Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Mpaka sasa nitaendelea kumsikiliza, maana baadhi ya mambo anayoyasema yana ukweli nusu-nusu. MOST OF YOU ARE NOT READY FOR THIS DEBATE.
Mkuu ukipata muda tuongoze kuchambua hizi hotuba za Polepole ili tujue kama tunalishwa matango pori au ni mmoja wetu?
 
Hii itawezekana vipi wakati mtandao wamejipenyeza kila mahali?

Huwezi tandika kitanda ulale wakati kuna chatu chumbani kwako, cha kwanza ni kumuondoa huyo chatu, ndiyo mengine yafuate.
 
Sikuwahi kukuona ukiongea kwa hasira hivi mkuu, ni kweli umekasirika sana na inaonekana yanayosemwa ni sehemu ndogo tu ya yasiyosemwa.
Well, kwa namna ambavyo mifumo ya kiutendaji kwenye vyombo vyetu vya usalama imeharibiwa/imemilikiwa, sijui hii meseji kwa ujumla wake unamtumia mwananchi wa kawaida au kuna masalia kati ya waliopo aliye na usafi walau 50% anayeweza kuanzisha mchakato wa mabadiliko na ikaleta matunda?
 
..yana ukweli nusu nusu ndio nini, wewe kabla ya Polepole kutoka kusema anayosema..ulishawahi kusema hadharani hata nusu ya haya unasema sasa? Nini kimekufanya utoke kuyasema SASA? Polepole kimtazamo ana-attack timu nzima inayoshughulikia USALAMA wa nchi hii km chanzo cha hali ilivyo sasa..imeanza lini, ilikuwaje, nani alizembea si hoja..HOJA ni nini kinapaswa kufanyika kuondoka hapa hata km ni kwa hatua moja mbele ni muhimu sana sabab itaweka maandalizi ya hatua nyingine mbele hata km ni hatua moja tena..si rahisi kuleta reforms/mabadiliko makubwa kwa mara moja kwa tatizo lililodumu muda mrefu na limejifungafunga km ilivyo sasa..! Unahitaji japo kwa sehemu kdg watu waliocraft part ya tatizo na sasa muda umewaruhusu kusimama upande wa pili kukataa kuendelea na hali ya kuumiza wengi! Binadamu huweza kuonekana kwa nje dhamira yake kwenye jambo fulani..Polepole ana dhamira njema na haijaanza alipojiuzuru ubalozi, imekuwepo muda wote..inahitaji nguvu ya ziada kupambana na uhalifu unaokukimu!
 
..ktk hili sikubaliani na wewe, nchi inasumbuliwa na kikundi kdg sana na kudeal nao ukiwepo umoja wa dhati miongoni wa raia, tatizo hili haihitaji wiki kulimaliza! na kuanza ukurasa mpya!
 
..inashangaza km leo ndio unafahamu si sawa kumuamini mtanzania, mbona iko wazi kbs toka zamani kwamba moja ya tatizo sugu linawahusu watanzania wengi ni UBINAFSI na UNAFIKI mtu yeyote mwenye sifa hizi huwezi kumuamini hata kwa sekunde moja! na hapa wapo wmejaa tele kila mahali! tabia hizi zimechagizwa na kabila mtu anatoka na imani aliyolelewa nayo!
Hata wewe uko kwenye category hiyo hiyo, ukisoma kwa kituo maneno yako yana hila ndani yake..hayatokani na kuwa na dhamira njema kusaidia nchi.
 
1970s watu hawakwenda china kusoma,ukasome nini 1970s china,wushu!?..
Unayajua mapana ya idara 1970s?
 
Umeandika mambo mengi mazuri ila kitendo cha Kumbagaza na Kumbananga dada wa Taifa Mange Kimambi na Shangazi wa Taifa Maria Sarungi hapo umeharibu kila kitu.

Kila mtu ana past yake, hii haimaanishi kuwa akifanya the right thing basi hiyo right thing haina maana.
 
Naogezea na ili juzi mahakamani alisema rasi Samia anafuatilia kesi yake kitu ambacho sio kweli Lissu ana mazuri yake sema hanaga subira. Lissu na Polepole ni watu tofauti sana polepole yeye CCM kwanza ndo anachoamini Lissu ni Muumini wa mifumo kua huru
 
Haya WAKUU, mimi NIWATAKIENI KILA LA KHERI

===================================================
​
Na Wanamtandao watajitahidi kuwagombanisha polepole na Lissu niko hapa Lissu inatakiwa kuruka huu mtego kwa akili sana akitoka achane na mambo ya polepole
 
LIPOTEE MARA NGAPI? WEREVU MWINGI MBELE KIZA..MULIDHANI KUIBAKISHIA ZANZIBAR UZANZIBARI WAKE NDIO KUIUA KIMKAKATI ILI MUUNGANO UWE NI LONG LASTING. IT WAS ONE OF YOUR BIGGEST HISTORICAL MISCALCULATION. ZANZIBAR NA MUUNGANO NI SAWA NA MTOTO ALIEKWENDA MATEMBEZI...SIKU ZA MATEMBEZI ZIKIISHA ANARUDI KWAO..JUST THAT!!!! THE REMAINING TO YOU IS KATIBA MPYA...NOTHING MORE.
 
So wali-recruit toka 'vyuo vikuu' vya nje?, palikua na wanafunzi wa kutosha watz huko vyuo vikuu vya nje kiasi cha kuweza kujaza nafasi baada ya 'safisha safisha' idarani?
Recruitemnt ya Idara huwa inafanyika hadi ngazi za shule za sekondary.
 
Hii hoja yako ni mfu. Nani kakumbia wafanyakazi wa Idara wote lazima wale wasomi wa vyuo vikuu? Recritment ya Idara huwa inafanyika hadi kwenye ngazi za shule za Sekondary na mitaani pia. Hao wasomi wa ngazi za juu wanaohitaji siyo wengi kiasi cha kuhitaji kuwa na vyuo vikuu vingi. enzi za Nyerere hatukuwa na vyuo vikuu vingi wala hatukuwa na wasomi wengi wa vyuo vikuu lakini Idara yetu iliheshimika na ilitenda kwa weledi. Na hata baada kuivunja na kuiunda upya mwaka 1975 bado ilifanya kazi bora.
 
Ujumbe mzuri sana huu
 
Mungu ibariki Tanzania, wabariki viongozi wake pamoja na wananchi wake, Bariki na vinywa na mioyo ya watawala wa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…