Uchaguzi 2020 Tusemezane: Uhalisia wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.

Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla hatujarejea katika mfumo huo wa kiushindani.

Miaka yote hii tokea 1995, zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu limekuwa ni zoezi la kutimiza wajibu tu, ili nasi tuonekane tuna demokrasia ya kuchagua viongozi wetu ilhali uwanja wa ushindani haupo sawa baina ya washiriki wa mpambano.

Walio wahalisia wa mambo kama mimi, tayari ‘tunajua’ ni mgombea yupi kwenye ngazi ya urais atayetangazwa mshindi.

Mgombea huyo atayetangazwa kuwa ndo mshindi, ndo mtu huyo huyo aliyewateua kwenye hizo nafasi zao kwenye tume ya uchaguzi hao wataomtangaza yeye kuwa ndo mshindi.

Sasa nikiona jinsi ambavyo wanachama wa vyama vilivyo nje dola walivyo na hamu na hamasa ya uchaguzi mkuu, nashindwa kuelewa.

Nashindwa kuelewa kama ni wamejitoa tu fahamu kwa muda na kwamba kabla ya uchaguzi akili zitawarudia au wamejitoa kabisa fahamu na kusahau kabisa jinsi vile uwanja wa mapambano haupo sawa!

Kwa sababu, nikionacho hapa ni kwamba, baada ya tarehe 28 Oktoba, tutarudi kule kule tulikokuwa 2005, 2010, na 2015.

Baada ya ‘kushindwa’ watu ndo watagutuka tena kuwa kumbe tunahitaji katiba mpya. Kumbe tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Kumbe tunahitaji uwanja ulio sawa kwa washiriki wote.

Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.

Sasa sijui kama kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua una vikwazo vingi ni jambo la busara au la. Ingekuwa uamuzi ni wangu mimi binafsi, nisingeshiriki mchakato ambao ni wa maigizo.

Wengine wanaweza kuwa na mtazamo ulio tofauti. Hakuna ubaya kwenye hilo.

Ila kwa kadri mtu unapozidi kushiriki mchakato wa jambo ambalo unajua kabisa halitoi fursa sawa kwa wote, unapokosa kupata fursa uitakayo, unakuwa umejipunguzia mamlaka ya kimaadili ya kupinga na kulalamikia matokeo.

Manake kama ulikuwa unajua kabla ya zoezi kuanza kuwa hakuna fursa sawa, kwa nini sasa ulishiriki? Si ungeligomea zoezi zima tu!

Kwa sasa endeleeni kufurahia maneno matamu ya Lissu. Sasa hivi anawapa nyie wapenzi na mashabiki wake kile kiitwacho ‘red meat’, yaani yale maneno mnayotaka kusikia na yanayoziamsha hisia zenu.

Naona na Bw. Membe naye anajitutumua kuwarushia mashabiki wake hizo nyama nyekundu lakini hamfikii Lissu.

Baada ya uchaguzi kuisha na Rais Magufuli kutangazwa mshindi, akili, kama mnazo, labda ndo zitawarudia na kutambua kuwa hamkuwa na lenu kwenye huo uchaguzi!

Kama mnabisha, siku ya siku ikifika nitawakumbusha haya maneno yangu. Msije kununa tu.😁
Wewe hupendi kabisa mabadiliko nchi hii na utakuta bado ni kijana mdogo tu, lazima una tatizo kuendelea kuishabikia ccm iliyoshindwa kuleta mabadiliko tuliyotarajia kwa miaka zaidi ya 60 sasa.
 
CCM ukiwambia tume huru hiyooo! wanakimbiana
 
Mimi hata siwaelewagi .... wanashangilia vijembe utafikiri vinageuka kura. Kwanza kwa hali iliyopo mwaka huu hata kama uchaguzi utasimamiwa na mabeberu CCM itashinda! Huko mitaani/vijijini Chadema imefutika, matawi yamefungwa mengi sana. Kabla hata ya issue za Katiba na tume chama hakina mizizi ya watu ngazi za chini kama CCM.

ushahidi huu apa
 
Jaribu kuliona jambo moja, vyama makini vya upinzani kama Chadema, ACT na pengine NCCR vingeamua kutoshiriki lakini vibaraka wa CCM kama TLP, UDP nk vikaamua vinashiriki huoni kuwa dunia itatambua kuwa uchaguzi wa vyama vingi umefanyika?

