Tusiukubali mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu zozote zile. Utakuwa ni mtego utakaotunasa kama nchi

Uzuri wa JF ni kama maktaba,naona kuna watu wana hangaika Ku-prove Magu alikosea ktk swala hili la Bagamoyo,ila kama mradi huu ukipitishwa kuna siku tutarudi kuuzungumzia huu uzi huku tukiwa na majonzi ya kupigwa na Tanzania tuko vizuri sana kupigwa kwenye mikataba ni swala la muda tu.
JF inaweka kumbukumbu katika mijadala yetu, hapo chini nimekuta kuna mchangiaji ameweza kuweka mawazo yake na mchango.
C&P.

Moja ya maoni ya wadau👇

Najua topic imepita, lakini ninajua kidogo kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo na napenda kumuunga mkono Mhe Spika kwa hoja zifuatazo. Na naamini Serikali yetu itazichukulia kama ushauri wa Mbunge kwa Serikali, ambao ndio wajibu wetu wa msingi kama Wabunge.

Muhimu kujua background ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Kwanza, mradi huu ulibuniwa na Serikali yetu kama Bagamoyo Special Economic Zone mwaka 2004 chini ya Mpango Kabambe wa Ujenzi wa Sekta Mpya ya Viwanda. Serikali ya Japan ndio ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa “Tanzania-Mini Tiger 2020” na ulikuwa chini ya Wizara ya Viwanda.

Mamlaka ya Bandari nayo ilibuni Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028) ambao ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022 ili iwe tayari kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo. Kwahiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba: (a) Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina; (b) mradi wa Bandari ya Bagamoyo sio ni mradi wa Bandari, bali ni mradi wa Ukanda wa Kiuchumi ambao unaendana na mji wa viwanda.

Mwaka 2009 Mamlaka ya Bandari, kupitia kampuni ya Hamburg Port Counsulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na
kuona una manufaa kutekelezwa. Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama Mradi wa Taifa wa Kielelezo.

Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza katika Mradi wa BSEZ na Bandari ya Bagamoyo. Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia Taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute” (“STEPI”) ilikamilisha Upembuzi Yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza “Bagamoyo High Technology Park” kwa kushirikiana na EPZA pamoja na COSTECH. Kwahiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo sio uwekezaji wa Wachina pekee, kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka pesa yao nyingi. Na Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (“FYDP II), Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ) ni Mradi wa Taifa wa Kielelezo. Mradi huo unatarajiwa kuwa utavutia uwekezaji wa Dola za Kimarekani bilioni 10; utakuwa na Viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya Utatu wa Serikali ya Tanzania, China Merchants na Mfuko wa Uwekezaji wa Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia Mikataba ya Uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: (1) utatutwika madeni kama vile Kenya na Sri Lanka ambapo Wachina walilazimika kutaifisha Bandari; (2) tutaua bandari ya Dar es Salaam; (3) haturuhusiwi kuendeleza Bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu pale Bagamoyo kwa miaka 99.

Hoja hizi zote sio za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wana-struggle namna ya kuzijibu kwasababu zinatolewa na watu wakubwa, na hao wawekezaji, hasa wa Oman, ni mamlaka za Serikali na wasingependa malumbano na Serikali yetu.

Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa sio ya kweli: kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo tunachukua. Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

Hoja ya pili kwamba tutaua bandari ya Dar haina mantiki, kwasababu hata kabla Wachina hawajafika ilikuwa ni ndoto na mipango ya Mamlaka ya Bandari kujenga Bandari ya Bagamoyo. Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028), wenyewe Mamlaka ya Bandari walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar sio bandari shindani. Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchi mwetu. Full stop! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port). Meli hizi, ambazo zitakuwa zinaongezeka kadri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 30, 50 ijayo, Bandari ya Dar ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi kujenga Bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza Bandari yoyote kwa miaka 99 na tuwape wao bandari hiyo bila sisi kutia mguu pale sio ya kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa hayo madai. Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka hela yake mwenyewe kwenye mradi atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession. Je, ni mingi au ni michache? Inategemea pesa iliyowekwa (US$10bn) na standard practice kwingine duniani. Reli ya kuunganisha UK na France, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari standard practice ni miaka 25-40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji. Cha msingi kwa timu ya negotiators wetu ni kupata financial models za wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani. Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya Bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizito bandarini.

Suala lingine la kutazama katika kufanya maamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwasasa ndio kinara wa biashara ya import and exports duniani. Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 inayokuja. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China na Afrika ya Kati na Kusini, zitafikia katika moja ya Bandari za Mwambao wa Mashariki ya Afrika, kama Mlango na Kituo Kikubwa cha kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na Reli ya Kati na TAZARA, itakuwa haina mshindani Nje ya Tanzania katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu Kaskazini yetu wanapigana kufa na kupona mradi huu usitokee. Kwahiyo mtaona disinformation nyingi kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie ule mradi Kenya kule LAMU. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzen kuzungumza na China Merchant kuwashawishi waende kwao. China Merchat walikataa na ndio walikutana na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa. Na majuzi, tarehe 25 Machi 2021 wameandika barua tena China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao (barua nimeiona).

