Tuungane Kwa pamoja kuwasemea walimu, wanakufa na njaa huku

Enzi za mwalimu,, mwalimu kumiliki hata baiskeli ya swala, angeitwa bepari,, sikuhizi ukienda shule, nje ya shule utaina IST, Rav4, noah, etc zimepaki,,
Standard ya maisha ya waalimu ime imarika sana[emoji2375]
Mkuu Elungata inapendeza hata wao ifike mahali wamiliki magari sio hayo mabox na vibakuri vya michuzi eti ni gari
 
Kuna watu wa kuwatetea ila sio walimu....hawa viumbe wana roho mbaya sana.....

Serikali iondoe kwanza walimu vilaza then ndio waboreshe we mazingira hawa walimu wenye elimu za kuunga unga sijui daraja la 111 A wana roho mbaya sana.
Kumsemea mwalimu ni kutafuta matatizo bure, walimu wenyewe kwa wenyewe hampendani, mnaoneana wivu, chuki na roho mbaya imewajaa mwalimu yuko radhi amuaribie mwalimu mwenzie kazi.

Mwalimu utanisamehe sana, hivi karibuni nitaleta humu uozo na ujinga mnaofanyiana walimu, kabla ujatuomba kuwasaidia jiulize nyie mmefanya nini na mmefikia wapi?
 
Mkuu Elungata inapendeza hata wao ifike mahali wamiliki magari sio hayo mabox na vibakuri vya michuzi eti ni gari
Ni kweli at least waalimu nao waendeshe V8, 😇,hili mbona linazungumzika tu,, serikali inaweza kuwakopesha waalimu wote V8,, sio ishu kubwa hii🤷🏽‍♂️
 
Mkuu Elungata inapendeza hata wao ifike mahali wamiliki magari sio hayo mabox na vibakuri vya michuzi eti ni gari
Vanguard brand new ni shilingi ngapi? Huku tuna walimu wa kawaida kabisa wanamiliki. Si mmoja au wawili ni wengi kiasi. Hivyo unategemea Unaishi wapi. Kama Mpwayungu village kule Kwa wagogo yawezekana hayako maana hata Rami haiko
 
Vanguard brand new ni shilingi ngapi? Huku tuna walimu wa kawaida kabisa wanamiliki. Si mmoja au wawili ni wengi kiasi. Hivyo unategemea Unaishi wapi. Kama Mpwayungu village kule Kwa wagogo yawezekana hayako maana hata Rami haiko
Mkuu Bigstone kwanza u bukheri wa afya ?

Turudi kwenye mada ndugu kaka mwalimu kumiliki Vanguard au Ist au Vitz sio kuonekana ana hela au tuseme wanalipwa vizuri mpaka kufanya hivyo .

Ila ni kuwa kwa leo kuna access za mikopo kwahiyo hata hiyo Vanguard uisemayo yawezekana kakopa ndiyo kanunua .

Sasa lengo anuwai sio huo ujinga wa kumiliki gari ya mamimilioni alafu huku unaliendesha siku za kutoka mshahara tu .

Ni imani yetu kuwa maslahi ya mwalimu yakiimarishwa vizuri tegemea mwalimu awe na biashara zake kubwa na maendeleo zaidi ya kumiliki gari la mkopo .

Hivyo wito ni kuwa masilahi yaongezwe ili hata akinunua gari la gharama vipi asiwe na hofu juu ya gharama za kuliendesha hilo gari .

Ila pia niwakumbushe kumiliki gari sio utajiri ni kuwa na kitu ambacho ni mahitaji ya binadamu katika karne ya leo .

Ulimbukeni wa familia nyingi watokazo ndugu walimu walio wengi ndiyo maana ufikiri kumiliki gari ni utajiri ila ni ulimbukeni uliopindukia .

Wito ni kuwa ni lazima masilahi ya walimu yaongezwe .

Teachers wake up the time of your liberation is now.[emoji123]
 
Toeni mifano hai. Mlisema mishahara yao ni midogo sana bila takwimu! Ukweli ni kuwa mishahara yao ni mikubwa ingawa haitoshi.
Kama ni biashara walimu wanazo na Wanazifanya. Wengi tu.
Kama sehemu mnayoishi walimu hawajitumi huo ni upuuzi wao na kamwe hawawezi kuwa walimu wote nchini.
 
Rafiki Bigstone
Asante kwa kuwatetea japo mimi siwapondi nawapenda walimu sana tena sana .

Ila mishahara ya walimu ni midogo lakini pia nikujuze kuwa ikiwa uliwahi kaa na mwalimu mwenye mafanikio basi ni wa kike aliyeolewa na mtu mwenye maisha mazuri kiasi .

Ila wa kiume mwenye mafanikio sijaona bado na uzee wangu .

Japo nikuulize je unajua maana ya mafanikio rafiki kipenzi ?