Nini matokeo ya utendaji wa bunge litakalo fuatia? Hali itakuwa mbaya sana pengine kuliko Korea kaskazini. Njia INAYOBIDI kufuata ni ile aliyo shauri Lissu tuu, kutokubali wizi wa kura na kusema tunamwachia Mungu.
Duu akili za bangi hatari sana, Kwani wewe unaishi kwa kuwafurahisha Wakoloni.
 
Uwepo wa jengo mahali hauwezi kuwa ndio kipimo pekee cha uwepo/ kukubalika kwa chama cha siasa.

Hii miaka mitano hao Chadema waliruhusiwa lini kufanya siasa?

Unasema Chadema imefutika kama ni hivyo kwanini mkafanya uhuni wa wazi kwenye ule uchaguzi wa serikali za mitaa?
punguzeni mdomo
 
Vyama vya Siasa vya upinzani havina ushirikiano na hapo CCM ndipo anapopatia Point.Nakumbuka kuna Vyama vya Siasa vipo 17 vya Upinzani na hivyo vyote vikiamua kwamba hatutashiriki katika uchaguzi wa Mwaka huu kama mambo 1,2,3.... hayajarekebishwa,unafikiri CCM itakuwa na nguvu ya kusema itafanya uchaguzi hata kama mumesusa kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, ni lazima wangekaa Meza moja na kurekebisha pale kwenye mapungufu ambapo upinzani unaona hautatendewa haki.Lakini utakuta kuna Chama chenyewe hakina Mbunge hata mmoja hata watu hawakifahamu kinasema kitashiriki uchaguzi na hapo CCM ndipo inapopiga bao .
 
Nawakumbushia tu na pia nitawakumbusha tena baada ya Oktoba 28, 2020.
 
Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.

Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla hatujarejea katika mfumo huo wa kiushindani.

Miaka yote hii tokea 1995, zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu limekuwa ni zoezi la kutimiza wajibu tu, ili nasi tuonekane tuna demokrasia ya kuchagua viongozi wetu ilhali uwanja wa ushindani haupo sawa baina ya washiriki wa mpambano.

Walio wahalisia wa mambo kama mimi, tayari ‘tunajua’ ni mgombea yupi kwenye ngazi ya urais atayetangazwa mshindi.

Mgombea huyo atayetangazwa kuwa ndo mshindi, ndo mtu huyo huyo aliyewateua kwenye hizo nafasi zao kwenye tume ya uchaguzi hao wataomtangaza yeye kuwa ndo mshindi.

Sasa nikiona jinsi ambavyo wanachama wa vyama vilivyo nje dola walivyo na hamu na hamasa ya uchaguzi mkuu, nashindwa kuelewa.

Nashindwa kuelewa kama ni wamejitoa tu fahamu kwa muda na kwamba kabla ya uchaguzi akili zitawarudia au wamejitoa kabisa fahamu na kusahau kabisa jinsi vile uwanja wa mapambano haupo sawa!

Kwa sababu, nikionacho hapa ni kwamba, baada ya tarehe 28 Oktoba, tutarudi kule kule tulikokuwa 2005, 2010, na 2015.

Baada ya ‘kushindwa’ watu ndo watagutuka tena kuwa kumbe tunahitaji katiba mpya. Kumbe tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Kumbe tunahitaji uwanja ulio sawa kwa washiriki wote.

Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.

Sasa sijui kama kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua una vikwazo vingi ni jambo la busara au la. Ingekuwa uamuzi ni wangu mimi binafsi, nisingeshiriki mchakato ambao ni wa maigizo.

Wengine wanaweza kuwa na mtazamo ulio tofauti. Hakuna ubaya kwenye hilo.

