Ila mimi nimemuelewa Magufuli kwenye baadhi ya mambo baada ya kufariki.
Kuna vitu nimekua exposed kwake kwa hivi karibuni kwa siku za mwisho mwisho za uhai wake, ndio nikaja kujua alikua na nia gani.
Kwenye ujenzi wa bwawa la umeme, nilikua nampinga tu Magufuli kwa kufuata mkumbo lakini baada ya kupata facts kuhusu gharama za uendeshaji wa mitambo ya gesi na mafuta kwa tanesco, nikajua kabisa Magufuli aliona mbali na alikua na nia njema kabisa kuhusu uchumi wa nchi yetu.
Sasa naamini ukiona mtu anapinga jambo flani inaweza kua halijui vizuri, ana maslahi binafsi, hajalielewa ama anafuata tu mkumbo au ameamua tu, maana watu wengine wanaweza kuamua tu kua dogma, akapewa undeniable facts na bado akaamua tu kutokuelewa.
Mfano mzuri watu dogma ni kama Magufuli mwenyewe juu ya covid 19, aliamua tu kua dogma juu ya corona na bahati mbaya udogmatic wake umegharimu maisha yake.
Ukweli ni kwamba uzalishaji wa umeme kutumia maji ni way cheaper kuliko sources nyingine zote za nishati, ni kati ya shilingi za kitanzania 60 hadi 90 kwa unit. Lakini pia maintanance ya mitambo yake ni baada ya muda mrefu sana, zaidi ya miaka 15 na hata gharama za utengenezaji wake sio kubwa.
Ukija kwenye gas, uzalishaji wa unit moja ni mara 2.5 ya uzalishaji wa maji, lakini pia mitambo ya gesi inahitaji overhaul maintenance kila baada ya miaka 2 na ni billion of money, hao ABB ya Uingereza, Siemens ya Sweden, General Electric ya Marekani, Wartisila na wengine hela wanazofyonza pale Tanesco sio za kitoto, sio za kitoto. Hawa hawataki kusikia tunakua na chanzo kingine cha umeme zaidi ya gasi ama mafuta mazito maana ulaji wao pale Tanesco utakata.