Tuwe makini na matapeli wa "ile pesa tuma kwenye hii namba". Ni kama vile wanapata taarifa tunapofanya miamala

Ni watu wa mitandao au tcra hao wanatula hela
 
Sidhani kama ni hivyo, ni kama tu io yako waliotea ikawa ni right time, sema tu ni kua wewe unafahamu hili jambo ndomana hawakukupiga. Ila kama ingekua mtu asie fahamu, hapo ndo wanapopigiwaga.

Yote kwa yote elimu iendelee kusambazwa kwa wasio jua ili hawa jamaa wafe njaa
 
Nafikiri kuna wanaopigwa kweli maana hawakomi means wanafanikiwa
 
ETI KAFANYENI KAZI NYIE WAKATI WENZAKO NDIO WAKO KAZINI TAYARI [emoji1][emoji38]
Kazini kwao kuna kazi.

Hawa jamaa kuna siku nilikua nawasiliana shem aliniomba kiasi fulan cha pesa ile tumemaliza kuwasiliana tu ikaingia sms yao, shem ile pesa tuma kwenye namba hii jina litakuja fulani fulani usitume kwenye namba yangu. Nikasita nikampigia kumuuliza akasema sio yeye.
 
Bahati yako tapeli wa zamu ni mgeni, angekua mzoefu angepiga cm kabisaa ili akuporee vyediii, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ndio halisi kabisa, unamaanisha jamaa walikuwa wanapata kila kituu. Hii mitandao kuna namna tunachezewa basi ni kuwa makini sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…