Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Pasipo katiba mpya ya wananchi na mifumo thabiti tunaweza kurudi enzi hizo muda wowote.
Mbaya zaidi, ni yeye kujifanya anajua kila kitu... aiseee watanzania itabidi tuwe makini sana huko mbeleni.... hii nchi ilikuwa ishafika point inaenda kuparanganyika.. ni kama miujiza imetendeka... halafu wale wapuuzi wanaongea mambo ya kufuta ukomo wa uraisi.. aiseeee
 
Ila mimi nimemuelewa Magufuli kwenye baadhi ya mambo baada ya kufariki.

Kuna vitu nimekua exposed kwake kwa hivi karibuni kwa siku za mwisho mwisho za uhai wake, ndio nikaja kujua alikua na nia gani.

Kwenye ujenzi wa bwawa la umeme, nilikua nampinga tu Magufuli kwa kufuata mkumbo lakini baada ya kupata facts kuhusu gharama za uendeshaji wa mitambo ya gesi na mafuta kwa tanesco, nikajua kabisa Magufuli aliona mbali na alikua na nia njema kabisa kuhusu uchumi wa nchi yetu.

Sasa naamini ukiona mtu anapinga jambo flani inaweza kua halijui vizuri, ana maslahi binafsi, hajalielewa ama anafuata tu mkumbo au ameamua tu, maana watu wengine wanaweza kuamua tu kua dogma, akapewa undeniable facts na bado akaamua tu kutokuelewa.

Mfano mzuri watu dogma ni kama Magufuli mwenyewe juu ya covid 19, aliamua tu kua dogma juu ya corona na bahati mbaya udogmatic wake umegharimu maisha yake.

Ukweli ni kwamba uzalishaji wa umeme kutumia maji ni way cheaper kuliko sources nyingine zote za nishati, ni kati ya shilingi za kitanzania 60 hadi 90 kwa unit. Lakini pia maintanance ya mitambo yake ni baada ya muda mrefu sana, zaidi ya miaka 15 na hata gharama za utengenezaji wake sio kubwa.

Ukija kwenye gas, uzalishaji wa unit moja ni mara 2.5 ya uzalishaji wa maji, lakini pia mitambo ya gesi inahitaji overhaul maintenance kila baada ya miaka 2 na ni billion of money, hao ABB ya Uingereza, Siemens ya Sweden, General Electric ya Marekani, Wartisila na wengine hela wanazofyonza pale Tanesco sio za kitoto, sio za kitoto. Hawa hawataki kusikia tunakua na chanzo kingine cha umeme zaidi ya gasi ama mafuta mazito maana ulaji wao pale Tanesco utakata.
1. U - dogma juu ya COVID -sicho ambacho kimemuua Mwendazake Magufuli..

2. Kuhusu COVID - 19, Rais John P. Magufuli was in the perfect stand. Alichukua msimamo sahihi kabisa wa Kimungu..

3. Shida au kasoro ya msimamo wa Hayati Magufuli dhidi ya COVID - 19, ni huu;

Kwamba, aliamua kuingia vitani kupigana na adui hatari (COVID - 19) bila ya yeye mwenyewe kuvaa silaha za KUMKINGA na KUSHAMBULIA.

å SILAHA ZA KUMKINGA ni: Utakatifu wake binafsi mbele za Mungu, Imani kwa Mungu sambamba na matendo ya haki, nia ya haki, dhamira ya haki, upendo, uvumilivu, utu wema nk nk...

å SILAHA ZA KUSHAMBULIA, ni; NENO LA MUNGU lilipaswa kukaa kwa wingi ndani yake. Neno la Mungu ndilo linaloitwa pia "UPANGA WA ROHO"..

4. Naona kama hamjanielewa. Ngoja niliweke hivi: COVID 19 ni shambulio toka kuzimu. Kukabiliana nalo ilikuwa ni lazima Mwendazake John Magufuli awe na UHUSIANO THABITI (MTAKATIFU) NA USIO NA SHAKA NA MUNGU YEHOVA. Haikuwa hivi kwa masikini Mwendazake..

Mtu hawezi kukabiliana na shetani (COVID - 19) huku akiwa mwili mzima unanuka dhambi. MUNGU hujitenga na wenye dhambi yoyote kwa hiyo anakuwa vulnerable na all kinds of devil's attacks...

Dhambi ni mlango wa kuruhusu mashambulizi ya shetani ibilisi. Na shetani anapoingia kwa binadamu, the furst and utter most target yake kubwa huwa ni kuiba, kuchinja na kisha kuua tu...

That's what the devil did to Mr Mwendazake..

Laiti Magufuli angekuwa anatambua "spiritual status" yake kuwa hakustahili kutumia approach hiyo kukabaliana na VOVID 19, leo angekuwa hai...!!

5. Magufuli hakufa kwa COVID - 19 bali kilichomuua ni makosa (dhambi) zake mwenyewe ikiwemo ya UNAFIKI na damu za watu mikononi mwake...

Na COVID-19 ilitumika kama risasi (bullet) tu kummaliza...
 
Yeye alimwombea beni Saanane? Risasi 16 za lisu mbona alikataza uchunguzi huru ? Azory gwanda unadhani mkewe na watoto wako kwenye trauma kiasi gani kupotea kwa baba Yao mpaka Leo siwezi kumuombea muuwaji alieuwa watu jambazi la chato Lile Mungu ka mmute milele.
Jiwe au "Mwamba" kwa jina jipya walllombatiza baada ya kifo chake ndilo lilimpa jeuri ya "KUJIMWAMBAFY" .
Wakti Jiwe akijimwambafy na kuelekeza wapinzani wapigwe marisasi na kupotezwa alifikiri hii Tanzania na dunia alikuwa amezifanya miliki yake!!!!!. Niliwahi kusema huko nyuma, kuwa kwa Watz hao waliokuwa wakiteseka, nyanyasika na kupotezewa maisha yao, GOD WAS JUST WATCHING FROM A DISTANCE. Sasa imekwisha......! It's now over!
R.I.P. Mwamba wa Chato!
 
JK alikuwa anapata wapi pesa za kujenga barabara za lami kuunganisha mikoa yote, vyuo, airport, kuajiri, kupandisha mishahara kila mwaka, sherehe, mbio za mwenge, kulipa pensheni n.k bila hata kunyang'anya wakulima wa korosho au bureau de change pesa zao?
Binafsi naona hizi ndiyo zile tunasema uchumi wa kwenye makaratasi ila kipindi cha JK tuseme tu ukweli fedha nyingi zilikuwa ni haram na hazikuwa zinaingia kwenye mzunguko ili lilipelekea mtaani hela kuzagaa kiasi ata laki ikaitwa si pesa ola sasa laki tunajua ni pesa.

Wafanyabiashara sikuzote wazo lao la kwanza kukwepa kodi, kipindi cha JK kuna meli 60 ziliwai kutia nanga pale bandarini Dar es Salaam na meli hizo zote hazikuwa recorded mahala popote na mwisho kontena zikapotea kusiko julikana, Zaman kipindi cha JK kontena kupotea huko bandarini kilikuwa kitu cha kawaida, Bandarini hapakuwa na scana ata ya kuscan vitu vinavyopita bandarini.

Nenda pale airport kipindi cha JK hakuna kikicho scsniwa ili kijulikane ni kitu gani...

Mwisho wa siku Magufuli alitamani kujenga Tanzania ya kesho, Magufuli hakuwa mwanasiasa ila alikuwa kiongozi, aliona bora aanze upya kuliko kuendelea na staili waliyotumia watangulizi wake.

Mwisho niseme tu huu wa kipindi cha Hayati ndo ulikuwa uchumi wetu halisi, huko nyuma kulikuwa na wajanja tu wenye kuchuma walivyotaka kuchuma lakini kwenye kujenga nchi hamna kitu.

Nakumbuka kipindi cha JK NGO zilopeta kweli lakini ki ukweli kabisa walikuwa hawalipi ata Tsh 150,000/= kwa mwaka wala hawapeleki ata hesabu zao za mwaka kwa msajili lakini alivyoingia Magufuli aligakikisha kila Wizara inayoona kuna sehemu inatakiwa ikusanye fedha inatakiwa kufanya hivo, hapo ukaanza utaratibu kama hupeleki hesabu zako kwa na hulipi ada shirika lako litafungwa na mengi yalifungwa maana yalikuwa hewa na hewa kweli cos ata mimi mwenyewe nishawah fanya kazi huko najua vyema na mpaka sasa mwenye NGO yake ninahakika anafanya kazi kwa unyofu mno.

Kiuweli tulichekea na tulipata mtu ambae alikuwa anatuambia ukweli, hizi habari za kulembeana na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa hakuwa nazo.View attachment 1741699
 
Wewe ukikosea maumivu utayahisi wewe, mke wako, mchepuko wako na ndugu zako wawili watatu wa karibu. Rais akikosea athari zake na maumivu yake ni kwa mamilioni ya watu na makovu yanabaki miaka mingi. Usichukulie poa tu kwamba yeye kukosea ni kama binadamu yoyote, ndio maana anapaswa kuwa makini sana na kusikiliza uchambuzi na ushauri wa watu wengi kabla hajafanya maamuzi. Baadhi ya maamuzi au kauli za Rais zinahahusu uhai au kifo wakati mwingine.

Maamuzi ya Kuingiza jeshi kwenye korosho na pia kuchukua pesa zao yameharibu kabisa chanzo cha mapato kwa watu karibu laki 4 wanaotegema korosho kuishi.
Lkn kumbuka binadamu kukosea ni kawaida yetu,mhurumie tu Mkuu
 
1. U - dogma juu ya COVID -sicho ambacho kimemuua Mwendazake Magufuli..

2. Kuhusu COVID - 19, Rais John P. Magufuli was in the perfect stand. Alichukua msimamo sahihi kabisa wa Kimungu..

3. Shida au kasoro ya msimamo wa Hayati Magufuli dhidi ya COVID - 19, ni huu;

Kwamba, aliamua kuingia vitani kupigana na adui hatari (COVID - 19) bila ya yeye mwenyewe kuvaa silaha za KUMKINGA na KUSHAMBULIA.

å SILAHA ZA KUMKINGA ni: Utakatifu wake binafsi mbele za Mungu, Imani kwa Mungu sambamba na matendo ya haki, nia ya haki, dhamira ya haki, upendo, uvumilivu, utu wema nk nk...

å SILAHA ZA KUSHAMBULIA, ni; NENO LA MUNGU lilipaswa kukaa kwa wingi ndani yake. Neno la Mungu ndilo linaloitwa pia "UPANGA WA ROHO"..

4. Naona kama hamjanielewa. Ngoja niliweke hivi: COVID 19 ni shambulio toka kuzimu. Kukabiliana nalo ilikuwa ni lazima Mwendazake John Magufuli awe na UHUSIANO THABITI (MTAKATIFU) NA USIO NA SHAKA NA MUNGU YEHOVA. Haikuwa hivi kwa masikini Mwendazake..

Mtu hawezi kukabiliana na shetani (COVID - 19) huku akiwa mwili mzima unanuka dhambi. MUNGU hujitenga na wenye dhambi yoyote kwa hiyo anakuwa vulnerable na all kinds of devil's attacks...

Dhambi ni mlango wa kuruhusu mashambulizi ya shetani ibilisi. Na shetani anapoingia kwa binadamu, the furst and utter most target yake kubwa huwa ni kuiba, kuchinja na kisha kuua tu...

That's what the devil did to Mr Mwendazake..

Laiti Magufuli angekuwa anatambua "spiritual status" yake kuwa hakustahili kutumia approach hiyo kukabaliana na VOVID 19, leo angekuwa hai...!!

5. Magufuli hakufa kwa COVID - 19 bali kilichomuua ni makosa (dhambi) zake mwenyewe ikiwemo ya UNAFIKI na damu za watu mikononi mwake...

Na COVID-19 ilitumika kama risasi (bullet) tu kummaliza...
Da! Kuna uchambuzi mwingine huku wa mambo ya rohoni.

......haya bana wacha mimi nichangie kwa kusema Amina
 
Walokole akili zenu zimejaa mavi.

Huko Italia na Vatican kwenye makao makuu ya Kanisa la Roma walikuwa wanachukua hatua zote za kujikinga na corona.

Nyie mnaosali kwenye makanisa ya maturubai na mabati kwa Mchungaji Gwajima mnaleta upuuzi.
Asante sana..

Lakini I bet kuwa hata hujasoma kisha ukaielewa hoja yangu...

Kuchukua hatua tu fulani fulani km kuvaa barakoa, sijui kuosha mikono na vidole, distancing nk nk bado haitoshi kukabiliana na shetani aitwaye COVID 19...

Shetani anakabiliwa na kushindwa kwa mtu (ukiwemo wewe) kuwa na usafi wa MOYO na NAFSI/DHAMIRA. Hii ndiyo ilikuwa logic yangu hata kwenye post yangu uliyoikwoti....

Nakushauri kabla ya kukomenti kwa matusi na lugha kali, ni vyema ukasoma "between lines" ukapata logic ya mwenzako kisha ndipo u - komenti...

Sasa kwa mfano ktk hili hata sijaelewa ni kitu kimekusalisha na kunirushia maneno makali huku deep inside ukiwa hata hujanielewa nilichokiandika...!!

Pole sana..
 
Wewe ukikosea maumivu utayahisi wewe, mke wako, mchepuko wako na ndugu zako wawili watatu wa karibu. Rais akikosea athari zake na maumivu yake ni kwa mamilioni ya watu na makovu yanabaki miaka mingi. Usichukulie poa tu kwamba yeye kukosea ni kama binadamu yoyote, ndio maana anapaswa kuwa makini sana na kusikiliza uchambuzi na ushauri wa watu wengi kabla hajafanya maamuzi. Baadhi ya maamuzi au kauli za Rais zinahahusu uhai au kifo wakati mwingine.

Maamuzi ya Kuingiza jeshi kwenye korosho na pia kuchukua pesa zao yameharibu kabisa chanzo cha mapato kwa watu karibu laki 4 wanaotegema korosho kuishi.
Well said mkuu.
Mimi kunakipindi nilikuwa nawashangaa baadhi ya watu wanasifia Hadi visivyofaa kusifiwa. Unakuta Mwendazake anasema mimi sipangiwi wala sishauriwi na yeyote afu watu wanapiga makofi
 
JK alikuwa anapata wapi pesa za kujenga barabara za lami kuunganisha mikoa yote, vyuo, airport, kuajiri, kupandisha mishahara kila mwaka, sherehe, mbio za mwenge, kulipa pensheni n.k bila hata kunyang'anya wakulima wa korosho au bureau de change pesa zao?

Swali muhimu sana na linahitaji majibu makini...

Majibu yake yatafuta unafiki wote wa Mwendazake na wafuasi wake...
 
Tunataka hela mkononi sasa, miundo mbinu ingoje kidogo
 
Wewe ukikosea maumivu utayahisi wewe, mke wako, mchepuko wako na ndugu zako wawili watatu wa karibu. Rais akikosea athari zake na maumivu yake ni kwa mamilioni ya watu na makovu yanabaki miaka mingi. Usichukulie poa tu kwamba yeye kukosea ni kama binadamu yoyote, ndio maana anapaswa kuwa makini sana na kusikiliza uchambuzi na ushauri wa watu wengi kabla hajafanya maamuzi. Baadhi ya maamuzi au kauli za Rais zinahahusu uhai au kifo wakati mwingine.

Maamuzi ya Kuingiza jeshi kwenye korosho na pia kuchukua pesa zao yameharibu kabisa chanzo cha mapato kwa watu karibu laki 4 wanaotegema korosho kuishi.
Ni Kweli Mkuu,ndio maana hata yeye mara kadhaa alisikika akiomba Watanzania tumuombee bila Shaka alikuwa anajua changamoto hizo.
 
Na bado alikuwa anasafiri kila mahali duniani kama Vasco Dagama, watu wanalipana posho za kufuru vikao vya bodi,mikutano ya wizara kwenye mahoteli ya kitalii na pesa zinapogwa kila mahali. Wanazi wa jiwe wakubali tu alikuwa mweupe kabisa kichwani kwenye swala la ku manage uchumi.
Swali muhimu sana na linahitaji majibu makini...

Majibu yake yatafuta unafiki wote wa Mwendazake na wafuasi wake...
 
Badala ya kuendelea kutegemea maombi sasa ili kutokurudi enzi za jiwe tunapaswa kurekebisha katiba yetu kupunguza mamlaka na nguvu kubwa mno zisizohojika zilizolimbikizwa kwa mtu mmoja kama Nyerere alivyotaadharisha. Vinginevyo tunaweza kurudi enzi za jiwe muda wowote na huenda jiwe namba 2 akadumu hata miaka 20.
Ni Kweli Mkuu,ndio maana hata yeye mara kadhaa alisikika akiomba Watanzania tumuombee bila Shaka alikuwa anajua changamoto hizo.
 
Hii hapa siyo kweli kwa sababu kutokuongeza kwa mishahara kulisababisha inflation Tanzania ibaki kuwa ya chini sana. Aliingia madarakani kukiwa na 5.59% na wakati anaondoka inflation ilikuwa 3.56% Kwa hiyo madai ya gharama za maisha kupanda siyo ya kweli. Tatizo lililokuwepo na mzunguko hafifu wa fedha kutokana kna kudhibiti matumizi ya pesa za serikali. Uchumi wa Tanzania umekuwa unategemea sana pesa za serikali kuliko pesa za watu binafsi; serikali ikibana matumizi ya pesa zake basi watu wanalia hawana hela. Ilikuwa hivyo enzi za Mkapa mwanzoni, na enzi za magufuli. Serikali ikishaanza kulegeza usimamaizi wa matumiz yake basi ndipo unaona pesa zinakuw nyingi mitaani na inflation inaongezeka.

View attachment 1741777
Kwa kawaida mfumuko wa bei unapokuwa mdogo unachochea ukuaji wa uchumi. Nadharia zinapendekeza asilimia 4-8 zaid ya hapo au chini ya hapo ni threat kwenye uchumi.
Serikali ndio inayosimamia sera za fedha kupitia benki kuu, serikali haina fedha zake ila ina njia zake za kupata mapato kutoka kwa watu wake na kutoka nje kwahiyo kusema serikali ikibania fedha zake unakosea. Sera za kifedha zinazosimamiwa na serikali ndizo zinaathiri mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Serikali ikikusanya sana afu hairudishi kwa Wananchi kunakuwepo na mzunguko mdogo na watu watalia hakuna ela and vice versa
 
I hope one day.....atatokea mtu mmchambue Nyerere kama anavyochambuliwa JPM. He was way too worse. ......

Ninamatumaini sana na hii serikali mpya. Ila kama wasemanyo waswahili. Usimcheke mamba kabla hujavuka mto!
 
uchambuzi umeenda shule, japo sio mtu wa uchumi ila imeweza kutoka na chochote...
 
