Tatizo sio hela tatizo ni mindset inayotengenezwa na hali ya kiuchumi. Nina mademu wawili mmoja familia inajiweza na mwingine familia ya kipato cha chini sana. Huyo wanaojiweza kwao mapenzi hajui ila yuko real, nikitaka kuoa kuhusu yeye sijiulizi mara mbili. Ana akili ya maisha kuliko maelezo, ana uzoefu na shughuli za nyumbani kwao na akishauri kitu unajua hapa kuna uhai wa akili. Nimeanza kumuona tupo sekondari, form four kapiga Div. 1 ya 10 serikalini, dip kamaliza na 4+ GPA.
Huyu mwingine mrembo zaidi, bright future behind her, ngozi nyororo na mapenzi anayajua sana. Huyu nimemkamata anacheat mara mbili, mara moja na mbaba mtu mzima kama sponsor. Tatizo ni umaskini hadi kodi ananitegemea wakati yuko chuo. Wadogo zake wote hawajafika form four wanakataa shule, yeye tu ndio kapiga diploma kwa mbinde na penyewe kasoma mwaka mmoja wa ziada kisa akili chache kichwani na kuendekeza starehe akafeli mtihani (sababu kwao huwezi pata starehe, na elimu sio kipaumbele ukoo mzima). Mdogo wake aliumwa familia ikashindwa kumpeleka hospitali baadae mara mapepo mara malaria imepanda kichwani.
Kuna muda wote nilitaka kuwaacha, huyu matako makubwa akasikitika kwanini namuacha wakati natakiwa kumlipia kodi mwezi unaofuata.
Huyu mwingine alidai anajifunza kunizoea maana namkaripia na mimi ni mkorofi (ni kweli), kwanza niko mpenzi wake wa kwanza.
Huyo mmoja kasoro zake zote nikitafuta chanzo ni hali duni ya nyumbani kwao ambayo imemuingia akilini na kwenye lifestyle. Anapenda sherehe kama MC, kuchangisha birthday parties, kwenda harusini kiholela na beach parties. Familia yao ina matatizo ambayo ukizaa naye tu lazima watoto wayaridhi na siko tiyari. We unaunganisha familia ambayo wajomba walikataa shule, binamu alijiua kisa umaskini, kule walikosa hela ya kwenda hospitali wakampeleka kwa mchungaji kuombewa. Tafrani tu.
Kinachokataliwa sio umaskini ni madhara yatokanayo na umaskini. Sasa nije kuoa miaka 5 au 6 baadae niambiwe nimebagua si kunisingizia, kwanza huyo matako makubwa najitahidi kumuacha. My worst nightmare ni itakuwaje nikimpa mimba? Maana habari za hubby na kunitajia majina ya watoto zimeanza.