Hapo tambua kuna mambo mawili,kuna kusoma na kuelimika na kutumia elimu kuratibu mambo,na kunakusoma ukaelimika na kushindwa kuratibu mambo kisomi,hili la kwanza,
Pili hakuna binadamu asie na mapungufu,hivyo basi kumhukumu mtu kwa mabaya na kushindwa kuona mema/jema lake nalo ni tatizo,
Lukuvi pamoja na mapungufu yake uswaiba wake na mwendazake vyovyote ilivyo hatuwezi kukataa kukubali amejaribu kuinyoosha wizara ambayo wengi ilikuw a changamoto tena kaalamoto,ardhi imekuwa wizara yenye mchango unaoonekana kwenye kulitunisha kapu la serikali,mifumo aliyosaidia kuiweka kukusanya mapato imetusaidia wengi katika kale ka ukakasi na mifumo ya kimazoea ya utendaji wa wizara nyingi.
Leo hii unamiliki kiwanja huko newala wewe uko muleba unakusanya uduvi kuitikia wito wa kujiajiri ila,muda wakulipa kodi ya ardhi ukifika unajiwekea kasaliokako kwenye simu na kuitisha control no yako ya malipo mnamalizana na Lukuvi,unaendelea na majukumu yako kwa amani.
Popote watakapokuweka Ndugu yangu Lukuvi,tambua baadhi yetu watanzania tutakuheshimu kW mema yako katika kuichakata na kujaribu kuipa sekta ya ardhi thamani yake,umejaribu kufanya jambo,umejaribu kwa weledi mkuu,hayo mengine waachie wenye mamlaka ya uteuzi wako.