Ila kwa kadri mtu unapozidi kushiriki mchakato wa jambo ambalo unajua kabisa halitoi fursa sawa kwa wote, unapokosa kupata fursa uitakayo, unakuwa umejipunguzia mamlaka ya kimaadili ya kupinga na kulalamikia matokeo.

Manake kama ulikuwa unajua kabla ya zoezi kuanza kuwa hakuna fursa sawa, kwa nini sasa ulishiriki? Si ungeligomea zoezi zima tu!

Kwa sasa endeleeni kufurahia maneno matamu ya Lissu. Sasa hivi anawapa nyie wapenzi na mashabiki wake kile kiitwacho ‘red meat’, yaani yale maneno mnayotaka kusikia na yanayoziamsha hisia zenu.

Naona na Bw. Membe naye anajitutumua kuwarushia mashabiki wake hizo nyama nyekundu lakini hamfikii Lissu.

Baada ya uchaguzi kuisha na Rais Magufuli kutangazwa mshindi, akili, kama mnazo, labda ndo zitawarudia na kutambua kuwa hamkuwa na lenu kwenye huo uchaguzi!

Kama mnabisha, siku ya siku ikifika nitawakumbusha haya maneno yangu. Msije kununa tu.[emoji16]
Magufuli kashaamza kutangaza atampa Lissu kazi.

Katangaza kwamba atampa Masele ukuu wa mkoa au ubalozi.

Yani mpaka mgombea mwenyewe, kwenye kampeni, si anafanya kampeni kwa kuomba kura awe rais, anatuambia tayari nani atampa kazi gani.

Kashajipitisha kwamba atakuwa rais.
 
Safari hii wakiiba kura ndo mwanzo wa kupatikana kwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi
 
Magufuli kashaamza kutangaza atampa Lissu kazi.

Katangaza kwamba atampa Masele ukuu wa mkoa au ubalozi.

Yani mpaka mgombea mwenyewe, kwenye kampeni, si anafanya kampeni kwa kuomba kura awe rais, anatuambia tayari nani atampa kazi gani.

Kashajipitisha kwamba atakuwa rais.
Well, simlaumu sana yeye.

Bali nawalaumu washiriki wa uchaguzi ambao kila mwaka wa uchaguzi tokea 1995, huwapa uhalali CCM.

Naamini kabisa kama tokea 1995 wapinzani wangekuwa wanagoma kushiriki hizo chaguzi za maonyesho, basi sasa hivi walau tungekuwa tuna katiba mpya pamoja na tume iliyo huru kutoka kwenye makucha ya CCM!

Hivi ni wapi kwingine kwenye demokrasia ambapo Rais wa chama tawala huunda tume ya uchaguzi na baadaye yeye mwenyewe kushiriki kwenye chaguzi zinazosimamiwa, kuratibiwa, na kuendeshwa na tume aliyoiunda yeye mwenyewe?

Where they do that at?

That should have been a no - no for the opposition from the get go.

But for whatever reason, they choose to take part in the CCM’s shitshow.
 
Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.
yaani huu uchaguzi maigizo tu. kuna mteule mmoja wa tume huwa namcheki tu mitaani lakini namwona dhahiri kabisa anajua matokeo ni yapi. anyway, mgoja tuangalie tu
 
Nachoweza sema "huwezi kuwa Tajiri kwa kukaa tu ndani ukasusia hata kazi za kubeba mchanga kisa tu hujapata ajira unayoipenda "

Unakula nini Kama hutaki fanya kazi hata ndogo ndogo ?

Vipi kama hio ajira utaipata miaka 20 ijayo ukisema uiaubirie utakuwa ushazeeka pengine ushakufa kwa njaa na watu watakuwa hawana habari na wewe tena .

Ufanyaje?

Fanya kazi yeyote inayokuja mbele yako itakuongezea hamasa , connection ,na kipato utaendela kuishi watu watakuona watakusapo

Ndipo hapo muda muafaka ukifika utapata ile ajira ya ndoto zako

Inaweza ikachelewa lakini hakika utaipata hata Kama Ni uzeeni kwako .

