Tuvunje Wizara ya Ardhi na Tamisemi tuwape Wazungu

Huwezi kumkwepa mzungu kwenye kitu kinaitwa ustaarabu wa kuishi.

Ametuacha mbali sana sisi waafrika weusi!

Kama hujatoka nje ya Tanzania na kufika kwenye nchi zao hutaelewa ila kama umetoka utaelewa.
Niko MIAMI FLORIDA mkuu, wazungu wamestaarabika kufuata muda na kuwajibika tu..

Kitabia hatipishani mkuu, yako majamaa ya hovyo sana huku ...
 
Niko MIAMI FLORIDA mkuu, wazungu wamestaarabika kufuata muda na kuwajibika tu..

Kitabia hatipishani mkuu, yako majamaa ya hovyo sana huku ...
Naongelea kupanga miji yao na makazi yao. Huko Florida kuna eneo limejengwa hovyo kama tandale? Au kigogo samaki?

Kuna eneo wanapanga biashara chini kama Mbezi Mwisho au Mbagala?
 
Hii 👆 nchi ujamaa umeiharibu kabisa daa.
Yan kila kitu kimeungwanishwa na siasa
 
Hao ni wahamiaji haramu ambao most ni homeless ndo wanafanya hayo.

Huwezi kuta mmarekani kajenga banda la mbao au mabati barabarani
Usitoke nje ya Topic, awali ulidai hakuna watu wanauza nyanya barabarani US

Nimekuthibitishia wapo, sasa wawe ni wahamiaji au wazawa sio dill ishu ni kwamba wanaouzia barabarani wapo ...

Naongelea kupanga miji yao na makazi yao. Huko Florida kuna eneo limejengwa hovyo kama tandale? Au kigogo samaki?

Kuna eneo wanapanga biashara chini kama Mbezi Mwisho au Mbagala?
Mkuu Tz ni nchi inayoendelea, usifananishe na nchi iliyoendelea .

Ukifukuza machinga barabarani unawaweka katika hali ngumu wakati bado wanajitafuta ,
 
Wazungu hawana shida na kila kitu kinakwenda kosher ?

Kwa taarifa yako tupo hapa na tutaendelea kuwa pabaya zaidi kwa watu wenye fikra kama zako kwamba umpe mtu mwenye motives tofauti na zako ili akufanikishie wewe ?

Kwa taarifa yako hao so called wazungu wamefanikiwa zaidi kwa marginalization ya sisi tunaowakaribisha leo na kuwaona ni wajomba zako....

We need to become self reliant hususan kwa vitu ambavyo tuna uwezo navyo kuliko kutumia dollar.., kwa kuanza tu jiulize kwanini tunahangaika kununua gesi kutoka nje (LPG) wakati tunaweza kutumia nishati ya kupikia tunayozalisha tena kwa gharama sawa na bure ?
 

Uwe unajifunza sio una copy na kupaste tu vitu vya mtandaoni. Hiyo picha umeitoa kwenye habari inayoonesha wenzetu wanavyochukua hatua kwenye hicho unachokisema. Huku kuna nini kinafanyika? Be it regularly or otherwise?
 
Inakera sana Kuna maeneo unakuta Bado watu hawajawa wengi watu wa ardhi na Mipango miji wanashindwa kupima maeneo na kuweka plan nzuri mwisho wa siku watu wanaongezeka wanajenga hovyo Yani kero unajiuliza ivi sisi tuna akili kweli?
 
Mkuu hatusemi machinga wafukuzwe,ila hapa tunaongelea Mipango mizuri ya sehemu wazouzia Hawa wamachinga.mfano Mwanza Kuna soko linaitwa soko la wakulima kayenzi Kona hapo wakulima wengi wanapanga vyakula chini kabisa na ni soko ambalo halmashauri inakusanya ushuru sasa unajiuliza ivi inashindikana vipi kuweka mazingira mazuri hapo?soko halima umeme saa 12 tu soko limefungwa hii ni sahihi?
 
Hapo umeeleweka mkuu ..
 
Hama hii nchi tu.
 
Wizara ya ardhi ilikuwa imepata daktari wa kuitibu Slaa, lakini ameondolewa kimizengwe na kuwekwa mtu asiejua anachokifanya wizarani.

Kwahiyo wananchi ya kwetu macho tu.
 
Maskini anachojua ni kulalamika tu, kila sababu anayoweza kuhisi kuwa ni chanzo cha umaskini wake ataitumia hiyo hiyo kujenga hoja za kulalamikia. Tumepotea katikati ya bahari na hatujui tunachomoka vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…