Turudi nyuma kidogo mgogoro wa DP World

Turudi nyuma kidogo mgogoro wa DP World

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Unganisha Dots, utagundua Uteuzi wa Kitila Mkumbo una maana gani, taifa lilianza kutengenezwa na kuwambwa tangu tulipotangaza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Zingati tarehe ya mkutano huu, mipango ilipikwa miaka mingi nyuma...

Kwamsiojua hawa ndio walimtengeneza Magufuli akakataa mradi wa UBIA wa Tanzania, Wachina na Omani wa kujenga Bandari ya Bagamoyo ambayo ingekuwa ndio bandari kubwa kuliko zote Afrika na ingekuwa ndio bandari yenye ushinda na Bandari ya Dubai huko Falme za Kiarabu ambayo mwekezaji mkuu ni Marekani... Kisha masharti yaleyale waliyoyakataa kwenye mradi wa Bagamoyo, ndio yakaletwa kwenye bandari ya Dar. Enzi za Magufuli, Kitila ndiye alitumwa kubadili dili la JK toka Bagamoyo kuja Babdari Dar, kumbuka JPM ndiye aliyefuta makubaliano ya Exim Bank China na JK kwenye SGR na kuyachepusha kuyapeleka Uturuki kwa gharama ya ziada toka 5% loan interest rate hadi 9%.

Alifuta mpango wa JK akijua tayari alikuwa na cut yake hivyo yeye asingeambulia na ndiyo maana SGR imekuwa ghali sana tofauti na initial plan. Masharti ya Exim Bank China ilikuwa watoe mkopo wa 5% interest lakini contractor atoke kwao sisi tutafute consulting engineer, JPM baada ya kuingia akaona upepo unampita, akafuta hayo makubaliano kama alivyofuta ya Bagamoyo na Wachina nao wakafuta mkopo. Funny enough waturuki wa JPM walipochukua tender wakatafuta financier, kwa hiyo wanapata faida kwenye contract na ile extra 4% interest on loan.

Katikati ya vita vya wanaccm kundi la tule na kundi la tukose wote, ndipo Ujasusi wa kiuchumi wa Marekani unajitwalia utukufu. Someni na mjue ulimwengu wa Ujasusi wa kiuchumi, Vita vya kiuchumi vya China vs USA vimepiganwa Tanzania... Na hapa USA kashinda... Bandari ya Dubai sasa haina mmshindani tena toka Afrika.🤣

IMG_20230705_224650_209.jpg
 
Masilahi ya Tanzania kwenye mkataba wa DP world yako wapi?

Mbona hili swali linazuungukwa sana na nyie wajinga?

Na kumbuka ule mradi MM ukapigwa kikumbo kikuu. Khalafu wajasiria siasa wakaja na ukawa ambao kauli mbiu yake ilikuwa hedikopta kubadili gea angani. Lakini umewagharimu kwelikweli na chamoto walikipata.
 
Imenishangaza kuona Yericko tuliekuwa tunambeza humu kajitokeza angalau kuona kitu beyond kanzu na waarabu...

Wakati kina Mbowe na Slaa na Lissu wanamsikiliza Pengo na kuona waarabu "wanakuja kujenga misikiti na kueneza dini au kurudisha utumwa"... Yericko kaenda ndani zaidi kaja angalau na theory tofauti kabisa...inayofikirisha....

In the end Yericko kajitokeza kama mtu mwenye akili kuliko Mbowe na Slaa na Lissu....

A lot has changed in Tanzania's politics....a lot ....
 
Unganisha Dots, utagundua Uteuzi wa Kitila Mkumbo una maana gani, taifa lilianza kutengenezwa na kuwambwa tangu tulipotangaza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Zingati tarehe ya mkutano huu, mipango ilipikwa miaka mingi nyuma...

Hii hoja binafis naona umechemka big time, yaani mtu aache 5% interest akimbilie 9% interest afu huyo aliepelekewa wa 9% ye akaenda kumfuata wa 5% kisha wakakubaliana ampe 5% yeye achukue 4%? Yaani kwamba JPM alikuwa level za akili kama hawa wanaompa DP World kila kitu for free?

Ye JPM hata hakujishughulisha kutafta watoaji wa chini ya iyo 9% ila wewe ndo unawajua waliyoyafanya daaah, kuna ujuaji mwingine huwa ni kama kujua kusoma kizani. Acha kudanganya raia, Jiwe alikuwa anasoma sio kusema document ikienda kwake ye anampasia Waziri wake ndo aipitie iyo big NO. Wote tunajua aliyoyafanya MwanChato acha kuwaadaa raia bhana kwa mtindo wa kichawa
 
Imenishangaza kuona Yericko tuliekuwa tunambeza humu kajitokeza angalau kuona kitu beyond kanzu na waarabu...

Wakati kina Mbowe na Slaa na Lissu wanamsikiliza Pengo na kuona waarabu "wanakuja kujenga misikiti na kueneza dini au kurudisha utumwa"... Yericko kaenda ndani zaidi kaja angalau na theory tofauti kabisa...inayofikirisha....

In the end Yericko kajitokeza kama mtu mwenye akili kuliko Mbowe na Slaa na Lissu....

