#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

ww ndo unaakili
 
Mbona mnapenda kuchonganisha sana?
Mh. Rais kama kiongozi wa taifa ameamua kupunguza tensions zisizo na msingi....Kwani watu wawili waki react na kukawa na sintofahamu mwingine akija kuleta suluhu yenye amani kuna taabu?

Ebu tumpe Rais support jamani kuleta umoja wa kitaifa....Kuna makosa yanataendwa kwasababu ya circustances na Rais ndiye mwenye dhamana ya kuamua kwa busara above all...Ametumia busara yake huu mvutano uishe
 
Usimkweze ki hivyo, he also needs to be mature and act wisely...Leo alitumia wisdom kwenda kwenye hoja na kuachana na kile ambacho hakibaliani nacho....Kwahiyo ni namna njema na ya heshima kusema no
 
Aya ya mwisho ni muhimu sana....Mjadala uishie hapo tuendelee na maisha...Kuna mengine zaidi ya hayo ambayo ni ya msingi na muhimu kwa taifa letu...Ahsante Mh. Rais
 
Mama alifanya vizuri kwa sababu kusema tunachanja hatuchanji na wananchi kuitikia tunachanjaaaa
Askofu kaishiwa pozi na hakutaka kuweka comment badala yake kabase kwenye matatizo ya wananchi wake wa kawe

Mama kambana askofu angemuhoji pale direct ingekuwa ni udhalilishaji
Lakini ni kama tu kamtaka askofu aseme tunachanja na ajue huo ndiyo msimamo

Mama hayupo upande wa askofu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Umeona mbali aisee Jamaa ana ushawishi kanda ilee
Licha ya kandaa na kwa lile kanisa langu ambao tupo wengi wa kutosha siku hizi....tena wasio na dini mpaka wale ambao hawajajifunua dhahiri...Japo sipendi kutumia imani kufanya manipulations....
 
Mama ni mwanasiasa mzuri, hayo mengine ni ninyi wapamne mnamharibia...Mama analinda wote ambao wameamua na ambao bado kuamua na leo amesomba kura zote...Mnamshauri mama vibaya sana kwakupenda kulazimisha matamanio yenu
 
Ukiangalia picha hiyo kwa makini, ukawaangalia watu waliopo hapo na jinsi walivyokuwa wakipokea yaliyosemwa hapo, sijui mwenzangu unaionaje hali ya nchi yetu!

Itazame vizuri picha hiyo, mara mbili, ikilazimu zaidi. Isome na uielewe vizuri, kwa sababu sampuli hii hata kama itatofautiana na hizo nyingine kwingineko ndani ya Tanzania, mpishano wake hautakuwa mkubwa sana.

Ukitaka kunishawishi niamini vinginevyo, niwekee picha nyingine inayokinzana zaidi na hii hapa, halafu tutaanza kujadili.
 
Askofu David Oyedepo aungana kupinga chanjo

 
Acha uchonganishi...Walijibu majibu yote mawili...Kwahiyo bado wapo ambao wanakubali na wapo wanaokataa na Rais ame prove kisiasa yupo sawa kabisa kwakua kawakubali wote...Tuache kumwondoa Rais kwenye reli...Aendelee na kutuletea maendeleo badala ya kubakia tu kwenye chanjo as if ni Mungu
 
Rais ndo ametoka hadharani, hivyo kuuliza ni kutaka kujua hari harisi.

Baada ya hapo amefafanua kwamba, wanao chanja wachanje, wasio chanja waachwe wasichanje.

Hakuna haja ya kuumizana kwa ajili ya jambo hilo.
Mh. Rais yupo sawa kabisa, kwakua wale ambao hawajachanja wanahitaji muda kujiridhisha...Na waliochanjwa nao wana sababu zap za msingi za kuchanja...Sote tu watanzania na kila moja ana haki sawa na mwenzake....Tatizo ni wachache wetu ambao walitaka kufanya tofauti na maelekezo ya Rais
 
Uzuri ni kuwa wengi wao wakiugua wataishia kwa waganga ambao watawaambia wamelogwa au kwa wakina Gwajima ambao watawafufua hata kama watakufa.

Amandla...
Ni haki yetu kuamua kuhusu afya yetu kwamba tunaenda kwa waganga au kwa Mungu wa Gwajima its our problem, we unapata shida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…