Tutaona mwisho wenu ninyi timu kusifia sifia ya Rais Samia

We mpuuzi katiba lenu bovu ndo limemuweka ikulu kama slivyoweka ikulu jiwe
Sisi tunampimia tu
Tunachofurahi ni kuwa amedenounce ukatili wa mtangulizi wake,at least kwa maneno kwa sasa
Tunampimia kwa siku hizi za mwanzo
Akizingua huyu rais atatukuta hapa tunamngojea kumpa makavu mbashara kama jiwe
We don"t discriminate
 
Sukuma gang + Mataga = Stupidity.
 

Mlizoea kuishi kwa kufanyia watu udhalimu, sasa zama zenu za udhalimu zimefika mwisho, itabidi muanze kula vya halali. Huyo mama anasifiwa kwa kujitenga na udhalimu na kuamua kuongoza Kiutu, lakini akiamua kuongoza kidhalimu basi hatasifiwa, na nyie mnaotegemea kuteka na kuua watu, mtarudi tena kwenye zama zenu za kujidai.
 
Ukiwa objective maisha ni mazuri tu. Wakifanya ujinga unakemea na wakifanya mazuri unasifia. Shida ni wale ambao wako programmed kusifia kilaaaaaaaaaa kitu, na wale ambao wako programmed kupondaaaaaaaaa kila kitu.

Ukiwa objective utasema mama ameanza vizuri, na akija kuanza kuharibu pia tutapiga kelele.
 
Sina Masilahi yoyote mimi.

Mimi ni mzalendo tunahitaji kuwa na misingi imara ya uongozi.

Uongozi imara ni kuteka wasiokusujudia, na kubambikia kodi wananchi ili uwapore fedha zao? Kwa sasa Mungu kutuondolea yule muovu kwa kufanya mabadiliko bila damu kumwagika. Katafute kazi ya halali, hiyo ya kuteka boss wenu hayupo tena.
 

Wakati huo watu wakimsifu JK ww ulikuwa upande gani? Naona unatoa mifano ya enzi za zama damu ili kubeba Utetezi wako dhaifu. Ni hivi hatutaki kuongozwa kidhalimu fullstop.
 
Du, povu namna hii tutafikia kweli! Iko hivi_timu Samia = timu Tanzania. Kiongozi yeyote yule anayetumikia watu katika ngazi ya juu mpaka chini ni lazima awe na sikio ndefu la kusikilizia wayatakao watu hao. Yaani hiyo huitwa serikali sikivu.

Hii ndio imetoka, chelewa wewe tu. Hii ni safari treni Dar...... Kigoma, haipotei
 
 
Mama akipatia atasifiwa, na akikosea atakoselewa.

Hivi nyie sukuma gang mliuza ng'ombe zote na kuwekeza kwenye praise team ya marehemu pombe??
Mbeligiji wenu kawaonya, suala la kumwaga sifa asubuhi na mapema.
 
Kuna wataalamu gani twiter.??
Na wewe unakuja na moto wa mabua: unajuaje kuwa amepata ushauri toka twitter, ulikuwepo huko wakati anashauriwa?

Mbona huyu mtu kakaa serikalini miaka mitano na zaidi, kwa nini usifikirie kwamba anayofanya sasa ndiyo aliyotamani yafanyike wakati akiwa chini ya boss aliyetaka yafanyike kivyake.

Usitake kumfanya huyu mama kana kwamba yeye yupo yupo tu.

Najua, baadhi ya watu humu wanapandisha mizuka kwa sababu tu huyu ni mwananmke. Hii tabia bado ipo sana , na itachukua muda watu kukubali kwamba mwanamke anauwezo wa kufanya maamuzi mazito bila ya kutegemea aambiwe cha kufanya.

Sasa naomba unielewe, sijasema kwamba mama anafanya maamuzi sahihi kabisa au mabovu kabisa. Binafsi nampa nafasi aonyeshe uwezo wake alionao kama kiongozi
 
Eeeeh uchaguzi Mkuu tena....??????
 
Kwa maoni ninayoyaona humu inaonekana kuna baadhi ya watu wachache walikuwa wanafaidika na yule " marehemu mkono wa chuma" na sasa wanapingana na mama ambaye ameamua kuleta maridhiano baada ya Nchi kuharibika. Wafaidika na yule marehemu acheni mama afanye kazi, zile zama za ubabe na vitisho zimeisha, mungu katafuta suluhisho la matatizo ya waTz akaona amchukue ili Mama awaliwaze kwa majanga yaliyowapata. Zama za ubabe, vitisho, uonevu, na kutoana roho zimeisha. Mama fanya kazi achana nao hawa washenzi wa yule bwana
 
Sina Masilahi yoyote mimi.

Mimi ni mzalendo tunahitaji kuwa na misingi imara ya uongozi.
Umekimbilia wapi? Rudi huku ujibu hoja. Uzalendo gani huo? Mchumia tumbo tu wewe! Zama zenu zimekwisha, ulitaka lia au kaji.......

UZALENDO ni kupenda watu wako si nchi tu. Hatutaki team maslahi.
 
Mzee utangojea sana hizi ni zama za kiongozi anayesikiliza wataalamu sio zama zile za stone age ambapo wataalamu waliitwa kushauriwa na sio kushauri, tunaiona +255 inayotembea na dunia kusonga mbele.
Kumbe MATAGA mmesharudishiwa akili mlishokua mmeshikiwa na jiwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…