1. U - dogma juu ya COVID -sicho ambacho kimemuua Mwendazake Magufuli..

2. Kuhusu COVID - 19, Rais John P. Magufuli was in the perfect stand. Alichukua msimamo sahihi kabisa wa Kimungu..

3. Shida au kasoro ya msimamo wa Hayati Magufuli dhidi ya COVID - 19, ni huu;

Kwamba, aliamua kuingia vitani kupigana na adui hatari (COVID - 19) bila ya yeye mwenyewe kuvaa silaha za KUMKINGA na KUSHAMBULIA.

å SILAHA ZA KUMKINGA ni: Utakatifu wake binafsi mbele za Mungu, Imani kwa Mungu sambamba na matendo ya haki, nia ya haki, dhamira ya haki, upendo, uvumilivu, utu wema nk nk...

å SILAHA ZA KUSHAMBULIA, ni; NENO LA MUNGU lilipaswa kukaa kwa wingi ndani yake. Neno la Mungu ndilo linaloitwa pia "UPANGA WA ROHO"..

4. Naona kama hamjanielewa. Ngoja niliweke hivi: COVID 19 ni shambulio toka kuzimu. Kukabiliana nalo ilikuwa ni lazima Mwendazake John Magufuli awe na UHUSIANO THABITI (MTAKATIFU) NA USIO NA SHAKA NA MUNGU YEHOVA. Haikuwa hivi kwa masikini Mwendazake..

Mtu hawezi kukabiliana na shetani (COVID - 19) huku akiwa mwili mzima unanuka dhambi. MUNGU hujitenga na wenye dhambi yoyote kwa hiyo anakuwa vulnerable na all kinds of devil's attacks...

Dhambi ni mlango wa kuruhusu mashambulizi ya shetani ibilisi. Na shetani anapoingia kwa binadamu, the furst and utter most target yake kubwa huwa ni kuiba, kuchinja na kisha kuua tu...

That's what the devil did to Mr Mwendazake..

Laiti Magufuli angekuwa anatambua "spiritual status" yake kuwa hakustahili kutumia approach hiyo kukabaliana na VOVID 19, leo angekuwa hai...!!

5. Magufuli hakufa kwa COVID - 19 bali kilichomuua ni makosa (dhambi) zake mwenyewe ikiwemo ya UNAFIKI na damu za watu mikononi mwake...

Na COVID-19 ilitumika kama risasi (bullet) tu kummaliza...
Kusema msimamo sahihi wa kimungu hapo ndio ujinga unapoanzia.

Mungu amekataza kutumia sayansi ana kutotumia akili?

Kama ni msimamo sahihi wa kimungu kwa nini tusifunge hospitali zote tumtegemee mungu kwa kila kitu? Ama mungu ana interest sana na msimamo juu ya corona ila magonjwa mengine hana interest nayo?

Magufuli covid 19 ndio iliyomuua kwa uzembe wake na kujiamini kupita kiasi kama vile yeye hawezi kua affected na magonjwa akaacha kuchukua tahadhari.

Hayo mengine uliyoyaandika hayana maana yoyote, ni hadithi tu za alinacha na za kina mwamposa na wajinga wenzake.
 
Sekta ya gesi zaidi ya kuzalisha umeme ingezalisha maelfu ya biashara za bidhaa, huduma na ajira za moja kwa moja mara nyingi zaidi ya zitakazozalishwa na huo mradi wa umeme wa maji.

Umeme ambao ungezalishwa na gesi ingekuwa pesa za uwekezaji na sio hii mikopo,kutopanda mishahara,ubabaishaji wa pensheni na kodi wanazokamuliwa wananchi hadi wanakonda.
Sijakuelewa, uneandika nini.

Unaweza kuiweka sawasawa hoja yako?
 
Cost accountants and economists bail us out of this calamity: Which is a cheaper and reliable source of electric power in the TZ environment? Please come up with quantified argument.
Vitu vingine huhitaji wahasibu wala wachumi kukusaidia, unatakiwa uwe una general understand halafu unasaidiwa vitu vichache kuelewa.

Kurudi kwenye swali lako, hili swali ulipaswa mwenyewe kua umejijibu kabla hujauliza.
 
Back
Top Bottom