Tuwaze mrejereo: Hivi DP World ingeletwa na Magufuli ingepingwa?

Mwabudu mizimu wewe
 
Ndio haikuletwa naye , sasa ni vigumu kutoa maoni , lakini alipoleta udikteta hakupingwa ?
Hakupingwa popote aliponajisi uchaguzi.
Kwa mujibu wa mleta mada inaonekana ni afadhali uchafue uchaguzi kama alivyofanya Magu hakutokuwa na kelele kuliko uuze bandari
 
Kufa kwa Magufuli hakuondoi ukweli kuwa alikuwa jitu ovu na katili sana. Lazima tuseme
 
Bali kuchezea uchaguzi kwenu ni jambo dogo sana
Sentensi hiyo inayonesha ufinyu wa akili yako katika kujadili mambo; nadhani wewe una addiction fulani inayopunguza uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja.
 
DP World wapo Durban,SA muda wamepewa ICD ila serikali imekacha kuwapa waendeshe bandari ya Durban badala yake imewapa wafilipino wa ICTSI miaka 25 ya kuanzia.

Wenzenu walitangaza tenda wazi (na kila kitu kipo wazi) wakajitokeza 18 huku 9 ni international companies,10 wakawa shortlisted na hatimaye 6 bidders waka- submit proposals na ICTSI wameula.

Nyie mmeenda Dubai Expo mmerushwa Burj khalifa tayari mkarudi na jina mfukoni.
 
Uuzwaji wa bandari kama mnavyodai, ni zao la ufisadi mkubwa alioufanya Dikteta lile. Waliopitisha jambo hili wote waliwekwa na shetani lile.
That's why tunasema kelele kubwa ilifaa ifanyike wakati shenzi lile linanajisi sanduku la kura.

Na ht sasa binafsi msimamo wangu ni kuona wapiga kelele hawa wangejikita kwenye katiba mpya kwa nguvu kama hii kuliko kuhangaika na bandari ambayo hakuna wanachoweza kubadili
 
Rule 1. Isingeletwa

Rule2. Hata kama ingeletwa isingekuwa na mashariti ya kipumbavu.

Rule3. Kama mashariti ya kijinga yangekuwepo see Rule1
 
Kwa kuwa Magufuli alifanikiwa kuiba uchaguzi wote then inampata uhalali Maza kuuza bandari zetu... Are you serious!!?
 
Ingepingwa kama kungekuwa na mkataba wa kitapeli kama huu wa Mwamvua. Ieleweke hapa haipingwi DP World unapingwa mkataba, mkataba ukiwa mzuri na wenye kulinda maslahi ya taifa hata wakija Mwamvua na nduguze investment hakuna mtu atapinga.
 
Hujanipata vizuri ndugu, ulichokiongelea ndio maoni yangu ila Mimi napinga tabia ya kumuita mkuu wa nchi "mama" yeye sio mama kwetu ni rais wetu na hivyo tumkosoe na kumpongeza kama rais wala sio mama. Hiyo tabia ya kuitana mama inaenda kutupeleka pabaya kama ulivyoona Lissu anatishwa na Nape eti kamkosoa "mama" bila staha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…