NB:Soma kwa akili sio hisia [emoji3578]
 
Beggar's cannot be choosers,
Acha wapambane then watakachokipata ndicho kitakachotumika kupamabania cha ziada. Na ni matumaini raisi ajaye atakuwa muelewa kama JK arasikiliza zaidi malalamiko ya watu na wahisani then atamalizia mchakato wa katiba mpya by 2035.

I just wonder what would've happened if we had the JK's constitution (regardless of its flaws). Maybe tungekuwa tuna bargaining power kubwa zaidi ya haya mengine ambayo yalikatwa juu kwa juu na bunge la katiba.
 
Hivi Kenya, Zambia, Malawi, Ghana etc. , waliwezaje kuving'oa vyama tawala? Pengine lipo la kujifunza kote huko.

Afrika Kusini najua ni case tofauti sana, but inaonesha kitu kimoja......wananchi wakiamua inawezekana hata kama itachukua muda........na "peserviarance" pia ni muhimu. Muhimu ni wananchi .....
 
Watu washavurugwa akili yani unakuta mtu ana shauku kabisa na huu uchaguzi anajipa imani ya kuwa kutakuwa na mabadiliko ila amesahau kuwa hata chaguzi zilizopita alikuwa katika hali hiyo hiyo ila haikuwahi kubadili matokeo.

Ifike mahali watu wakubali kwanza hili tatizo lao la akili ndipo wataweza kubadili hii hali maana huku kila uchaguzi kuwa na shauku ya kuona ccm inatoka madarakani hali ya kuwa mnajua hakuna usawa kwenye uwanja wa mapambano na hakuna kilichofanyika katika kutatua hilo tatizo,ni wazi hili ni tatizo la akili.
 
Jaribu kuliona jambo moja, vyama makini vya upinzani kama Chadema, ACT na pengine NCCR vingeamua kutoshiriki lakini vibaraka wa CCM kama TLP, UDP nk vikaamua vinashiriki huoni kuwa dunia itatambua kuwa uchaguzi wa vyama vingi umefanyika?

Nini matokeo ya utendaji wa bunge litakalo fuatia? Hali itakuwa mbaya sana pengine kuliko Korea kaskazini. Njia INAYOBIDI kufuata ni ile aliyo shauri Lissu tuu, kutokubali wizi wa kura na kusema tunamwachia Mungu.
Lama Nyani Ngabu amejibu hoja hii naomba unitag, tafadhali. Maana naona kwenye mada yake amefafanua changamoto kwa vyama vya upinzani bila kupendekeza hatua dhidi ya changamoto hizo za "unfair ground" ya uchaguzi.
 
Jaribu kuliona jambo moja, vyama makini vya upinzani kama Chadema, ACT na pengine NCCR vingeamua kutoshiriki lakini vibaraka wa CCM kama TLP, UDP nk vikaamua vinashiriki huoni kuwa dunia itatambua kuwa uchaguzi wa vyama vingi umefanyika?

Nini matokeo ya utendaji wa bunge litakalo fuatia? Hali itakuwa mbaya sana pengine kuliko Korea kaskazini. Njia INAYOBIDI kufuata ni ile aliyo shauri Lissu tuu, kutokubali wizi wa kura na kusema tunamwachia Mungu.

Nimepima ujumbe wangu kwa mizani huru,
Nimetambua unaakili nyingi kuliko aliyeanzisha mada!
Mwanzisha mada itakuwa katumwa na either ndiye amekuwa akishauli wapinzani kususia chaguzi kama zile za serikali za mitaa.
Nadhani mkakani wa mleta mada ulishapitwa na wakati akamwambie aliyemtuma kuwa hawanielewi tena!

Hapa kazi ni moja tu ,twende jino kwa jino,pampa to bampa,haki bin haki,bandika bandua lazima wateme nyongo na ushindi upo kikubwa tusifumbe macho.
 
Back
Top Bottom