inasemekana, kuanzia ethiopia hadi south, garama kiujumla hufikia hata 6m. hii ni zaidi ya ticket ya kwenda na kurudi Marekani. okota wabongo wa kawaida hapa waambie wanunue tiketi ya kwenda na kurudi marekani, uone. kutoka ethiopia hadi mpaka wa kenya huwa wanaandaa pesa ya kutosha, toka mpaka wa kenya waingie Tanzania hadi mnpaka wa zambia au malawi, toka pale waende hazi zimbabwe na kuingia south, kote huko kuna fungu lako. ni kama biashara ya madawa ya kulevya, vilevile walivyo kwenye mafuso wanakuwa wametoa pesa ndefu tu si chini ya milioni kila mtu ndio maana watu hawaachi hata wakamatwe vipi. Na ukikamatwa, wanasheria tunajua, kifungo au faini 20m. wanasevu kwa muda mrefu hiyo hela na nyingine wanatumiwa na jamaa zao ambao tayari wameshafika kule na wametoboa, na wakifika wanafanya kazi kwenye mikahawa na maduka yao. na kule wakifanikiwa huwa wanapanda ndege kirahisi kwenda ulaya na marekani.