Hiyo mikopo alikukopa wewe?
KWA TAKWIMU HIZI ZA DENI LA TAIFA HAKIKA TUNAANGAMIA.
01. Awamu ya kwanza chini ya Mwl. Nyerere alieongoza kwa miaka zaidi ya miaka 20.
-Deni la Taifa lilipotoka mwaka 1979 mara tu baada ya vita ya Kagera lilikuwa Trilioni 3.
02. Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza kwa miaka 10.
-Deni la Taifa lilipanda kutoka Trilioni 3 hadi kufikia Trilioni 18. Hii inamaana kuwa, Mzee Mwinyi alikopa fedha kiasi cha Trilioni 15 pekee ndani ya awamu zote mbili.
03. Awamu ya tatu ya Mhe. Benjamin Mkapa aliyeongoza kwa miaka 10.
-Mzee Mkapa alipoingia alikuta deni ni Trilioni 18. Mzee Mkapa akafanya jitihada za kupunguza deni hilo na kufanikiwa kulipunguza hadi kufikia Trilioni 10.
Mpaka anaondoka madarakani uchumi ulikuwa unakuwa kwa 6.7%
Kwa neno moja tu tunaweza kusema, Mzee Mkapa alikuwa ni "Mpiganaji wa uchumi".
04. Awamu ya nne chini Mhe. Jakaya Kikwete alieongoza miaka 10.
-Ameingi amekuta deni la Taifa ni Trillion 10. Lakini katika kukopa kwake mpaka anamaliza muda wake wa uongozi (awamu zote mbili) ameacha deni la Trilioni 35. Maana yake kwa miaka yote 10 amekopa kiasi cha Trilioni 25.
05. Awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ambae mpaka sasa ana miaka minne (4) ya uongozi wake ikiwa hajakamilisha hata awamu moja ya miaka mitano.
-Ameingia madarakani amekuta deni la Taifa lililoachwa ni Mzee Kikwete ni Trilioni 35.
-Mpaka kufikia mwezi huu wa January mwaka 2019, deni la Taifa limefika Trilioni 61.8
Kwa lugha rahisi ni kwamba Rais Magufuli amekopa Trilioni 26 ndani ya miaka minne (4) tu.
Hivyo basi, ni dhahiri kusema kuwa, Rais Magufuli ndiye Rais pekee kati ya marais wote waliopita, aliyekopa pesa nyingi sana kwa muda mfupi sana.
Tuna wakati mgumu sana kama Taifa. Na hapa tulipofika ni hatari zaidi katika nchi hii ambayo watu wake wengi ni Wakulima na Wafanyakazi.
Ninajiuliza ikiwa kiasi hicho ni cha miaka minne tu, je, Rais huyu akipewa awamu ya pili tutaangukia wapi?