Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ukumbi wa the Dom Masaki Leo

Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ukumbi wa the Dom Masaki Leo

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
9,616
Reaction score
22,521
Leo ndio usiku ambao wanamichezo mbalimbali Tanzania watapewa tuzo katika shughuli inayoendelea Sasa hapa ukumbi wa the Dom Masaki.

Mgeni rasmi ni Kasim Majaliwa na MC ni msemaji wa Azam
NB

Nje ni gari tupu
=============

Ahmed Arajiga: Ameshinda tuzo ya Mwamuzi bora wa kiume

Esther Chabruma: Ameshinda tuzo ya Kocha bora mwaka kwa upande wa Wanawake

Yanga SC: Imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kwa upande wa Wanaume

JKT Queens: Imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kwa upande wa Wanawake

Anthony Mwingereza: Ameshinda tuzo ya Kocha bora wa kiume

Taifa Stars: Imeshinda tuzo ya timu bora ya kiume kwa ngazi ya Taifa

Timu ya Taifa ya Cricket: Imeshinda tuzo ya timu bora ya Wanawake kwa ngazi ya Taifa

Grace Joseph: Ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa Kike

Yusuf Lucas Changarawe: Ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa Kiume

====================

Usiku wa jana kulifanyika hafla ya utoaji Tuzo za Wanamichezo bora mwaka 2023 katika ukumbi
wa The Super Dome
Ifuatayo ni orodha ya waliobeba tuzo za wanamichezo Bora mwaka 2024
1. Timu bora ya mwaka upande wa vilabu (wanaume) ni Yanga SC
2. Mwamuzi bora wa mwaka 2023 (wanaume) ni Ahmed Arajiga
3. Tuzo ya heshima kwa nahodha wa zamani wa Taifa Stars ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
4. Vosta Isaya Lengonela wakati akipokea tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka kwa wenye ulemavu.
5. Mwamuzi bora wa kike wa ngumi mwaka 2023 ni Pendo Njau
6. Taifa stars timu bora ya mwaka 2023 upande wa timu za taifa (wanaume).
7. Mwanamichezo bora wa kike mwaka 2023 ni bondia bondia Grace Mwakamele
8. Mwanamichezo bora wa kiume mwaka 2023 ni bondia Yusuph Changalawe
9. Tuzo ya Timu Bora ya klabu kwa upande wa wanawake, imekwenda kwa JKT Queens.
10. Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa kiume mwenye ulemavu imekwenda kwa Vosta Isaya Lengonela.
11. Tuzo ya mwanamichezo bora wa kike na wa kiume kutoka shuleni zimekwenda kwa Happyness Kongoka na Agape Mwenda
12. Tuzo ya Mwanahabari Bora za Michezo wa kike imekwenda kwa mtangazaji wa #AzamTV Fatma Abdallah Chikawe
 
Gerson Msigwa katibu wa wizara anahutubia mda huu huku akijaribu kuhamasisha watu wanaoonekana wamepoaaaa!
 
Tuzo hizi ni mara ya pili kutolewa na zitaendelea kutolewa Kila mwaka
 
Huyu Msigwa namuona anarudi pale ikulu kuchukua nafasi ya mboga saba yunusi
 
Hashim Ibwe anaendelea nadhani upande wa soka Fei anaweza akachukua kwa wanaume
 
CHalamila kaongea kwa kifupi sana hii ni nzuri sio hotuba hadi unaboa
 
Tenga ambae ni mwenyekiti wa Baraza la Michezo amepanda kuongea
Alifanya vizuri akiwa tff nadhani ameendelea kufanya vizuri BMT ambapo michezo mbali mbali imeanza kuinuka
 
Damas Ndumbaro anaelezea mafanikio makubwa ya michezo chini ya uongozi wa Samia Suluhu
Serengeti girls kucheza kombe la dunia na kufika robo final
Tembo warriors pia nao walishiriki kombe la dunia mpira wa miguu
 
Huyu Neema msita ni pisi Kali sana halafu very natural na inapiga kazi hatari pale BMT kifupi ndie katibu wa Baraza
Nadhani ifike wakati apewe wizara kabisa
 
Kasimu Majaliwa kumbe ana cv iliyoshiba sana kwenye uwanda wa michezo huyu anapenda sana michezo
Kama anaweza anaweza kupewa Simba na akaifikisha mbali sana
 
Kqsim Majaliwa PM amepewa tuzo maalumu ya mchango wake katika soka
 
Tuzo ya pili ya heshima katika mchango wa michezo imeenda kwa msomi wa kwanza mwenye degree
Leodigar Chila Tenga
Ndumbaro kataja sifa zake kedekede inawezekana kabisa Majaliwa na Tenga wakawa ni agent of change kwenye soka kwa kipindi Cha miaka 20
 
Back
Top Bottom