Mwisho, nitamalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, wazungu waliona potential ya location ya Dubai kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wakajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30. Washauri wake wakamwambia tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu. Sheikh akawauliza “sisi tuna pesa ya kujenga?”, wakajibu hapana, akawauliza “tutaipata lini”, wakasema hatujui, akawauliza “Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?”, wakajibu ndio, akawauliza “baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?”, wakajibu hapana, akasema “tuwape”. Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya makampuni makubwa duniani. Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari, wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya logistics.

Mpendwa wetu hayati Rais Magufuli alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi na kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa kwenye mradi wa Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya negotiators itakuwa makini kuzingatia maslahi ya nchi.
 
1.Spika wa bunge hajasema kama aliuona huo mkataba bali alifanyiwa "presentation".
Presentation na mkataba ni vitu viwili tofauti kabisa. Presentation ni kama summary tu ambayo muwasilishaji atachagua vitu muhimu vizuri na kuviwasilisha kwa mbwembwe nyingi kukufanya uvutike.

2. Spika wa bunge letu sio mwanasheria, sio mtaalamu wa kodi, sio mtaalamu wa uwekezaji hasa wa bandari na ardhi.

3.Spika wa bunge anasema alikutana na bodi ya hiyo kampuni "kwa bahati mbaya!" Wazee wachache waliobaki kwenye hiyo bodi walimsisitiza wao wanaoifahamu Tanzania vizuri wakiondoka itakuwa vigumu kuipata hiyo fursa tena!
Still bado huu mkataba ungewekwa wazi au tuachane nao.
 
Hayo mawazo yao ila kilicho andikwa kwenye mkataba hawajakiona,Magu aliupiga chini baada ya kuona unauumiza Tanzania.Kama wakitaka wauweke wazi tusijie kulia kilio anacho lia Zambia na Kenya.Wachina si watu wazuri.

Tuna sababu moja kubwa ya kuukata Mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo nayo ni historia mbaya ya China kona mbalimbali za dunia walipotekeleza miradi ya aina hii au walipozikopesha nchi mikopo mikubwa ya miondombinu. Wamechukua bandari Sri Lanka, Pakistan, Australia na Djibouti kupitia mikataba ambayo haieleweki ni yenye utata sana.

Kama huko wameweza kufanya hivyo sisi hatutaweza kuwadhibiti na kuibakiza bandari ya Bagamoyo kuwa bado mali yetu endapo tukiwakubalia wajenge bandari hapo.
Tusijidanganye, sote tunafahamu jinsi gani mikataba midogo tu ya madini imekuwa changamoto kubwa kwa taifa hili, huu ukizingatia na usiri wa mikataba utakuwa funga kazi, tutauzwa mchana kweupe kama enzi za Mangungo wa Msovero.

Tukubali tu kwamba wao ni wajanja na kutekeleza kwa miradi ya aina hii duniani kumewapa ujanja zaidi. Tusikubali bandari zetu kujengwa na kuendelezwa na wageni kwa sababu yoyote ile. Kama tunafikiri ni muhimu sana na tunatakiwa kuwa na Bandari Bagamoyo tukope pesa tujenge wenyewe, vinginevyo tutaiuza nchi yetu nzuri.
Kwani mkataba umeusoma na unasemaje na hivyo vipengele vya kipuuuzi vipoje!?
 
Hayo mawazo yao ila kilicho andikwa kwenye mkataba hawajakiona,Magu aliupiga chini baada ya kuona unauumiza Tanzania.Kama wakitaka wauweke wazi tusijie kulia kilio anacho lia Zambia na Kenya.Wachina si watu wazuri.
Basi wacha waweke wazi huo mkataba nasi tuweze kuuona na kuuchambua.
 
Hatujasikia nchi nyingine kubwa duniani zikiwa zinachakua bandari za nchi nyingine katika mazingira ya utata zaidi ya China, kwa nini tuweke imani yetu kwamba hazitatokea figusu zitakazopeleka Bandari ya Bagamoyo kuchukuliwa na wao?

Kama miaka yote tumekuwa tunalizwa katika mikataba midogo ya uekezaji katika miradi ya madini, maji, ujenzi n.k tumepataje uwezo mkubwa ghafla wa kuweza kuingia mkataba mkubwa kabisa kuwahi kuingiwa na nchi na wawekezaji/wafanyabiashara ambao wamekuwa na utata mkubwa sana sehemu nyingine duniani?

Kuna uwezekano wowote wa huu mkataba kuwekwa hadharani kila raia anayetaka kuusoma aweze kuupitia? Kama hakuna uwezekano huo kwa nini tuwaamini wanaotuambia mkataba ni mzuri? The default position kabisa katika hali si kuwaamini upande mwingine waliouona na kutuambia tunapigwa?
JF inaweka kumbukumbu katika mijadala yetu, hapo chini nimekuta kuna mchangiaji ameweza kuweka mawazo yake na mchango.
C&P.

