Tuseme ukweli, uchaguzi wa CCM uliofanyika una viashiria vya udini

Status
Not open for further replies.
Wakiristo walikuwa wakimkemea Magufuli ktk ukabila na Ukanda tu ila kwenye udini walikuwa wakimtetea
Uongo mtupu. Hamna wakati wamisheni wameacha kumkemea mtu kwa sababu ni mmisheni mwenzao. Hata pale wachungaji wao walipodai kuwa ni chaguo la Mungu waliwakemea. Teuzi na uongozi wa wakina Polepole, Sirro, Makonda, Sabaya n.k. zilikemewa kama ambavyo wakina Bashiru, Hapi n.k walivyopigiwa kelele. Hii ni tofauti na wengi wa wenzetu ambao kwenu dhana ya Umma ni ya muhimu kuliko utaifa.

Haya mambo ya false equivalence hayatawafikisha mbali. Mimi ningedhani kuwa mngewafunda hao waliopata uteuzi ili wasiwaangushe maana bila shaka kuna wapuuzi ambao watahukumu jamii yote ya waislamu kwa mapungufu yao.

Amandla....
 
Nimependa sana ulivyoandika mkuu.Hii ndiyo maana halisi ya kua great thinker.Hata viongozi wote wakiwa Wakristu,mradi wanatenda haki na kuwatetea Watanzania hakuna tatizo.Naandika kila siku huu udini tunaouendekeza karibuni tuta
 
Kinachofuata ITV ni hoja ya Tanzania kujiunga na Organization of Islamic Countries (OIC) na Zanzibar kuwa mwanachama wa FIFA na kupewa kiti UN.

Fuatilia ata Mapesa ambayo Bi.Mkubwa amepewa kutoka Uarabuni!
Mizunguko ya Nini?

Wavunje tu Muungano.
 
Una akili kiduchu sana aisee. Chadema ni serikali?
 
Naona unachanganya kachumbari na kande kidogo

Mwenyekiti wa BAWACHA aliyepita ni Halima Mdee Mkiristo

Mwenyekiti wa BAVICHA ni Pambalu Mkiristo, yupo mpaka Sasa
Ndio nmekutajia Sasa BAVICHA in general Ili uone team nzima ilvyojaa waislam mpaka Katibu mwenezi ni Twaha Mwaipaya Muislam pure kabisa.

Huko BAWACHA ndio usiseme Kulikua na Mdee lakini makamu alikuwepo Hawa Mwaifunga, Kunti Majala, Sharifa Suleiman na Katibu mwenezi alikua Muislam pia hapo mkristo ni Mdee na Kishoa tu. Sasa hapo udini uko wapi?
 
Hizi lugha hizi "wamisheni" ,wavaa kobaz" hizi zote ni chuki.Kwa nn usiseme Wakristu au Waislam au namna ambayo hutajionyesha una chuki dhidi ya mwenzio??
 
Mwanzilishi wa ujinga huu ni jiwe Uchaguzi ktk awamu yake ulikuwa na viashiria vya kichato-chato.
 
Nimependa sana ulivyoandika mkuu.Hii ndiyo maana halisi ya kua great thinker.Hata viongozi wote wakiwa Wakristu,mradi wanatenda haki na kuwatetea Watanzania hakuna tatizo.Naandika kila siku huu udini tunaouendekeza karibuni tuta
Asante Mkuu. Ubaya wa kuendekeza udini ni kuwa watu wanasita kukosoa wenzao kwa sababu tu ni dini yao. Aidha, wanawakataa watendaji wazuri ambao wangewasaidia kwa sababu tu sio dini yao. Wanapoteuliwa wenye dini yetu tujue kuwa wana dhamana kubwa ya kuwatendea haki wale ambao sio wa dini yetu. Na tunatakiwa tuwakemee pale tuu tunapoona dalili za kutupendelea badala ya kukaa mkao wa kula na kujitetea kuwa mbona wenzetu walikuwa wanapendeleana.

Amandla...
 
Hi

Hizi lugha hizi "wamisheni" ,wavaa kobaz" hizi zote ni chuki.Kwa nn usiseme Wakristu au Waislam au namna ambayo hutajionyesha una chuki dhidi ya mwenzio??
Mimi natumia neno wamisheni kwa sababu nimeitwa sana hilo na sina tatizo nalo. Hilo lingine silitumii maana naona linatumiwa kuwadhalilisha wenzetu.

Amandla...
 
Kama ndio hao hao waliopitishwa kugombea maana yake kulikuwa hakuna alternative.lazima wapigiwe kura.
 
Kwenye Utawala nyie wenyewe ndio mnasema hii ni zamu ya hawa au hawa

Hakuna ulazima ww kumuweka Rais kwa Udini kisa aliepita ni dini hii au ile na ajae atakuwa dini hii au ile

Wananchi wapewe haki yao kuchagua wanaemuona anawafaa hata kama watajirudia mara 3

Tuache dhana hizi za Udini maana wengine wanasema mbona utawala wa Magu aliwajaza upande wake?
Hapo mnaonyesha kiasi gani mmeamua kuonyesha tofauti zetu

Hao waliochaguliwa awamu iliyopita tuliona waliyoyafanya acha tuangalie na hawa wataleta nini
 
Udini, Rushwa na ukabila
 
Ni mjinga tu anaetazama/kufikiri mambo kwa mwamvuli wa udini...hivi hata wakiwa waislam au wakristo wote ndo sisi waislam au wakristo tutaneemeka?

Sisi tuwahukumu kwa kushindwa kutekeleza majukumu Yao na sio kwa dini zao
Umejibu vyema ndg

Mleta mada ndio mwenye udini!

Na anaonyesha jina lake lilikatwa
 
Hao wote si wamepigiwa kura tena za siri?

Ama wamejiteua wenyewe?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…