Pre GE2025 Tuseme bila unafiki: Kikwete ni tatizo kwa sasa nchini kuliko wakati wowote

Pre GE2025 Tuseme bila unafiki: Kikwete ni tatizo kwa sasa nchini kuliko wakati wowote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkapa! Nitajie aliyemrudisha.
Mkuu kwa ungwana ungeanza kutaja kama nilivyo kuomba halafu ndio unitake nikutajie.

Ila kwa kukufundisha ungwana nakutajia kama ifuatavyo:

Baadhi ya mawaziri waliohudumu kwenye serikali ya Ali Hassan Mwinyi (1985–1995) na baadaye wakateuliwa tena kwenye serikali ya Benjamin Mkapa (1995–2005) ni hawa:

1. Mheshimiwa Jakaya Kikwete

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Maji, Nishati na Madini (1990–1995).
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (1995–2005).

2. Marehemu Edward Lowassa

  • Serikali ya Mwinyi: Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini (1990–1995).
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Nishati na Madini (2000–2005).

3. Hayati John Pombe Magufuli

  • Serikali ya Mwinyi: Naibu Waziri wa Ujenzi (1995).
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Ujenzi (2000–2005).

4. Marehemu Joseph Mungai

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Elimu na Utamaduni.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Kilimo na Chakula.

5. Mheshimiwa Anna Abdallah

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Afya (2000–2005).

6. Marehemu Basil Mramba

  • Serikali ya Mwinyi: Naibu Waziri wa Fedha.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Fedha (2000–2005).

7. Marehemu Iddi Simba

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Viwanda na Biashara.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Viwanda na Biashara (1995–2000).
 
Kwani JK alifukuzwa na nani?
Mkuu nimekujibu ulichouliza, hayo maswali mengine kafanye utafiti mwenyewe. Ila kwa kukusaidia na kuongezea majina mengine:- Rudi kwenye ubao wangu wa awali utayaona!
 
Anaropoka kuwa wachawi wamekufa (Mkapa,Mwinyi,Magufuli,Lowasa,Membe.et) amabaki yeye,kweli anahitaji wataalamu wa psychology kumuweka sawa..
Mkuu hapa nakuunga mkono, kwa kweli alipotoka.
 
Ungetuambia kuna vinini ame/nafanya.. wengine kukomenti kwa hisia hatuwezi
 
Huyu Mr. Smile file lake la hukumu kwa Mungu li tayari. Linasubiria aitwe tu kusomewa hukumu yake na kibaya ni kwamba makosa yake yapo wazi hatatakiwa kujitetea,hivyo ni moja kwa moja motoni. Maana kutubu kwake ni ngumu. Hawezi kurudisha kwa watanzania vyote alivyofisidi au hasara yoyote kwa taifa iliyotokana na kuhusika kwake.
🤣 🤣 🤣
 
Hazina yetu pekee iliyo baki nchini ni Rais Mstaafu JK, Watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama tunamuombea Mungu azidi kumpa maisha marefu yenye afya na maarifa tele.
Taifa linamtegemea na Afrika pia.
Wachache wenye chuki watakufa mapema kwa uchungu.
 
Samia hamuitaji mtu yeyote kubaki madarakani nguvu yake ya urais aliyo nayo inamtosha kufanya chochote anacho jisikia na asiwepo mtu atakayebweka ndani nchi hii.
Nguvu ya kimamlaka aliyo nayo Samia kwa sasa anaweza kuitumia kumpoteza hata huyo Kikwete.
kwel kabisa ifike mahali tukubali kuwa samia ndiye top wa Tanzania na kikwete sio lolote kwake.
 
Jk ni rais aliyeko madarakani Kwa njia nyingine tofauti kabisa na njia tulizozizoea. Yeye ndo ana remote control. Maza ni geresha tu.

Le Bepari la msogaland
 
Hatumchukiii. Kikwete ndiye mtesi wa taifa hili.
Watesi wa nchi hii ni nyinyi wenyewe msio kuwa na akili, kikwete kaingia madarakani kakuta nchi ina miaka 45 imepata uhuru na bado akaikuta inanuka umasikini kila sehemu, akatawala miaka 10 akaondoka akaiacha nchi inanuka umasikini mpaka ana miaka 10 ameondoka madakani nchi bado inanuka umasikini.
 
Back
Top Bottom