Tuwe makini na matapeli wa "ile pesa tuma kwenye hii namba". Ni kama vile wanapata taarifa tunapofanya miamala

Tuwe makini na matapeli wa "ile pesa tuma kwenye hii namba". Ni kama vile wanapata taarifa tunapofanya miamala

Kazini kwao kuna kazi.

Hawa jamaa kuna siku nilikua nawasiliana shem aliniomba kiasi fulan cha pesa ile tumemaliza kuwasiliana tu ikaingia sms yao, shem ile pesa tuma kwenye namba hii jina litakuja fulani fulani usitume kwenye namba yangu. Nikasita nikampigia kumuuliza akasema sio yeye.
Hapa ipo namna siyo bure!
 
Jana nimemaliza tu kuwasiliana na mtu kwa njia ya simu ya sauti na kunisisitiza pesa nimuwekee kwenye namba yake ya airtel. Nakata simu dakika moja mbele napokea hii text. View attachment 2942530hii inaweza kuwa ni bahati mbaya kweli au hawa matapeli wana-pata mawasiliano yetu.
Hicho ndicho cha kujiuliza. Cha ajabu zaidi anza pokea michango au pesa iwe imetumwa kwenye simu yako ndiyo utaanza ona sms za makampuni zinaanza mara sijui kopa, sijui nini haichukui muda unakutana na ujumbe ntumie pesa namba hii. Wanajuaje kama nimepokea pesa kwenye simu kama hakuna connection na makampuni au mtaalam na mwenye access na mtandao? Mbona simu ikiwa haina mpesa,tigopesa n.k jumbe hizo haziji?
 
Back
Top Bottom