Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Namuona jirani anaongea na mke wake, baada ya dk 5 mke anakuja nyumbani kaingia ndani anaomba jembe, mara naona mme wake akiongozana na kundi la wajumbe na wazee wanaingia ndani wanasema wanahisi nimemuweka mke wa jamaa kimada,, nikawaambia si kweli wakasema ngoja tusachi kama kweli, kuingia chumbani wakamkuta kalala kitandani, wanamuamsha anakoroma tu baadae ndo anaamka anajinyooshaaa hajielewi
Khaaa! Ikawaje mkuu Mana story haikuishia hapo
 
Duh! Story yako Kama yangu mkuu Mimi imezidi kidogo tuu.
Kilichozidi majirani wa pande 3 za mji wangu waling'oa alama za upimaji wakajimegegea eneo langu kabla Sijajenga uzio mwingine kachimba bonge ya karo, mwingine kajenga choo mwingine mabanda ya kuku.
Nilicho wafanya hawata sahau!
Uliwafanyaje
 
😂😂😂😂Uliwafanyajee mkuu???
Mkuu niilikuwa na tofali km elfu 4 nilitafuta mafundi nikawapa kazi sharti wajengee usiku na bila makelele.Kazi ilifanyika kuanzia SAA 5 usiku nikazungusja fensi mabanda ya kuku choo na karo ndani nikasubiri matokeo.nilijenga ijumaa usiku ilipofika j3
Jamaa wakaenda kushtaki wakapewa samansi naitwa ofisi ya kata.
Nilikaa siku 6 ya Saba ndo nikaripot .Sababu ya kuripot late ukuta ukauke
Kwenye mahojiano kwanini nimeingia maeneo yao.?
JIBU kuwa SIJAINGIA ENEO LA MTU NA JIJI NDO WANAJUA MIPAKA HALALI YA ENEO LANGU NA YAO KWANI HAO NDIO WALIOPIMA NA KUWEKA ALAMA.NAOMBA WAKATUONESHE MIPAKA HALALI!
IKAPANGWA SIKU NYINGINE.
ILIPOFIKA HATUA YA WATAALAMU KUJA KUONESHA MIPAKA WAKAPATA AIBU NA MABANDA NA VILIVYOMO VIKABAKI KWANGU! MWISHO WASIKU WAO NDO HAWAELEWANI KWANI WAMEPATA HASARA WASIYO ITARAJIA!!!
 
Mpaka nimeogopa nimezungukwa na wahaya na wanyakyusa wagombania ardhi[emoji1751][emoji1751]
Njoo huku chuga uone waarusha wanavyopenda ardhi,ukifanya mchezo utanunua na njia ya kufika hapo kwenye kiwanja alichokuuzia.

Kiboko yao ni wachaga wananunua eneo LA mwarusha wanahakikisha wanamnunua mpaka na yeye anakuwa mlinzi wao baadae.
 
Wakati nanunua kiwanja,huyujirani alikuwepo na muuzaji akaniambia njia hiihapa kwa jirani nayeye yupo hapohapo anasikia.

Ila palikuwa na shimo kwenye eneo alilo nionyesha njia.
Jirani kwa kauliyake akaniambia nifukie shimo nipate njia nikaagiza roli la kifusi nikafukia shimo.
Nikampa na pesa kama laki na sabini hivi mana alikuwa kama hatakiela anajifanya ni ujurani mwema.

Baada ya miaka kama miili akauza kiwanja eneo la mpakani kwenye njia, aliemuzia akajenga mbaka akamaliza njia, wife akanipigia cm nikiwa kazini akaniambia njia inazibwa sikuamini.

Nikaomba ruhusa fasta kufika home nakutakweli mafundi wapo kozi ya nne.

Daaah jasho likanitoka nikamuita jamaa pale kwenye ujenzi na mnunuzi akiwepo nikamuuliza vp jirani mbona unazibanjiatena.

Akasema alisahau kumuambia aliemuuzia kwamba aache njia.

Mwisho wakakubali kuniachia kama futi 5 hivi kwa masharti kwamba niwalipe mafundi kuvunja ukutauliozidi, ninunue sement na kulipa mafundi kujenga upya nikalipa pesa tena waka vunja.

Baada ya miezi kadhaa tena huyu jirani alienunua akapanda mnazi na mpapai kwenye njia.

Yani siwezi kuelezaninavyo wachukia hawa jamaa.

Nikaamua kununua kiwanja kingine nakujenga sasa nasubiri umeme tu nihamie huko mana hapa gari haiingii.
Upande mwingine kwenye mpaka kuna kinjia kidogo ambacho nirahisi kufika maeneo ya madukani na hospitali, chaajabu wao wanapita kilasiku kwenye njia niliyoacha mimi hapa kwangu najiuliza sipatijibu.
Ijapo maelezo ni ya upande mmoja, ngoja tujaji kwa kutumia maelezo yako peke yake.

Kwanini umekuwa mnyonge kwao kupitiliza?

Kuna faida gani kuwekwa viongozi wa ngazi za chini kabisa kama balozi na 'vitongoji'?

'Ardhi' wako wapi kuja kurekebisha mpaka nk nk?

Ujue bila kaubabe flani, binadamu mwenzako aweza kukutia dole machoni kwa uonevu wa kijinga jinga sana.

Pole kwa usumbufu uliosababishiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom