake na watoto>

Ila uwezeshi wa waumini kiuchumi nadra sana
 
Nadhani umetumwa wewe. Uislamu unajitosheleza. Una watu wana elimu nzuri na ya kutosha.
Umeakisi waislamu wengi sana wa Africa ambao sio open minded,hili ni tatzo ambalo waislamu tupo nalo miaka yote ushauri wa kujenga unaonekana ni ukafiri na kinyume na uislamu,sasa sijajua suala la elimu hapa limeingiaje,

Kwa ufupi kama hujamuelewa ni kwamba kuwa na visima vingi vya maji katika jumuiya ya waislamu ni bora zaidi kuliko kuwa na misikiti minne ya kisasa katika eneo hilo..
Islamic Foundation wale jamaa wa Morogoro naona na wao kwa sasa wamestick kufanya hivi baada ya kujenga misikiti mingi kwa miaka yote waliyokuwepo..kwa sasa wanajenga mashule,visima vingi sana kuliko misikiti
 
Hii pia iende kwa wakristu,Mimi nimekuona Sana unakuta michango mingi ya ujenzi wa jengo la billions,wkt jengo lililopo linatosha kabisa hiyo pesa kwanin isitumike kuinua vipato vya watu humo humo wale wenyebiashara wawezeshwe kwa kufatiliwa kuona maendeleo yao ili kila mtu awe Sasa na uwezo km alikuwa anatoa Mia mbili aweze kutoa elfu moja na kulisha familia yake

Yani ni pande zote mbili tujitafakari,mada nzuri sana kwa wakristu na waislam pia
 
Uzi umeshaharibika pamoja na nia safi ya mtoa mada.
Nia ya mtoa mada ni nzuri ila binafsi nilifarakiana nayo baada ya kuona jambo haswa ni la kiislam na la waislam yeye kaona pakulileta ni jf, utafikiri huku kuna chombo cha kuratibu issues za Muslims... Huku ni kama una jambo la kudarasisha au kuuliza japo pia siafiki sana maana mwisho huwa ni matusi na makufuru siku zote duuh....akiwa naimani kuwa tutajadili apate majibu wakati mpaka sasa ukute over 60% ya waliochangia hii mada hata si waislam.... Maoni yangu lakini..



Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Nani wa kumfunga paka kengele, ikiwa kiongozi mkuu wa nchi naye anaomba msaada wa kujengewa msikiti nchini mwake.

Bajeti ya ujenzi wa msikiti wa ghorofa mbili inatosha kujenga dispensary.

Ndani ya mtaa wetu pana misikiti minne mikubwa, ila huduma za afya mpaka ukimbilie mnazi mmoja
Ni tatizo, ndio hilo litatuliwe
 
Haya mambo tukisema sisi tusiokiwa waislam tunashambuliwa na kutukanwa.

Sasa hatimaye ninyi wenyewe mnauona ukweli ambao tumekuwa tukiusema mara nyingi.
Watu wanatakiwa kurudi katika misingi ya dini na mafundisho yake, dini ni maisha
 
Kuna mambo yanafanyiwa manipulation haswa kwa wanaofuatilia kwa mfano mambo kama ya kiuchumi yameelezwa hata umuhimu wa kutafuta elimu kwamba ni faradhi(kwa mwanamke na mwanaume) ila haya mambo watu wanayaacha kabisa wanafuata sehemu ndogo wanayoona nyepesi .

Kiufupi watu hawafuati uislamu wanafanya manipulation na kusoma elimu stahiki.. Alhamdulliah nimesoma taasisi mbili tofauti na zote mpaka sasa walianza na nursery schools mpaka dispensary pamoja na mradi wa kusomesha mayatima.
Hakika, umezungumza jambo la mantiki sana
 
Back
Top Bottom