Uchaguzi 2020 Tusemezane: Uhalisia wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

Mbona inasemwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania walikataa mfumo wa vyama vingi lakini Nyerere ndo akaupigia debe...uongo?
Sasa jambo la msingi likikataliwa na wajinga wengi utaliacha ili uwaridhishe au utawapa wale werevu wachache halafu wale wajinga siku wakiamka akili zao ndio waone walivyopotoka?

Bahati mbaya mpaka sasa bado wamebaki wajinga wachache ambao bado hawajatambua ule ujinga wao wa wakati ule.
 
Uwepo wa jengo mahali hauwezi kuwa ndio kipimo pekee cha uwepo/ kukubalika kwa chama cha siasa.

Hii miaka mitano hao Chadema waliruhusiwa lini kufanya siasa?

Unasema Chadema imefutika kama ni hivyo kwanini mkafanya uhuni wa wazi kwenye ule uchaguzi wa serikali za mitaa?
 
Experience inaonyesha kuwa kususia uchaguzi haijawahi kuwa na better outcome kwa wapinzani.

Jakaya aliwapa option ya katiba mpya, yenye tume huru ya uchaguzi na madaraka ya raisi yaliyounguzwa na mfumo kedekede mizurimizuri wakalazimisha kuwa ni Lazima wapate serikali tatu ndo wataukubali mchakato, matokeo yake serikali tatu haipo na Rais alitekuja mdarakani anayependa udikteta akaona katiba ya sasa inamfaa zaidi kwa hulka yake ba matokeo yake akaharibu mchakato wa katiba mpya uliokuwa umebakisha kuitishwa kura ya maoni tu!

Historia ya wapinzani kususia chaguzi inaonyesha haijawahi kuwapa benefit mfano
1.Walisusia uchaguzi wa marudio ya ubunge Dar mwaka 1995, kulichotokea CCM ikatwaa majimbo yote isipokuwa la Lamwai

2. Walisusia uchaguzi wa Marudio Zanzibar, matokeo yake CCM wakafurahi kweli kwa hilo

3. Walisusia ushiriki wa uchaguzi wa serikalu za mitaa baada ya asilimia 97 ya wagombea wao kuenguliwa, sasa hivi CCM wana vijiji vyote na wala hawajifeel guilty kabisa

Mimi naona kuwa Wapambane kupitia uwabja huu mbovu huku wakiendelea kushinikiza uwekwe uwanja mzuri zaidi
 
Sio kwamba hivyo vyama pinzani havilifahamu nyaningabu, watu wengine wapo tu kwa ajiri ya maslahi yao binafsi (Ruzuku) , wengi hawavumi, hawataki kuvuma na haitatokea wavume ila Wamoo
 

Ni haki yao kushiriki uchaguzi na ambalo wanaliweka wazi kabisa kwa watawala ni kwamba watakapo jaribu kutumia hila kushinda wataitumbukiza nchi kwenye machafuko makubwa sasa ni watawala kuamua kuwe na machafuko hayo au ushindi upatikane kwenye sanduku la kura. Hawa watu siyo wa kuwadharau ni vema serikali ambayo imekuwa kikwazo cha tume huru ikaliona hilo kuwa uchaguzi huu hakuna atakayekubali watu kukimbia na mabox ya kura au wasimamizi kukimbia ofisi zao kwa nia ya kuengua wagombea wa upinzani. Kinachofanyika ni kuwaandaa wafuasi wao kiakili.
 
Listern mimi siipendi. Ccm yaani ccm na matope niko radhi niyachague matope yatawale

Ila alichokiongea NN kina mashiko .. CCM ina credibility nyingi za kushinda katika chaguzi zote huu wa sasa na hata huo wa 2025 endapo tu kama vyama vya siasa vya nchi havito badilika na kuendelea kutumia mbinu zile zile za upambanaji dhidi ya chama tawala .. Kama NN alivyosema Tume ya uchaguzi imewekwa hapo ilipo na mwenye kiti wa ccm .police na vyombo vyote vya usalama vina isapoti ccm ... Narudia tena kama vyama pinzani vitathubutu kutumia njia zile zile za awali kupambana na chama tawala basi ni vigumu sana kuitoa ccm madarakani

Ila kama vyama pinzani vita tafuta mbinu mpya chanya za kupambana na chama Tawala basi mwaka huu ccm kazi inayo

Mbinu moja wapo vyama hivi pinzani vinapaswa kuamsha morali ya wafuasi wao .kuwaondoa uwoga na ujinga walionao kuwaandaa wafuasi wao walete mapinduzi pindi vyama hivyo vitakapo porwa haki yao ya ushindi endapo vitakuwa vimeshinda katika uchaguzi mkuu
 
Wakati unamshangilia Padre Slaa akili zako zilifungiwa kabatini?
 
Nyani , kati siku akili zako zilipikurudia ni pamoja na post hii. Lakini nakuona kama msomi asiyependa nchi yake. Kasoro za ki muundo unaziona halafu lawama unawarushia wapinzani !!. Hii akili ya msomi wa aina gani ?!.

Kwamba wewe mamlaka zilizotakiwa kutoa haki kwa wananchi kujichagulia viongozi wao ni wapinzani ?!. Usomi huu mbona bure kabisa Ngabu ?!.

Nchi hii ni yetu sote. Tujiwekee utaratibu mzuri wa watu kuwaweka viongozi bora na wanaowataka. Si hii ya lazima utokane na chama cha ki communist cha Ccm !!. Usomi wako usaidie badala ya kuwazodoa wapinzani wanaopambana kupata haki hiyo [emoji120][emoji120]
 
Hili ndilo tatizo la Watanganyika, unajuwa ni kwa Nini nchi jirani ya Zanzibar mpaka Cuf ya Maalim walitowa makamishina kuunda tume ya uchaguzi Zec?

Hakuna haki bila kujitowa sadaka ya damu. Hii ni duniani kote, angalia hata Kenya.
 
Hana mshindani ndiyo mgechpisha fom moja tu kama tochi ya muwindaji?
Hivi Unamiaka 23
Mbowe kwenye uenyekiti ana Karibia 20
Hahah
Yaani alianza kuwa mwenyekiti unanyonya
Leo una miliki Tecno
 
Ni sahihi usemalo ila huyu TL naona kajipanga na jawabu, nadhani kuna maandamano yanaandaliwa kukabili hilo. Swali muhimu la kujiuliza, huyu TL akiitisha maandamano atapata wafuasi hata 1m nchini? Kama jibu ni ndio basi tatizo bado lipo kwa chama tawala.
 
Sijui ccm mnafurahia nini mazingira mabovu ya uchaguzi na hayo hayo ndio yatawaangusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…