Turudi nyuma kidogo mgogoro wa DP World

Mkuu hata hapo kwenye demokrasia mpe credit.
Angalia nchi aliipokea vipi kutoka kwa Kikwete?
Migomo,maandamano,wanasiasa kususa na kutoka bungeni,mapigano polisi na raia wakichonganishwa na wanasiasa kwa mikutano ya kila siku.

ILIMLAZIMU afanye vile ili kutengeneza hishma kati ya serikali,wananchi na wanasiasa.

TO me the man was right kwenye demokrasia japo kama mwanadamu hakukosa kasoro
 
Unahimiza "global strategic economic intelligence", na wala huoni la maana na "national strategic economic intelligence"?
Hiyo 'global' itakupeleka wapi kama hata nyumbani kwako ni mbumbumbu?

Mnatumia maneno haya kuwalaza watu akili tu basi!
Unajua hata maana ya global strategic economic intelligence au unatujazia tu server?
 
Mkataba wa DP World sio wa kushusha makontena.
Ni wa kuitawala Tanganyika.
Waarabu wameamua kulipa kisasi Tanganyika baada ya kupinduliwa Zanzibar.
"Madaraka yetu yamehamishiwa Dubai" (Profesa Shvji)
 
Tutunze kumbukumbu watoto wetu watakuja kutucheka Kama tunavyo wacheka hawa ndugu zetu
 
Yeriko kwa kweli ana akili sana ila si kwamba anawazidi akina Mbowe na Slaa. Alichokifanya Yeriko ni kueleza ukweli ambao ni silaha makini sana kwa opposition parties na timing yake kwa Mbowe na Slaa haikuwa hii. Kumbuka kuwa hii story ya Kitila kuonana na CEO wa DP World 2020 siyo mpya ila kwa walio wengi. Yawezekana kuna wengi walikuwa hawaijui (licha ya kwamba kwa kiasi fulani nadhani ilikuwepo kwenye mainstream media) na bado wengi hawaijui maana huku kwenye mitandao ya kijamii hawamo.

Wote wanaolisemea jambo hili kwa maana ya kuonesha mapungufu ya makubaliano/mkataba, kwa namna yoyote ile wako sahihi. Wote tuendelee kushirikiana kuhakikisha kuwa, hata kama ni kwa kulipa fidia ya namna fulani, ardhi yetu haiuzwi kamwe.

Tuwaombee ulinzi waliotishiwa hata kifo kwa ajili ya kuwa vocal kwenye hili. Tushikamane na kuuchangia harakati za kuhakikisha bandari zetu na maeneo yote yanayotanjwa kwenye makubaliano/mkataba na DP Word, yanabakia kuwa ya watanzania, sasa kwa kwa vizazi vyote, na kwa kadri dunia itakavyoendelea kuwapo.

Kudos kwa wapambanaji wote.
 
Unamtuhumu sana Pengo bila ushahidi.
At least akina Lissu wanatia hoja kwa kutumia document iliyosainiwa na serikali.
Tupe maoni yako juu ya vipengele vya makubaliano na sio kufanya personal attacks kwa akina Mbowe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…