Moja ya maoni ya wadau[emoji116]

Yoda ndugu yangu usiwaamini wanasiasa hata kidogo, mwanasiasa pindi anapolitaka lake atakuaminisha kitu chochote hata kuweza kukuambia wewe ni mkubwa wa kiumri kuliko mzazi wako. Bila ya mkataba kuwa wazi basi tusijepandisha presha bure, kwani vichwa vyetu vina mambo mengi ya kufikiria.
 
Nilisikia wachina wakiukamilisha wataanza kupokea pesa wao kwanza kwa miaka kadhaa, kama ni kweli huu ni ujinga.
 
Kitendo tu cha kuruhusu wajinga wawe huru kukushauri ujinga wao ni dalili tosha wewe ni dhaifu na ipo siku wataweza kukuingiza mkenge, hiyo ndio hali ya SSH.
Aliwahi kukaririwa sehemu Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere akisema ;
Mtu mwenye akili timamu na anafahamu kuwa unaakili timamu alafu akakwambia kitu cha kijinga nawewe ukakikubali atakudharau sana !

Wachina & Ndugai na Co. Sijui kwann wanatuambia vitu vya kijinga namna hii Na wakifaham kabisa hili sio Taifa la wajinga!
 
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa aliekuwa mkuregenzi wa bandari, ni mbumbumbu tu au mchumia tumbo anaeangalia maslahi yake binafsi na sio taifa anaeweza kukubaliana na masharti haya ya kidhalimu.
1. Wanataka wapewe bandari l kwa miaka 99 kinyume na miaka 33 ambayo serikali ina afiki. Kwa mujibu wa makadirio, inaonyesha gharama zitarudi ndani ya miaka 10 mpaka 15 lakini wao wanataka miaka 99.
2. Bandari nyingine yeyote isiendelezwe kwa kipindi hicho.
2. Wanataka wasamehewe kodi zote zaidi ya misamaha inayotolewa na TIC kama kivutio kwa wawekezaji. Yaani kwa miaka 33 wasilipe kodi.
3. Wanataka wamilikishiwe ardhi iwe yao kinyume na taratibu ardhi inatolewa kwa mradi.
4.wanataka watozwe gharama za chini za umeme, maji na gesi.
5. Wanataka wasilipe mrabaha wa kutumia bandari ambao hulipwa na muendeshaji kwa mamlaka ya bandari kama ambavyo TiCTs hulipa TPA.
6. Wanataka wapewe ardhi pembeni ya bandari kwa ajili ya kujenga magodown na pia ardhi isitozwe gharama za banadari kavu..
7. Wasilipe tozo za ardhi...
Angalia hapa akieleza...
 
  • Thanks
Reactions: IoT
Baada tuu ya deusdedth kakonko kutumbuliwa wimbo wa bandari ya bagamoyo ukashika kasi sana .
 
Tuna sababu moja kubwa ya kuukata Mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo nayo ni historia mbaya ya China kona mbalimbali za dunia walipotekeleza miradi ya aina hii au walipozikopesha nchi mikopo mikubwa ya miondombinu. Wamechukua bandari Sri Lanka, Pakistan, Australia na Djibouti kupitia mikataba ambayo haieleweki ni yenye utata sana.

Kama huko wameweza kufanya hivyo sisi hatutaweza kuwadhibiti na kuibakiza bandari ya Bagamoyo kuwa bado mali yetu endapo tukiwakubalia wajenge bandari hapo.
Tusijidanganye, sote tunafahamu jinsi gani mikataba midogo tu ya madini imekuwa changamoto kubwa kwa taifa hili, huu ukizingatia na usiri wa mikataba utakuwa funga kazi, tutauzwa mchana kweupe kama enzi za Mangungo wa Msovero.

Tukubali tu kwamba wao ni wajanja na kutekeleza kwa miradi ya aina hii duniani kumewapa ujanja zaidi. Tusikubali bandari zetu kujengwa na kuendelezwa na wageni kwa sababu yoyote ile. Kama tunafikiri ni muhimu sana na tunatakiwa kuwa na Bandari Bagamoyo tukope pesa tujenge wenyewe, vinginevyo tutaiuza nchi yetu nzuri.
Mimi naona uwekwe wazi tujue yaliyomo maana spika kasema alichoambiwa raisi na walichoambiwa wao ni tofauti raisi alipotoshwa. Sasa ili kujua ukweli waupeleke bungeni wachambuzi wa mambo wauchambue kama wanavyochambua ripoti ya CAG, japo pia nina mashaka na uelewa wa wabunge wetu kama wanaweza kusoma kikataba wakaelewa
 
wachina waliambiwa waende wajitafakari then warudi sasa kama wamejitafakari na wameamua kurudi basi tuwekwe wazi vipengele vipi wamebadili na nini hasa kimewavutia hawa viongozi wetu kuweza kuukubali huu mradi kirahisi hivyo ilihali mradi ulipingwa vikali tena kwa hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lupo ktk mktataba hatuwezi kukubaliana na kitu hatujaona na kuchambua
 
wakitaka ukweli waweke Mikataba tena kwa kiswahili kila mtanzania asiye jua kiingereza haweze kusoma . waache kuongelea bungeni
 
Back
Top Bottom