Tusiukubali mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu zozote zile. Utakuwa ni mtego utakaotunasa kama nchi

Kwani mkataba wake unasemaje? Kwani naona maneno mengi, si uwekwe wazi ndio watu waamue? Huyu anasema vile, huyu anasema hivi hata hatuelewi, utakataaje/utakubalije kitu ambacho hujijui?
Ila unakubali ambacho hukijui?
 
Baada ya mzee magufuli kuondoka,kuna watu watakua wana pressurize mama kuhusu huo mradi.sidhani kama ataweza kusema No.
Kama atashindwa ni bora hata kukaa pembeni tu, kwani uRais ni lazima?
 
Daaaa!!hivi nyie huwa hamsomi mchango wa mtu hadi mwisho, ?ila ni kurukia tu kujibu!!niliposema kuwa unakubalije/unakataaje kitu ambacho hukijui nilimanisha kukubali??
Hiyo ni Fallacy, kama hukubali means unakataa, na haukatai means unakubali, na sio both at the same time. Hivyo hiyo ya pili ni kama hukuisema, by logical implication.
 
Naamini hakuna mtanzania hata mmoja makini anayepinga ujenzi wa bandari ya Bagamoyo sababu manufaa ya bandari yanajulikana. Tatizo ni mashrti ya huo mkataba kama tulivyoambiwa ni hovyo labda kama viongozi wetu wanatuambia uongo lakini kama kweli ndiyo hivyo hata mimi siwezi kukubali kuuza nchi kijinga namna hiyo.
 
Kwani hatuwezi kwenda nchi za ulaya kwa mabeberu kuomba msaada. Wazungu hawanaga noma tunaweza kuwapa hekari 20000 sehemu walime miaka mia alafu watujengee bandari bure tuindeshe nwenyewe. Mchina masharti yake yakukupiga tu.
Mkuu ni kama TANWAT, nasikia JKN alimpa malkia elizabeti eneo la Njombe wali me miti,chai na wao wAkajenga barabara ya lami Songea Njombe ambayo ipo mpaka leo na mkataba wa miaka 100 unaelekea mwisho.
 
Kuna watu bungeni serikalini walisha kula hela ya mchina ili kupitisha dili zake, na ndio hao wameanzisha mjadala wa kujengwa bandari ya bagamoyo. Mchina ni mkoloni mpya anaeingia kwa mbinu mpya, japo hazipishani sana na zile za enzi za Mangungo. Tofauti ni kuwa Mangungo hakuelewa kilicho andikiwa kwenye mikataba, wa leo kalamu ya ku-sign mikataba inawekwa juu ya box la pesa.
 
Sema kuna MTU anaitwa ndugai anasomeshewa mtoto wake China, Ndugai ni wa kupigwa makofi hazarani haoni tabu wanayoipata wasri Lanka waliwapa wachina Bandari, kama tunavyotaka kuwapa Bagamoyo!? Hili zee linafki sana amekufa JPM limeanza tena wakati Jpm aliwaambia ni kichaa tu anayeweza kukubali ujinga ule.
 

Kama unakumbuka, mwezi January 2021 Foreign Minister wa China(Wang Yi) na diplomats wengi from China walikuja TZ na wakaenda mpk Chato kwa mazungumzo ya faragha na JPM.

Huo ugeni sio wa kawaida, mwenye macho na maskio kazi kwenu. It was a matter of time ila Mchina kashawin.
 
Bunge lipi la kujadili mikataba kama Ndugai ameibariki?
Hao wote waliingizwa kibabe na Meko Hawakushinda sasa wataachaje kuunga mkono kitu ambacho Ndugai amekibariki?
System ndio inayoamua tunamtaka huyu ...huyu hatumtaki anapenda kupinga pinga sana ..Nimekuelewa sana Pro Assad 60% ya Viongozi hawana weledi
Na huu ndio ukweli

Sent from my HUAWEI CAM-L21 using JamiiForums mobile app
 
Your browser is not able to display this video.
 
Ugeni ule ulifanikisha mkataba wa ujenzi wa SGR Kahama - Mwanza
 
Hii issue ya Bagamoyo inautata sana...

Na hii yote ni kwa ajili ya yule fulani na mambo yake...
 
Au cyoo tusikubalii kwan wanachukua maoni yetu ndo mkataba usainiwe..!? We pambania life lako liwe njemaa mengne utayakuta uko mbele ya safari
 
Kusomeshewa mtoto hiyo sio hongo, ni hela kidogo anaweza ilipa, hata iwe level ya PhD, ni chini ya £10,000 kwa mwaka. Hongo kupitisha mkataba wa kukufilisi mtanzania ni balaa.
 
Pamoja na kumchukia Kenge mfu kwa kuua na kutesa watanzania wengi,
Namchukia mchina mara mia
Hii clause ya usijenge wala kuendeleza bandari nyingine kama ukweli ni UMAFIA tosha kuaamini ya hata mchina kutaka kusimamia na kukusanya mapato mwenyewe.
Port of Entry iwe bandari, airport au land border ni mali ya nchi si ya kumpa mchina asisimamie kama alivyochukua airport Zambia
 
TUKUMBUKE!,Sisi Tanzania tunapaswa kuwa na bandari nyingi kuliko nchi ya Afrika Kusini.
Tanzania tunazo bandari muhimu(Tanga,Kilwa,Lindi,Mtwara)! Tena kuna zile bandari za Ziwa victoria,Tanganyika na ziwa Nyasa).
Kuwa na bandari nyingi ni sahihi kabisa ila sio kuua zingine. Bandari ya Bagamoyo moja ya Terms zake ni kuziua bandari zingine za mwambao huu kwa Tanzania mpaka ile ya Mombasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…