Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Hakuna awamu ya CCM yenye uongozi wa wizara wenye kuwajali wananchi linapokuja suala la ardhi.
Mikoa yote ya Tanzania wao wanajikita katika kulipanga jiji la Dar pekee, wakati mifumo yenye kurahisisha upimaji na upangaji wa ramani inatakiwa ifanye kazi kila sehemu ya kila mkoa.
Kuwepo kwa vurugu mechi katika suala zima la miji kutokaa sawa ni fursa ya upigaji wa viongozi wa wizara. Mtaalam fulani aliyekuja na mfumo wa kisasa wa kila kitu kuwepo kwa mujibu wa ramani alifanyiwa fitina mpaka akataka kuuawa na watumishi wa hapo ardhi.
Ukafika wakati akawa hagusi maji ya hapo wizarani wala hagusi chakula chochote, mfumo wao wa wizi aliuletea suluhisho hivyo wakamchukulia ni adui namba moja.
Dodoma ungeweza kuwa ni mji uliopangika kuliko yote Tanzania, kwani ramani ya CDA ndiyo iliyokwenda kuijenga Abuja huko Nigeria.
Wameingia vijana maofisa wa wizara ya ardhi na tayari wameshauchafua huo mji, tamaa za utajiri wa haraka zimepelekwa Dodoma na kwa sasa hauna tofauti na Dar, ni mji wa hovyo tu.