Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Mkuu kwa uswahilini hata vikiwa vimepimwa Bado Kuna WATU Ni watata bila sababu za msingi.Mimi kwangu kulipimwa toka 2003 mijitu inakuja fanya umbwanda 2013 miaka 10 baada ya kupimwa nami nilinunua 2012.
Ndo hivyo! Hata kuliko pimwa kuna migogoro kibao!
 
mie nililima mahindi katika eneo langu kwa lengo la kushika kiwanja,yalipofikia umri wa kukomaa nikapata vi hela flani nkaona nijenge ntakapo ishia ni hapo hapo. nikamjulisha jirani yangu awe anachuma mahindi ya kula kula anapopata shida maana walianza kuyaiba. upumbavu wake akaanza yalinda ili yakauke afanye mahindi ya ugali ile nimepata vihela nikaja yachuma ili kujenga msingi hahahahah acha ani maindi kwamba nilisha mpa hayo mahindi na alitaka yakauke ndio ayachume ndo mwanzo wa kuzinguana.
 
Nimepakana na Muhaya pamoja na vurugu zote alizonifanyia siku hizi anajifanya mwema kwangu.

Haipiti wiki lazima atagonga hodi kuja kwangu kusalimia namchora tu namuona mshamba wa maisha.
Wakati mwingine mtu mbaya anaweza kubadirika kutokana naww ulivo mpe ushirikiano tu ila akili itumike
 
mie nililima mahindi katika eneo langu kwa lengo la kushika kiwanja,yalipofikia umri wa kukomaa nikapata vi hela flani nkaona nijenge ntakapo ishia ni hapo hapo. nikamjulisha jirani yangu awe anachuma mahindi ya kula kula anapopata shida maana walianza kuyaiba. upumbavu wake akaanza yalinda ili yakauke afanye mahindi ya ugali ile nimepata vihela nikaja yachuma ili kujenga msingi hahahahah acha ani maindi kwamba nilisha mpa hayo mahindi na alitaka yakauke ndio ayachume ndo mwanzo wa kuzinguana.
Duh
 
nililewa kwakua milango yetu inafata nkajkuta nmelala seblen kwake et akamaind mpaka leo atusemeshan nangoja mkesha wa pasaka nilewe nkanye mlangon kwake

Ungelala kwangu nakuapia leo ama haunitazami usoni ama nimefungwa maisha!! Ulevi gani huo??
 
M
Mkuu samahani nilikuwa bize na Jambo Fulani ninakupa makadirio ya tofali cement na mchanga.
Maximum uwe na tofali 3870.
Cement mifuko 40
Mchanga Lori kubwa 2
Kama gari haifiki site kwake! Mikokoteni mingapi
 
dah dunia ina visa sana....ila kikubwa uwa sichunguzi mambo ya watu...na ni desturi yangu pia kuchukia sana pindi ninapogundua kuwa kuna mtu kwa namna moja ama nyingine ananifuatilia...hivyo ugomvi wangu mkubwa sana na majiraani zangu huwa mara nyingi ni hiyo hali ya kuchunguzana ambayo huwa inaniuzi sana
 
Hahahah
 
Wakati wa ujenz wa msingi , 2018 , niliomba jiran wa upande wa juu niweke Kibanda cha mabati ili mafund wahifadhie vifaa (stoo) kwa muda. Mita 2 hiv kutoka kwemye mpaka.

Ujenz ulikamilika vitu nikavifungia ndan kusubiria awamu ya pili. Jiran nae anaka hapo hapo.

Nikapigiwa simu na Spy niliyomuweka bila jiran kujua kuwa wamefungua banda na kutoa mirunda na Mbao na kumkodishia mtu mwingine.

Nampigia simu jiran hapokei, nikapata nafas baada ya siku 2 nikaenda, kuongea nae anasema kibanda nimejenga upande wake hivyo hana sababu ya kuniomba kuazimisha mbao.

Sikuongea sana, maana nilipatwa na hasira za ajabu,

Nikatoka nikamuita yule spy anipe details zaid za yulr jiran, kijana mdogo tu makamu yangu, na anapokaa ni kwa baba yake.

Basi nikapata wazo la kumkomesha na kununua upande wote wa lile banda.

Nikamtafuta yule Mbaba mwenye eneo na tukakubaliana na akaniuzia 1 Million.

Alaf baada ya maandikisho na makubaliano.

Nikamfuata yule kijana nkamwambia hata na ww ntakununua muda si mwing [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mpaka leo heshima ipo, ananiita bro
 
Kuna watu hawapendi ujirani wa amani kabisa. Na kundi hili la majirani wagomvi ni kubwa sana kuliko tudhaniavyo!

Binafsi ugomvi mkubwa na jirani yangu ilikuwa ni kwenye kununua Umeme. Huyo umeme ukiisha tu alikuwa hawashi taa na hapandishi mapazia anajifungia kimya!

Tulikalishwa vikao hadi vya mjumbe lakini wapi! Ikabidi nihamie nyumba nyingine! Huku nako nilikutana na mama mmoja jirani mchafu hatari, watoto wake walikuwa wanajisaidia kwenye corridor! Halafu hajali wala nini, ukiweka kanyagio la kufutia miguu ukitoka baadae unarudi unakuta wamelichukua wao kufutia miguu!

Nikadhani mtu aliyejenga hana kero ya ugomvi na majirani kumbe huku ndiko kuna balaa zaidi! Huku nako kuna watata vilevile, usipoangalia unaweza pata presha. Wapo majirani mabingwa wa kusogeza mipaka ya viwanja! Huu ugomvi ni mwingi sana umeharibu mahusiano ya majirani wengi sana!

Wapo pia majirani wanaojenga hadi kiwanja wanamaliza halafu paa la nyumba linamwaga maji kwa jirani ilimradi tu wawakere!

Yote tisa, wapo majirani wafugaji wenye mifugo inayoharibu mali za jirani yake na wala hawajali.

Nisiseme mengi. Leo Naomba tushirikishane, ni mgogoro gani hasa ulionao wewe na jirani yako hapo?
Hakuna haja ya kugombana na majirani cheif, kama kuna jambo halijakaa sawa mnaitana mnazungumza na kuyamaliza na sio kugombana, majirani ni kama ndugu kwa sababu ni watu wa karibu tunaoshirikiana nao katika kila jambo na hata unapopatwa na jambo usiku wa manane mtu wa karibu yako ni jirani
 
Mfano kama jirani kazidisha mipaka nahataki maelewano utafsnyaje
 
Mfano kama jirani kazidisha mipaka nahataki maelewano utafsnyaje
Ni bizuri kuguata taratibu za kisheria, kuna wajumbe wa serikali za mitaa, ambao ndio ngazi ya mwanzo wanaweza kuzungumza nae kama hataelewa then utaendelea na utaratibu unaofuata
 
Back
Top Bottom