Tuungane Kwa pamoja kuwasemea walimu, wanakufa na njaa huku

Tuungane Kwa pamoja kuwasemea walimu, wanakufa na njaa huku

Hii posho ya madaraka kwa walimu wakuu,ndi tatizo lingine kwa walimu, walimu wanarogana kisa madaraka, wanabambikiziana vikesi vya ajabu kisa posho ya madaraka.

Niombe serikali ya awamu ya tano hii posho ni divide and rule policy ya mkoloni wote walimu wapewe posho katikati ya mwezi hata kama ni elf 50 tu
Hata Watendaji Kata siku hizi Wana POSHO ya madaraka, Tsh 100,000 kwa mwezi
 
Navipi kuhusu overtime na per diem, house na food allowances wanapewa pia walimu?
CWT hawajitambui hawapo kwa ajili ya walimu, wapiganie posho yaani Teaching Allowance

Walimu wana hali mbaya, hivi serikali kwa mtazamo wao wanafikiri elimu itaboreka kwa kuweka policy ya divide and rule?

Kwamba mwalimu mkuu apewe posho alafu wengine wengi waachwe, hapa kuna shida nakwambia
 
Sisi sote ni binadamu tuwe na utu, walimu sio mbwa ni binadamu kama sisi. Wanaishi Kwa mateso kama wapo kuzimu ninaomba wanachama wote wa jamiiforums tuandae siku maalum ya kuandaa thread juu ya matatizo na changamoto zinazowakumba walimu, haki zao wanazonyimwa na maslahi Yao. Hiyo siku ijae thread za walimu tuuuu, yani iwe ni walimu mwanzo mwisho mpaka serikali isikie kilio Chao.

Walimu nao ni watu tunaishi nao mitaani, kama ilivyo Kwa watumishi wengine Tunaomba nao pia wapewe heshima Yao nawathaminiwe pia maana hii serikali imezoea kuwapuuza sana walimu. Walimu msikubali kuchelewa daini haki zenu walahi mimi kama mpwayungu village nipo pamoja na nyinyi Kwa lolote lile [emoji120][emoji120]
Sekta ya 2 Kwa Idadi kubwa ya Chawa baada ya wasanii.
 
Kama huna evidence usikatae kitu. TGTS I ni shilingi ngai? Ni almost 3m.
TGTS H ni mshahara tu mkubwa wa kumwajiri Mpwayungu na family yake yote. It's over 2m.
Unajua inachukua miaka mingapi kufika TGTS H NA TGTS I ?

NI ZAIDI YA MIAKA 20 KAZINI.
 
Tatizo ni wajuaji , alaf ni makada , ukisema makosa ya serikali wanakutenga na wanakusinitch , waoga kinyama , huwez kutetea kundi hili unajitakia majanga tuu, wajanja huwa wanajiondokea kwenye hyo Kada , mtu unafundisha physics na chemistry, ni kijiaibisha tuu , fundisha miaka mitano chepukia Afya
Afya ndo kuna pesa mingi sana?
 
Tatizo ni wajuaji , alaf ni makada , ukisema makosa ya serikali wanakutenga na wanakusinitch , waoga kinyama , huwez kutetea kundi hili unajitakia majanga tuu, wajanja huwa wanajiondokea kwenye hyo Kada , mtu unafundisha physics na chemistry, ni kijiaibisha tuu , fundisha miaka mitano chepukia Afya
Haya maneno kama umechukua mdomoni kwangu
 
Back
Top Bottom