Binafsi naona hizi ndiyo zile tunasema uchumi wa kwenye makaratasi ila kipindi cha JK tuseme tu ukweli fedha nyingi zilikuwa ni haram na hazikuwa zinaingia kwenye mzunguko ili lilipelekea mtaani hela kuzagaa kiasi ata laki ikaitwa si pesa ola sasa laki tunajua ni pesa.
Wafanyabiashara sikuzote wazo lao la kwanza kukwepa kodi, kipindi cha JK kuna meli 60 ziliwai kutia nanga pale bandarini Dar es Salaam na meli hizo zote hazikuwa recorded mahala popote na mwisho kontena zikapotea kusiko julikana, Zaman kipindi cha JK kontena kupotea huko bandarini kilikuwa kitu cha kawaida, Bandarini hapakuwa na scana ata ya kuscan vitu vinavyopita bandarini.
Nenda pale airport kipindi cha JK hakuna kikicho scsniwa ili kijulikane ni kitu gani...
Mwisho wa siku Magufuli alitamani kujenga Tanzania ya kesho, Magufuli hakuwa mwanasiasa ila alikuwa kiongozi, aliona bora aanze upya kuliko kuendelea na staili waliyotumia watangulizi wake.
Mwisho niseme tu huu wa kipindi cha Hayati ndo ulikuwa uchumi wetu halisi, huko nyuma kulikuwa na wajanja tu wenye kuchuma walivyotaka kuchuma lakini kwenye kujenga nchi hamna kitu.
Nakumbuka kipindi cha JK NGO zilopeta kweli lakini ki ukweli kabisa walikuwa hawalipi ata Tsh 150,000/= kwa mwaka wala hawapeleki ata hesabu zao za mwaka kwa msajili lakini alivyoingia Magufuli aligakikisha kila Wizara inayoona kuna sehemu inatakiwa ikusanye fedha inatakiwa kufanya hivo, hapo ukaanza utaratibu kama hupeleki hesabu zako kwa na hulipi ada shirika lako litafungwa na mengi yalifungwa maana yalikuwa hewa na hewa kweli cos ata mimi mwenyewe nishawah fanya kazi huko najua vyema na mpaka sasa mwenye NGO yake ninahakika anafanya kazi kwa unyofu mno.
Kiuweli tulichekea na tulipata mtu ambae alikuwa anatuambia ukweli, hizi habari za kulembeana na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa hakuwa nazo.
View attachment 1741699