Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Nimetuma 100,000 kwenda tigo pesa kwa simbanking, VAT sh. 974.70, govt levy sh. 1,009.00, TMS CHARGE TIGO 5,415.00, wenye akili timamu nimekatwa sh 7,398.7 kwa transaction hii moja tu. Pesa ilitoka kwa mshahara ambao wajuba walishakata PAYE. ni 7.4%. Mwaka 2017 kwa muamala kama huu nilikuwa naktwa sh. 2,360 maana yake sh. 5,038 imeongezwa kwa kipindi cha miaka mitano. Hali ya uchumi na inflation ni kubwa sasa kuliko ilivyokuwa 2017.

Jinsi mambo yanavyokuwa magumu tigo nimetoa sh 5,000 makato ni sh. 1,010 ambayo ni 20.2% hii ni zaidi ya 18% VAT. Tujuzane hapa mambo haya ya kukatana pesa tulizotolea jasho yataisha lini? Kwanini mnatukata kwa kiasi hiki kwa value ipi mnayotuongezea? Wale ambao mnalipwa kwa kushadadia na kujibu humu hata hili na nyie linawagusa pia, twendeni kwa namba kwanza.

Maisha sasa ni ghali mno na watunga sera lazima wawe flexible, kama mashirika ya kimataifa yanaona hali ngumu na kutoa nafuu kwa nini hawa viongozi wetu wanaweka pamba masikioni na kulazimisha kuendelea na mipango yao tu?! Maana hata midege tumelazimishwa kuyanunua bila kuona hali halisi na midude inaleta hasara. Reli toka waanze kujenga hawamalizi tu(Dar, Moro tu) politiks kila kukicha na wanatutwisha gharama bila sababu matokeo yake hata makampuni ya simu na yao yanatupiga pia.
Nimesoma malalamiko yako nimeona ni ya msingi nadhani Serikali yetu ni sikivu watafanya kitu au wanafanya kitu kuokoa hali lakini ulipofika kwenye midege na SGR hapo nahisi umepotoka..hizo ni njia za kujenga uchumi ambao ni stable na za milele...kazi ni usimamizi tu ili ziendelee kuleta tija
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, Magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Unatakwimu na kithibitisha maelezo yako au ulikaa chumbani na mmeo mkaona mseme utumbo huu...umeshawah sikia Raiswetu SSH alitamka haya..! Au Waziri Mkuu au Makamu wa Rais..viongozi ambao walikuwa walishauriana kwa pamoja na JPM kila uchao... Sasa nakuonya ukome usije mgombanisha Rais wetu na wananchi kwa utumbo wako..mama Alisha tuambia yeye na JPM Lao lilikuwa moja...na nchi ilikuwa inapaa..na inaendelea kupaa..uchumi wa Kati ungefikiwa vipi kama viongozi Hawa hawakufanya vitu sahihi..au unadhan uchumi wa Kati wazungu waliandika tu from nowhere..uwe na adabu .tuendelee kuunga mkono CCM na awamu hii inayoendeleza mazuri yote yaliyoanzishwa huko nyuma..CCM chama kubwa mama
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, Magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Akili za kidangaji hizi... nchi inaharibiwa na kufilisiwa tunaona....unaleta habari za kudanga?
 
Makali gani ya Covid wakati hata ugonjwa haukuwa tishio sana nchini. Zaidi ya kuwafyeka Elites na wazee kadhaa wa kadhaa.

Maumivu ya Covid wala hayakuhitaji loans sababu hata lockdown hatukuwa nayo. Kwa aibu kubwa hizo hela zimesingiziwa ni za Covid ila zilivyotua wameelekezea kwenye madarasa na zahanati. Ila ukiskia ya tozo zinafanya kazi hio hio.
Hizi pesa za COVID ziko wapi, zimetumiwa wapi,, au wamegawana?

Sisi wananchi tulipie vitu tusivyovijua kumpeleka mtoto wa Mwigulu International School of Tanganyika.
 
Akili za kidangaji hizi... nchi inaharibiwa na kufilisiwa tunaona....unaleta habari za kudanga?
We tahira fukara mmoja akufilisi Nani pimbi wewe?!

Wenzio wanakamatia fursa we umebakia kusubiria Samia akuletee ugali nyumbani
 
Nimesoma malalamiko yako nimeona ni ya msingi nadhani Serikali yetu ni sikivu watafanya kitu au wanafanya kitu kuokoa hali lakini ulipofika kwenye midege na SGR hapo nahisi umepotoka..hizo ni njia za kujenga uchumi ambao ni stable na za milele...kazi ni usimamizi tu ili ziendelee kuleta tija
Point ni uwekezaji mzuri nakubali lakini kwa midege wakati haukuwa sahihi na reli imechukua muda mrefu mno ilipaswa kuwa imeshaanza kuingiza pesa. Haya madude yasipoingiza pesa gharama tunatwisha sie wananzengo.
 
Hizi pesa za COVID ziko wapi, zimetumiwa wapi,, au wamegawana?

Sisi wananchi tulipie vitu tusivyovijua kumpeleka mtoto wa Mwigulu International School of Tanganyika.
Hawawezi kuwa na majibu yani majitu ya CCM yanakera sana kwa ulafi. Mtu mwenye roho ngumu anaweza kuwafyeka wote kimya kimya.
 
Asubuhi hii nimetuma 55000/= kwa mama kupitia simbanking, nimekatwa 5500/=...

Kwa lugha rahisi ni kwamba makato au gharama za kutuma hiyo pesa ni 10% ya nilichomtumia mama.

Nikiendelea kutumia hii simbanking basi CRDB mje mnivishe kibao cha "ZUZU" nimekaa palee Kariakoo Gerezani.

View attachment 2338471
Mungu tuhurumie wanao kama ulivyotenda mwezi march 2021 basi tenda haraka maana Mwigulu ataangamiza waaja wako.
Tenda Baba Tenda
 
Hiyo mikopo ya Magufuli aliyochukuwa imerekodiwa wapi? Wapi records? Mpaka Magufuli anafariki deni la Tanzania lilikuwa dogo karibia kuliko wakati wowote ule, sasa hiyo Mikopo gani unayoiongelea aliyochukuwa Maguguli? Deni la Tanzania limeongezeka kwa kiasi kikubwa sana kuanzia raisi wa sasa alivyoingia!
Deni dogo bei gani poyoyo.
Mkopo wa sgr, na bwawa la nyerere ulikopa wewe
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, Magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Hizi akili nyingine sijui zinatoka wapi! Kwani ye ndiye alienza kulipa? Ina maana Magufuli hakukuta madeni yalikopwa na watangulizi wake? Mbona miradi iliendelea kama kawaida kipindi cha Magu na hakukuwa na tozo? Hivi unaanzisha tozo kwa wananchi huku ukiongeza posho za safari kwa wafanyakazi per Diem mtu anakula 250,000 toka 150,00 alafu unasema alikuta hazina kutupu! Serious!
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, Magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Alikuta nchi ikiwa na sh ngapi?,Sasa hivi IPO sh ngapi talk by figures ,unasema nchi haikuwa na hela huduma zilikuwa zinatolewaje?watu kama nyie ni kupiga risasi mnatetea ujinga.
 
Alikuta nchi ikiwa na sh ngapi?,Sasa hivi IPO sh ngapi talk by figures ,unasema nchi haikuwa na hela huduma zilikuwa zinatolewaje?watu kama nyie ni kupiga risasi mnatetea ujinga.
Nikikupa silaha utaweza kunipiga hiyo risasi? Ngosha alivuruga uchumi wa Nchi, lawama mnamuangushia Samia mlivyo wajinga
 
Unamchukia sababu ya dini yake, ana akitoka Samia anaingia January au Ridhiwan Kikwete, wa imani yenu Ni makatili hawafai kupewa nchi
Wa imani yenu ni walegevu. Rahisi sababu ya uwezo mdogo. Na zaidi ni mafisadi na wezi wa mali za umma. Na wakiongoza nchi inajaa uzembe na ulegevu
 
Yeye si ndiye alikuwa makamu wa Magu,Mama amefuja pesa kwa kununua maushungi na madera mengi.
Pamoja na safari zisizo na umaana ambazo jata ivyo gharama zake haiziendani na upatikanaji wa fedha wa kawaida, ndimaana kila leo zinaanzishwa tozo.
 
Unamchukia sababu ya dini yake, ana akitoka Samia anaingia January au Ridhiwan Kikwete, wa imani yenu Ni makatili hawafai kupewa nchi
Nyinyi mafukara ni laana kwenye nchi yoyote ile, watu wanaotafuta pesa kikwelikweli hawawezi kuwa mazuzu kwenye huu mjadala unaohusu makato ya kishenzi kwenye hela zao wanazotafuta. Ila wewe ulichokiona ni dini tu?

Huyo unaetaka kumsifia kwa misingi ya kidini mbona nae failure tu, weka hapa CV yake tuone kama ni ya kueleweka.
 
Back
Top Bottom