Tutajie orodha ya kozi ambazo hazitoi ajira ili tupate kuzifahamu

Asante mkuu.
Nashukuru Mungu Lugha iko vizuri sana.
Kuna raia mmoja wa Spain tulikutana kwenye mihangaiko yangu, nae alisema kitu juu ya actuarial science.
 
Kwenye Kujiajiri Mchawi Capital kaka.....
Ni kweli mtaji ni kikwazo. Ila usisubiri hadi uwe na mtaji mkubwa wa mamilioni ya shilingi ili uanzishe kitu chako. Anza na hicho kidogo ulichonacho.
Kwenye Biblia Mungu alimuuliza Musa una nini mkononi mwako, Musa akajibu, fimbo. Fimbo ile ile ilitumika kufanya muujiza. Soma Kitabu cha KUTOKA

Kutoka 4:1-5
[1]Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.

[2]BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo.

[3]Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.

[4]BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia; (akaunyosha mkono wake akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mw

[5]ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.
 
Nyie sio ndio mnabaki chuo nakuanza kuja na matheory mzee. Watu wa mathematics aio wakuka kitaa bwana nyie ni watu very important ni kubukua tuu hapo chuo
Nilisoma hiyo course ni ngumu haswaa, ila haina fursa kitaa, sema binafsi ilinipa ajira japo sio rahisi kwa wanaohitimu miaka hii.
 
Boss unafanya vizuri ila kukimbia nchi ni uoga wa maisha. Mbona watu wanafanikiwa hapahapa.
Sijasema uoga. Ni kutafuta green pasture, pia kama nchi haiheshimu watu wenye fani muhimu ya nini kuendelea kuishi sehemu ya hivyo? Dawa ni kwenda wanapo value fani za watu. Mimi nawaunga mkono wanaotimka kwenda kwenye nchi za waliostaarabika na kuheshimu ujuzi
 
Nilisoma hiyo course ni ngumu haswaa, ila haina fursa kitaa, sema binafsi ilinipa ajira japo sio rahisi kwa wanaohitimu miaka hii.
Na hili ndio tatizo la nchi za africa ndio maana wadhungu watatawala dunia tuu
 
Na hili ndio tatizo la nchi za africa ndio maana wadhungu watatawala dunia tuu
Hii course iko njema maana mtu anaweza fit kufanya kazi kada mbalimbali ila bahati mbaya waajiri hawaijui hii course.
Kazi zote zinazohusu takwimu, mipango, usafirishaji, baadhi ya mifumo ya computer n.k kote huko ndo kwao hawa watu.
Dunia ya kwanza wameiboresha course hii kwa kuiunganisha na course nyingi za computer hivyo kuwa rahisi kutengeneza na kuvumbua mifumo mbalimbali lakini huku kwetu tunaishi kivyetu vyetu na hizi akili kubwa zinaishia kuuza icecream mtaani.
 
Vijana tujikite katika mawazo ya kujiajiri na siyo kuajiriwa hizo kozi utakazo ona zinatoa ajira unaweza kuta uwezo wa kuajiri ni asilimia kumi tu ya Watu kwenye uhitaji, hivyo suluhisho ni kusomea kozi inayokuwezazesha kujiajiri, somo LA ujasiriamali lipewe kipaumbele katika kozi zote
 
Kweli kabisa...hna nchi inayokuwa donor countey bila kuwa na great advances in acience and technology ambayo vyote hivyo hutegemea mathematics. Katika watu ambao walitakiwa kusoma bure yaani nchi inagharamia kila kitu ni watu wa namba. Na kuhakikisha wanapata employmwnt kwenye research institutes.

Huu ufala wa kusifiana biashara za survival mode ni ujinga tuu. Mtafanya biashara but mwisho wa siku viwanda machinery zote zinaletwa na wadhungu...bado utakuwa mtumwa tuu.
 
Huo ndo ukweli, ukiwatumia watu hawa kwenye tafiti zinazohitaji akili kubwa, hakika watakuzalishia vitu vikubwa ambavyo hautaamini, ila ukija kitaa bora aliyeamua kusomea ualimu akafundishe azalishe D zake mbili kila mwaka form four.
 
Na ndio hapo tunafeli na tutaendelea kufeli , hatu value proffessions ,wenzetu wana value proffessions ,Sisi mtu akiongelea udhaifu wa hii nchi kutovalue proffessions watu wanakebehi na kuandika ujinga ,na imekuwa hivyo Africa nzima ,kama hatuwekezi kwenye proffessions kuhakikisha hawa wanaograduate wanakuwa channeled katika mkondo wa kuadd value katika uchumi kupitia proffessions zao , hatutoboi nakwambia , huwezi kuwa na graduates mfano mechanical engineer na agricultural Engineers thousands of them in the streets wanafanya umachinga halafu ukajidanganya siku moja utapata maendeleo kwenye hiyo sekta ya kilimo .Si bora mfute hizo courses huko chuo ,muache kupoteza kodi za wananchi na muda wa wanafunzi ili mjenge taifa la illiterates na wachuuzi ?
Mfano nilishawahi andika humu kuhusiana na revolution Tu inayoweza patikana kwa kuanzisha serious incubator ya kufanya research na building ya modern mechanical equipments mfano pumps , matrekta nk ambazo tunaweza tukazitengeneza na zikasaidia kuondokana na kilimo cha ovyo cha jembe la mkono ,kuzalisha ajira na kuleta tija na ufanisi kwenye kilimo kwa kuongeza uzalishaji .
Tuna chuma kule mchuchuma na Liganga why ,hatufanyi mambo ya maana kama haya ,mjapan kutengeneza vitu kama matrekta ,ndege ,magari na heavy diesel equipments nyingine za ujenzi ,kilimo na madini alijifunza kule USA na then akaenda kuimplement kwake kazalisha makampuni ambayo yamedumu na yameshika soko la dunia mpaka leo mfano Nissan ,Toyota ,Suzuki , Komatsu NK Sisi tunabung'aa hapa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…