Tusiwabeze wanaosomesha watoto shule za Tsh. Milioni 40

Kweli kuna ndugu yangu anafanya kazi shule moja ya awali ipo mikocheni inaitwa lexis, nilijitia kihelehele kutaka kumpeleka mwanangu akaniambia hii shule ada yake huiwezi kwanza wanaosoma hapo ni watoto wa mabalozi, mawaziri na madoni kucheki ada nursery tu ni usd 3500 kwa mwaka halafu ni day, nikasema kweli hii shule siiwezi ila hao wanafunzi wao wa miaka 5 wanafanya vitu mtoto wa darasa la pili au latatu wa english medium schools za milioni 2 hadi 4 kwa mwaka hawezi kufanya maana nilienda kwenye mahafali na exhibition ya shule yao. Tuzidi kutafuta hela kwa bidii kubwa
 
cha mtoto hapo, braeburn ama internetional school of Tanganyika, chekechea milioni 20 huko
 
Sema wamekudanga sana.
IST ipo Dar, na kusoma hizo shule huna guarantee Ya kufanikiwa maisha.
 
Usome shule ya kata hio connection unatoa wap?,
 
Hao wanasoma sio kutaguta ajira kama mimi na wewe.

Hao tayari kila kitu kiko poa.
 
Kuna ukweli fulani hapa.
 
Zamani nilikuwa nabeza, leo hii dogo yupo la 4 ada ni 3m. No problem. Elimu ni muhimu
Kwa sababu unazo. Kwa hiyo akimaliza hilo la Saba atapata Cheti cha Diploma?

Bahati mbaya akimalize Chuo aje na bahasha kutafuta kazi mshahara wa milioni moja kwa mwezi.

Hii ni hasara kubwa mno.

Kwa kuwa unazo sawa endelea lakini usisahau kumwekea mazingira ya kiuchumi hapo baadae asitarajie ajira.
 
[emoji23][emoji23]
 
Inshu sio walimu inshu ni wanafunzi anaokutana nao pale ni watoto wa mabalozi wa nchi mbali mbali watoto wa wanadiplomasia hao marafiki zake mwisho wa siku ndio watakaompa maconnection
Na mimi nachojua ni hivyo. Lakini pia wanaosomesha huko ndio hawa hawa mafisadi wenye pesa ambao watoto wao hawahitaji elimu hiyo kutoka kimaisha.

Yaani hata asipoenda kusoma huko yeye maisha yake tayari ni mazuri.
 
Yaani unataka kulinganisha kusoma Feza, International school Tanganyika, havard, na kusoma udom temeke secondary!?
We jamaa acha utani,hizo shule na vyuo vya kishua vina miundombinu Bora na waalimu wenye weredi. Mtoto anapata mafunzo kwa vifaa Bora,
Sisi tulijifunza practical physics, chemistry kwa nadharia tu, chemical hakuna, huwezi kulinganisha na wanaosoma na vifaa duni.
Ukiwa DIT,practicals unafanya na mashine za kizamani zilizotolewa msaada na Soviet Union, ukienda field tanesco,unaishia kufunga service line, harafu unataka Uwe engineer kama aliyetoka havard!
 
wachaga mna sifa za kijinga sijui kwanini hata hamuoni aibu? nyie mnaumwa siyo bure.
 
Acha kutulisha matango pori ndugu. Kwa hiyo wote waliofanikiwa hapa Tz wamesoma hizo shule? Theory ya maisha ni complex sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…