Tusisahau kuwa Dkt. Eliona Kimaro ni Mwajiriwa wa KKKT anayelipwa mshahara kila mwisho wa mwezi!

Tunakumbushana tu kwa sababu maneno yamekuwa mengi kufuatia Mchungaji Kimaro kupewa Likizo ya lazima na mwajiri wake ambaye ni KKKT.

Hiyo ni kawaida sana kwenye ajira za Sekta binafsi

Tusikuze mambo na kumpa faida shetani
Na huo mshahara sisi waumini ndio tunao toa. Hata askofu ana lipwa na waumini. Hivyo waumini ndio waajiri wa watumishi.
 
Wewe upo wapi tukufuate ambako una uhakika wa kwenda Mbinguni?
 
Tunakumbushana tu kwa sababu maneno yamekuwa mengi kufuatia Mchungaji Kimaro kupewa Likizo ya lazima na mwajiri wake ambaye ni KKKT.

Hiyo ni kawaida sana kwenye ajira za Sekta binafsi

Tusikuze mambo na kumpa faida shetani
Watu wana miheamko sana. Na asipokuwa na akili akadhani yeye ni Mkubwa kuliko Kanisa atapotea...
 
Ila Malasusa kaingia mno kimwili.

Maonyo yalitosha , ona sasa navyo kanisa liko utupu.

Au tukumbuke yale ya yule mke wa mtu hadi kufikia kuzaa.

Wote wana madhambi tena ya aibu, hata Kimaro alipowasifia Waislam na Wakatoloki alikuwa na haki.

Kwani ya mkuu huyo wa jimbo je, hatuyajui?
 
Kuna tetesi wachungaji wote wa Dayosisi aliyozaliwa Dr Eliona Kimaro wanaandaa mgomo na maandamano makubwa kupinga alichofanyiwa mchungaji Kimaro
 
Mchungaji Kimaro mwenyewe ameridhika na maamuzi

Tatizo liko hapo Ufipa st ndio mmegawanyika
 
Hv unajua walevi ni watu wanaopatana zaidi na kusaidiana kuliko watu wanaoshinda makanisani!?
Baar is my church.
 
KKKT iliwahi kusimamia mauaji huko Meru Ili wazuie kuanzishwa kwa Dayosisi ya Meru.
Ila Wameru walikomaa hadi tone la mwisho na Dayosisi ikapatikana.
Ili KKKT Ipate amani , hadi Shoo na malasusa waitwe mbinguni.
Vinginevyo hakuna
 
Swala la Mwajiri na Mwajiriwa Waumini wamelishikia bango

Hawajui hata Sheria ya Kazi
1. Wapi sheria ya kazi imetamka likizoya siku 60?
2. Kapewa likizo (batili) na mtu asiye mwajiri wake (Msaidizi wa Askofu, wakati mwajiri Ni Katibu Mkuu, Dayosisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…