A lot has changed in Tanzania's politics....a lot ....
Tokea wananchi wazalendo wa Tanzania waanze kuhoji maslahi ya Tanzania kwenye makubaliano kati ya Tanzania na DPW imekufanya ukachanganyikiwa kwelikweli, au wewe ndiye mkurugenzi wa kampuni wa DPW unikumbuke na mimi kwenye ajira ya kusimamia mifumo ya TEHAMA.
 
Imenishangaza kuona Yericko tuliekuwa tunambeza humu kajitokeza angalau kuona kitu beyond kanzu na waarabu...

Wakati kina Mbowe na Slaa na Lissu wanamsikiliza Pengo na kuona waarabu "wanakuja kujenga misikiti na kueneza dini au kurudisha utumwa"... Yericko kaenda ndani zaidi kaja angalau na theory tofauti kabisa...inayofikirisha....

In the end Yericko kajitokeza kama mtu mwenye akili kuliko Mbowe na Slaa na Lissu....

A lot has changed in Tanzania's politics....a lot ....
Mvaa kobazi katika ubora wako

Hata umtaje Pengo mara elfu, Pengo mwenyewe au Kanisa kwa ujumla haliwezi fyata mkia 'na unalijua hili kwani hamjaanza leo hizo harakati'
 
Unganisha Dots, utagundua Uteuzi wa Kitila Mkumbo una maana gani, taifa lilianza kutengenezwa na kuwambwa tangu tulipotangaza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Zingati tarehe ya mkutano huu, mipango ilipikwa miaka mingi nyuma...
Katika kelele zooote za DP World zianze wewe ndiyo umekuja na hoja fikirishi. Wengine wote pamoja na usomi wao wa majigambo lakini wamekuwa wanabwabwaja na kupayuka. What you have written here seems to be the most credible reason why DP World acquires various ports, especially African ports.

Tulisema huko nyuma kitendo cha JPM kudanganywa kuhusu ujenzi wa Mega Port ya Bagamoyo ni pigo kubwa kwa Tanzania. Na hii ndiyo sababu kubwa ya kijasusi kwa DP World kutaka wajulishwe fursa za kibandari Tanzania, tofauti na wengi wanavyodhani. Maana yake ni kuwa DP World atacheza game-tactics kuzuia credible investor kwenye bandari ya Bagamoyo ili pasijengwe Bandari shindani.

Nakubaliana na wewe pia, haingii akilini kutokuwa na mkono wa Marekani kwenye deals za DP World. Marekani ana kawaida ya kutengeneza hadi washindani ili kudhibiti maadui wake. Amefanya sana trick hizi Asia kule.
 
Katika kelele zooote za DP World zianze wewe ndiyo umekuja na hoja fikirishi. Wengine wote pamoja na usomi wao wa majigambo lakini wamekuwa wanabwabwaja na kupayuka. What you have written here seems to be the most credible reason why DP World acquires various ports, especially African ports. Tulisema huko nyuma kitendo cha JPM kudanganywa kuhusu ujenzi wa Mega Port ya Bagamoyo ni pigo kubwa kwa Tanzania. Na hii ndiyo sababu kubwa ya kijasusi kwa DP World kutaka wajulishwe fursa za kibandari Tanzania, tofauti na wengi wanavyodhani. Maana yake ni kuwa DP World atacheza game-tactics kuzuia credible investor kwenye bandari ya Bagamoyo ili pasijengwe Bandari shindani.
Ni wapumbavu sana watakaoingia mkataba wa masharti ya kipumbavu namna hiyo
 
Unganisha Dots, utagundua Uteuzi wa Kitila Mkumbo una maana gani, taifa lilianza kutengenezwa na kuwambwa tangu tulipotangaza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Zingati tarehe ya mkutano huu, mipango ilipikwa miaka mingi nyuma...
Unaweza kuweka aina zote za 'spinning', ulizojaliwa kuzitumia katika maswala haya; kisichobadilika ni kwamba uhuru wetu siyo wa kuchezewa na mtu yeyote yule, awe toka Marekani, Uarabuni, Uchina na kwingine kote duniani.

Kinachohitajika, ni wazalendo wa nchi hii kusimama na kuelewa haya yote yanavyoinyemelea nchi yetu na kuyasemea ili wananchi wayajue kwa jinsi yalivyo.

Ni wananchi pekee ndio watakaoamua hatma ya ujinga huu.

Kwa hiyo, kwa taarifa yako na wengineo, Mmarekani hajashinda vita yoyote hapa, na wala mChina hajashindwa chochote. Msindi atakuwa ni mTanzania mwenyewe.

Hawa wanaotumika kutuhujumu ndio tunaotakiwa kupambana nao sisi wenyewe; na tutawashinda tu.
 
Mada hii ni beyond kidogo kwa watu ambao hamna knowledge ya global strategic economic intelligence.
Unahimiza "global strategic economic intelligence", na wala huoni la maana na "national strategic economic intelligence"?
Hiyo 'global' itakupeleka wapi kama hata nyumbani kwako ni mbumbumbu?

Mnatumia maneno haya kuwalaza watu akili tu basi!
 
Hahaha. Ni vitu vinavyohusiana. Unatumia understanding ya global intelligence kunufaisha au kuathiri national strategic economic intelligence.
 
Back
Top Bottom