Basi tafuta maana ya mafanikio alafu muaattach mwalimu lazima figure zikatae .

Nakaa vijijini sana ila hakuna mwalimu mwenye maisha mazuri hata kidogo ni funga kamba twende vitani tu .

Shida ni kuwa wengi wao pia thinking capacity ziko chini hasa walimu wa primary sasa sijui sababu wengi ni wale form four failures walioenda soma vusacertificate na diploma hivyo ni dhahiri kuwa hawana thiinking capacity nzuri na exposure ya mambo mengi .

Sasa nikuchekeshe kidogo rafiki Bigstone huu mshahara uliotoka juzi kuna mwalimu upenda kuniita baba basi uwa ni rafiki yangu nikiwa bar mimi na yeye upeana offer sana .

Sasa ameamua kununua private computer (PC) sasa kichekesho hajui kuitumia si kaja kwangu eti nimuelekeze kuitumia maana anataka aende kusoma

Nilikubali nikaingia chumbani nikacheka mpaka machozi alafu nikarudi kumpa darsa kijana wa makamo ya 28's na mimi 50's yaani ni kicheko .

Inatosha kujua kuwa hawa ndugu tusimame kuwasaidia tu bila wao kupenda au kutopenda
 
Mkuu ongea yote hujamaliza
 
Uwe unakaa kimya hujui kitu
 
Vanguard brand new ni shilingi ngapi? Huku tuna walimu wa kawaida kabisa wanamiliki. Si mmoja au wawili ni wengi kiasi. Hivyo unategemea Unaishi wapi. Kama Mpwayungu village kule Kwa wagogo yawezekana hayako maana hata Rami haiko
Prado new model au V8 mwambie anunue kumamae
 
Kama huna evidence usikatae kitu. TGTS I ni shilingi ngai? Ni almost 3m.
TGTS H ni mshahara tu mkubwa wa kumwajiri Mpwayungu na family yake yote. It's over 2m.
Lofa kweli wewe unanitajia pesa mbuzi hizo, ambazo naingiza Kwa siku
 
Waalimu wanapenda kujiliza ujinga mtupu, wana maslai duni hebu waweke scale zao za mishahara tulinganishe na wengine
 
Waalimu wanapenda kujiliza ujinga mtupu, wana maslai duni hebu waweke scale zao za mishahara tulinganishe na wengine
Hebu weka wewe wa kada zote uone Hali ilivyo!!! Nilichojifunza jamii forum Kuna utoto mwingi mno watu wengi ni mbumbumbu hawajui kitu
 
Mleta mada mwenyewe ni Mwalimu pia kama bado ulikua hujaligundua hilo.
 
Na sisis tusiokua na ajira tunaruhusiwa kuwaonea huruma walimu?
 
Mtoa mada ni mwalimu 100%. Huwezi kulalamikia kazi ya mwenzako kirahisi na kwa uchungu hivyo. Labda nikwambie tu, kazi ya ualimu ukiifanya usitarajie kuwa tajiri au kuishi maisha yanayofanana na wafanyakazi wa makampuni au mashirika ya serikali utajitia stress bure.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba walimu wana mishahara mikubwa ishu inakuja pale unapotegemea mshahara kuanzia tr 1 mpaka 30 bila ya kuingiza hela yoyote hapo katikati. Hapo ndipo panakuwa pagumu.

Ishu nyingine ni kujiingiza kwenye mikopo ya mabenki. Hii ni cancer inayowatafuna walimu. Unakuta anakopa anaenda kujenga halafu ujenzi unaishia katikati hela imeisha at the same time anapokea mshahara robo tatu. Hapo ndipo maisha yanapoanza kuwa magumu na kuanza kuishi kwa madeni mpaka unaichukia kazi.

Ushauri kwa walimu hasa walimu wa kiume ambao wao ndio wanatakiwa wawe na maisha ili waishi vizuri na familia zao, nawashauri wasikope kwa ajili ya ujenzi. Wakope kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kuongeza kipato... mambo yakikaa vizuri ndio uanze kujenga kidogo kidogo.

Walimu waache kuiga maisha ya watu wenye vipato vikubwa. Waishi kulingana na vipato vyao. Hii inapelekea mwalimu kwenda kukopa hela na kununua gari huku ukibaki na mshahara mdogo na kuanza kuishi kwa tabu. Walimu warizike na wanachopata na wasitegemee utajiri kwenye ajira ya ualimu.
 
Hii posho ya madaraka kwa walimu wakuu,ndi tatizo lingine kwa walimu, walimu wanarogana kisa madaraka, wanabambikiziana vikesi vya ajabu kisa posho ya madaraka.

Niombe serikali ya awamu ya tano hii posho ni divide and rule policy ya mkoloni wote walimu wapewe posho katikati ya mwezi hata kama ni elf 50 tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…