Tuseme ukweli, uchaguzi wa CCM uliofanyika una viashiria vya udini

Status
Not open for further replies.
Hao ni wakatoriki, jaribuni wengine
 
Katika hawa waliochaguliwa ni nani aliyekemewa kwa sababu ya dini yake? Watu wanachokifanya ni kuhoji idadi yao na sio kila mtu mmoja mmoja katika nafasi yake. Watu wanahoji itakuwaje katika jiji kama Dar es Salaam nafasi za juu zote zishikwe na waislamu? Ni kama vile watu wangehoji kama nafasi zote za juu wangechaguliwa watu wa kabila moja au jinsia moja au hata wakristu watupu. Ni hoja ambayo inapaswa kubebwa na kuthibitishwa kuwa haina mashiko kwa matendo yao kama viongozi. Wasiwasi wangu ni kuwa watu kama wewe mtakingia kifua hata pale watakapoonekana kuwa wanapwaya kwa kisingizio kuwa wanakosolewa kwa sababu ni waislamu.

Hebu tumzungumzie Magufuli ambae unasema teuzi zake zilijaa taswira ya udini. Uchaguzi wa 2017 ulikuwa hivi:
1. Mwenyekiti Kheri James (Mkristu).
2. Makamu Mwenyekiti Thabia Mwita ( Muislamu Mzanzibari)
3. Mwakilishi wa UVCCM katika UWT Dotto Nyirenda ( Mkristu)
4. Mwakilishi wa UVCCM katika Jumuia ya Wazazi Amir Mkalipa (Muislamu)
5. Wawakilishi wa UVCCM katika Baraza Kuu la CCM Rose Manumba ( Mkristu), John Katarahiya ( Mkristu), Seki Boniventure Kasuga ( Mkristu)
6. Wajumbe wa UVCCM kwenda kwenye Halmashauri Kuu Sophia Kizigo ( Mkristu), Mussa Mwakitinya ( Muislamu) na Khadija Taya ( Muislamu).

Hapo pia kuna wajumbe wa UVCCM kutoka Zanzibar wawili kwenda kwenye Baraza Kuu na wawili kwenda kwenye Halmashauri Kuu, wote wanne walikuwa waislamu ( tunasahau kuwa kuna wakristu Zanzibar). Kwa hesabu zangu wakati wa JPM kulikuwa na wajumbe 6 wakristu na 3 waislamu kutoka bara. Ukijumlisha na wazanzibari idadi inakuwa waislamu wanane ( Makamu Mwenyekiti, Mwakilishi katika Jumuia ya Wazazi, wajumbe wawilikwenda kwenye Halmashauri Kuu na wanne kutoka Zanzibar) na wakristu sita.

Huo udini wa JPM hapo uko wapi?

BTW, chaguzi zetu nyingi ni uteuzi maana wajumbe ( sio wana CCM wote) wanawapigia kura watu walioteuliwa na vyombo vilivyopewa mamlaka ya kufanya hivyo.

Amandla...
 
Matola umejawa upumbavu mwingi sana. Mara nyingi siku hizi unaandika hoja zilizojaa uchonganishi na upuuzi mtupu. Unafaa kupuuzwa.
 
Duuuh aiseee
 
CCM ni Chama sio Dola.
Tuliani mnyolewe tulisema bila katiba mpya Kuna siku hii nchi itaendeshwa kidikteta au kikabila au kidini au kirafiki mkapuuza.

Kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Kama waliopiga kura ni wajumbe halali wa CCM basi waliochaguliwa ni halali na wamechaguliwa kama wanachama wa CCM sio kama waumini wa dini yoyote. Tuache udini. Haya yote yanatokana na Vyombo vya Dola kushindwa kupambanua kuwa CCM ni Chama kama vyama vingine na wanaokiongoza ni watu kama watu wengine matokeo yake ni wao vyombo vya Dola kujipendekeza CCM , Mashekhe kujipendekeza CCM, mapadri ,maaskofu, manabii na Mitume kujipendekeza CCM na kumweka Mwenyekiti wa CCM kwenye kiti Cha Enzi kama mungu wao awapaye riziki yao na familia zao.

Tulieni dawa itaingia taratibu mkizinduka.
 
Pamoja na kugombea kuna kuteuliwa, mteuzi kama hakutaki jina lako halitaonekana kwa wapiga kura.
 
Wajumbe uletewa majina
 
CCM siyo jumuia, kigango, Parokia wala Jamaati. wanachama wa CCM wamechagua viongozi wanaowataka.

By the way wakati Magufuli anajaza Wakiristo serikalini mbona hizi kelele hatukuzisikia?
Nyerere aliwahi sema wewe unaweza mcharaza mke wako bakora lkn isiwe news kubwa kwa siku hiyo lkn yeye Nyerere akimcharaza mke wake bakora nchi nzima italipuka.
 
Usichokijuwa ni kwamba Magufuli ni zao la Mkapa, na Mkapa ndio alisimama Kidete kwenye vikao vya Ccm kuhakikisha Magufuli ndio anateuliwa kuwa mgombea wa Ccm.
Unazungumza usiyoyajua. Labda unasikia tu juu juu.

Ukweli ni kwamba:

Mkapa hakusimama kidete kwaajili ya Magufuli.

Wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu walikuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa. Wajumbe walipoona jina la Lowasa halipo wakaanza kuimba kuwa wana imani na Lowasa.

Jina la Lowasa liliondolewa kwa sababu kwa uwepo wa jina la Lowasa, Membe asingeweza kushinda. Hivyo zikafanywa figisu jina la Lowasa lisiwepo. Wakaamua libakie jina la Membe na wengine wawili ambao kwa vyovyote wajumbe hawawezi kuwachagua. Mgufuli ndiye aliyeonekana kuwa kamwe wajumbe hawawezi kumchagua.

Wajumbe waliojipanga kumchagua Lowasa walipoona jina la Lowasa halipo, wakaamua kutoka nje ya ukumbi. Waliobakia ukumbini idadi yao haikuwa inafikia hata 40%. Ndipo Kikwete akampigia simu Mkapa akimweleza hali ilivyo, na kuomba ushauri wafanye nini. Mkapa akasema kuwa kura zinazohesabika ni za watu waliopiga kura, hivyo waliobakia ukumbini waendelee na zoezi la kupiga kura. Wale watu wa Lowasa wakati huo wakiwa nje walikuwa wakijadili wafanye nini. Ndipo akaja mjumve mmoja toka ukumbini akawaambia kuwa wenzao waliobakia ukumbini wameanza kugawiwa karatasi za kupigia kura. Ndipo wakakubaliana wote kwa pamoja kuwa ili kumkomesha Kikwete, wote wakampe yule asiyetakiwa, ambaye alikuwa ni Magufuli. Kwa hiyo, kura alizopata Magufuli zilikuwa ni kura za chuki za watu wa Lowasa dhidi ya Kikwete.
 
Sisi tunazungumzia uongozi wa juu kitaifa, achana na hao wanaoendesha chama kwa kufuata maagizo kutoka kwa mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu nk.
 
Tanzania miaka mi5 mbeleni haitakuwa sehemu salama ya kuishi tena.
Kama haulo kwenye 'system' nashauri utafute mpango wa kuhama makazi
 
Hawa jamaa mimi nawaona wanafq tu
Malalamiko yao huyatoa kipindi cha waislam
Wakikaa wakristo wenzao hufunga midomo yao, zile nyaraka ndefu ndefu Hua hazionekani kipindi hicho
Wanajikuta watakatifu, jau sana Hawa watu
 
Sibitisha angao kidogo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…