Uchaguzi 2020 Tusemezane: Uhalisia wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

You said it all. Wengi wao
 
Tayari kuna watu washaanza vilio vya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kujiuzulu!

Watanzania tuna matatizo sana!
Miaka nenda rudi tumetoa hili somo kwa Wapinzani, halijaeleweka
Huwezi kuwa na Polisi, TCRA, NEC, Msajili wa vyama ukategemea kupewa haki sawa na CCM

Fikiria hivi, 'OCD aliyetangaza' matokeo wiki mbili zilizopita leo ndiye anasimamia uchaguzi, unategemea nini?

Mkurugenzi wa NEC ambaye ni mteuliwa wa Mwenyekiti wa CCM , anatangazia wapinzani wazungumzie sera za madaraja, barabara na vituo vya afya. Kwamba, yeye si refarii tena bali kada. Unategemea nini?

Matokeo yanapelekwa kwingine si kutolewa vituoni, unategemea nini.
Tena yanasindikizwa na Polisi kama yule OCD ambaye wiki mbili zikizopita alishatoa matokeo. Unategemea nini.

Unapokuwa chama kikuu cha upinzani tayari una platform.
Wapinzani wangetumia hiyo kudai katiba mpya, tume huru kwanza. Haya ndiyo mambo ambayo yangeweka mizani sawa kwa kuanzia.Tena kuna evidence kwamba umma upo upande wao kuliko ule

Nilishangaa TV moja duniani imetengaza ''opposition' ya Tanzania kulalamika kuonewa. Mbali sana
Dunia inaona lakini si kwa hoja ya mchimba magimbi au Queen au Hashim bali real opposition

NN kasema si kususia tu bali kususia kwa malengo!
 
Nadhani upinzani wangetengeneza ushirikiano na vyama vya upinzani vya nje kupata ujuzi sahihi ila twende mbele turudi nyuma mwalimu alichemka suala moja tu hii katiba aliyotuachia!

Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema binadamu mwili wake umeumbwa kustarehe tu by nature kwa kifupi hakuna ambaye hapendi shida! Tuje kwenye maana ya hili jambo hivi mtu atapataje hofu ilhali katiba inamuambia akiondoka madarakani ana kinga ya "kutoshtakiwa" pili uchaguzi wa urais matokeo yakitangazwa na tume anayoiteua yeye "hayapingimwi/kuhojiwa" popote!


Je kama mtu umempa uhuru wa hivyo bado 90% yeye ndio anawateua serikalini nani wa kubisha akitoa order?

Suluhu :tusizunguke kote katiba mpya ya wananchi ndio suluhu!
 
Na huu ndiyo ukweli.
 
Utamu wa ndoto huisha asubuhi!

 
Kwa uongozi wa kisiasa uliopo kususia uchaguzi ili kushinikiza katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi ni mbinu isiyokuwa na tija hata kidogo. Ile kauli tu ya uongozi wa sasa ya kuhakikisha kuwa ifikapo 2020 vyama shindani viwe vimekufa ni ushahidi tosha juu ya aina ya uongozi tulionao sasa. Ongezea sarakasi za kuvurugwa kwa CUF, shauri la wakurugenzi kutosimamia uchaguzi, uchaguzi wa vijiji/mitaa, nk. Kususia uchaguzi ni kuwa "passive" wakati ambapo kinachohitajika ni kuwa "aggressive". Kubanana hapa hapa ndiyo mwendo sahihi.
Lakini muhimu zaidi ni kwamba pamoja na changamoto zilizopo tangu 1995 ushindani wa kisiasa umekuwa ukiongezeka nchini. Ilitarajiwa kuwa utafika wakati ambapo kutakuwa na idadi ya kutosha ya wabunge wa upinzani kufanya maamuzi muhimu. Haikutarajiwa kuwa utakuja kutokea uongozi utakaoturudisha kidemokrasia miaka 60 nyuma. Haikutazamiwa kabisa kuwa wanasiasa wetu watakuja kuwafanyia wenzao wa vyama shindani mambo mabaya ambayo hata wakoloni hawakumfanyia Nyerere na wezake. Hakika, kufuatia uchaguzi wa 2020 hali ya kisiasa nchini itabadilika. Hii ndiyo njia ya kuharakisha upatikanaji wa katiba mpya na tume huru kuliko kumwachia mlevi tembo!
 
Ipo siku mtanielewa tu.....tuombeane uzima tu.
 
Good thinking
 

Kuwa na katiba mpya kwa ajili ya mfumo wa vyama vingi ni kitu kimoja na kuwa na katiba bora kwa ajili ya mfumo wa vyama vingi ni kitu kingine!

Let’s say umeamua kuandika katiba mpya kabla ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Kwa maoni yako, wajumbe wa bunge la katiba ambao wataangalia maslahi mapana ya taifa, watatoka wapi? Bunge la katiba liko more likely kuwa dominated na wajumbe kutoka chama pekee kilichopo, ambao wengi wao wana maslahi ambayo wasingependa kuona yanapotea baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi. Matokeo yake, katiba mpya haitakuwa na playing field rafiki sana kwa vyama vitakavyoanzishwa!
 
Tunaweza kupata vyote kwa wakati mmoja.

Katiba mpya na iliyo bora zaidi inawezekana!
 
me nimepiga kuonesha kuwa upinzani ni iman hauwez kupotezwa kwa kauli ya mtu mmoja
 
Dogo wakati mwingine unaongea point sana, CDM na ACT walifanya makosa makubwa sana kuingia kwenye uchaguzi huu pasipo kwanza kupatikana TUME HURU YA UCHAGUZI. Walipaswa kujifunza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…