Tuzo za Muziki Tanzania 2021, Bado tuna safari ndefu sana

Tuzo za Muziki Tanzania 2021, Bado tuna safari ndefu sana

Aisee hizi tuzo hawakuzifanyia promo ya kutosha ndio naamka nakuta kumbe kulikuwa na tuzo😆
 
wasanii wengi wana uchumi mdogo sana hii imewafanya kuishi maisha ya kinafiki na kujipendekeza, kwa akili ya kawaida tu kuna vitu vingi tu walitakiwa kuvikataa/gomea kuhusu hizo tuzo.

Nawapongeza wasanii waliozigoea hizi tuzo, waliozikataa na wale waliojaribu walau kutoa constructive criticisms waziwazi, ujue kuna muda mtu unafigt battle lako gumu halafu mtu mwingine anataka kukuhusisha kwenye ujinga ujinga wake.
 
Wanaogopa kutengwa na WCB, wanajua ndiyo inayoongoza kwa fan base kubwa na wasanii wao wote ni A-list hivyo wakiwepo wataziheshimisha zaidi tu na excitement itakuwa ni kubwa zaidi.
Raha za tuzo ni majina kusababisha suspense, imagine hizo nominations zingekuwa na majina ya wasanii wa WCB yaani the whole shit would have been a completely different game.
Kujaribu kufanikisha hilo ndiyo wanamvuta karibu kisanii kwa ajili next year.

Nadhani issue kupoa ni mpangilio mzima wa event haswa peformance, celebrities walikuwa wachache hasa powerful names kama wema ambao wangewatumia kugawa Tuzo ingekuwa na vibe zaidi

Kuhusu WCB sidhani kama wangeleta kitu kikubwa sanaaaaaa, nakumbuka last year kulikuwa na miss East Africa na wenyewe ndio walikaa mbele na major peformer alikuwa mbosso lakini issue mzima ilibuma.

Kikubwa nadhani labda wangeongeza msisimko Tu hasa kama Zuchu angeingia maana this year kafanya vizuri sana, labda na Diamond na Mbosso. The rest sidhani kama wangeleta impact kubwa sana kuzidi uwepo wa Ali kiba, Marioo, Konde na Mbosso
 
Naona wanatoa Tuzo ya video vixen lakini kwenye kutaja nominees hakuna hata picha zinazooneshwa

Hivi hizo tuzo wanapewa na pesa au ????
Faida yake nin hizo tuzo
 
Hizi tuzo zilipoteza mvuto kuanzia siku ya kwanza walipo muweka Darmian Soul kama up coming artist yeye mwenyewe alishangaa kujiona kwenye hicho kipengele
 
Kiukweli nilikuwa hata sijui kama ni leo ila
Katika pitapita za kubadilisha TV channels ndio nakutana nazo

Ukiachilia promo ambayo imeonekana kuwa na udhaifu, bado kuna mambo mengi ya kuboresha

1. Utoaji wa Tuzo
Nimeona kuna tuzo 3 za heshima ikiwemo ya Ruge Mutahaba na Diamond platnums bado na Mama Samia Suluhu. Si kama hawastahili ila sioni umuhimu wa watu watatu kugawana spotlight

2. Too much politics
Sijaelewa ni Mimi Tu au vipi, yaani Tuzo zimekuwa kama platform ya kupromote siasa kuliko muziki wenyewe, nimeona hadi mabango ya kudai haki na background sound za kusifu uongozi.. Sio mbaya lakini haikuwa necessary

3. Management
Hapa waandaaji waangalie hata kili music awards zilivyokuwa zinaendeshwa maana nimeshangaa watu almost wanne wamepewa Tuzo ila kuna watu wamekaa stejini muda wote kama wanakamati, sijui ni public figures ama ushers

3. TBC Coverage
Mixing ya picha na presentation kiasi haijanivutia, hopeful next time watafanya vizuri zaidi


Nimeangalia high table au sijui ni VIP kumejaa political figures, sio mbaya ila wangemix na musical figures maana ni usiku wao

Nimependa stage settings wamejitajidi lakini pia wasanii naona wamejitahidi

Japo ndio imeanza, ngoja niangalie itaendeleaje
Pole sana kwa kukutana na huo upuuzi, leo kuna Grammy awards kama ni mfatiliaji basi itakusahaulisha huo upuuzi wa jana.
 
Pole sana kwa kukutana na huo upuuzi, leo kuna Grammy awards kama ni mfatiliaji basi itakusahaulisha huo upuuzi wa jana.
Ngoja nitajitahidi kuiangalia japo Mimi huwa fan wa black excellence, BET
 
Hivi hizo tuzo wanapewa na pesa au ????
Faida yake nin hizo tuzo
Tuzo ni heshima, ukiangalia hata profile ya msanii ili ujue alikuwa mkubwa kiasi gani wanaangalia mauzo ya album na Tuzo. Pia Kuna pesa huwa inatolewa kwa kila category
 
Tuzo ni heshima, ukiangalia hata profile ya maanie ili ujue alikuwa mubaarak kiasi gani wanaangalia mauzo ya album na Tuzo. Pia Kuna pesa huwa inatolewa kwa kila category
Sawa
 
Kumbe tuzo mmepeana jana, si mngesema tu hata tufatilie!
 
Chenja za mabio ya jeshi ni nouma zina vibe, tuzo kwa mabeyo😂😂
#mycountrypeople
 
wasanii wengi wana uchumi mdogo sana hii imewafanya kuishi maisha ya kinafiki na kujipendekeza, kwa akili ya kawaida tu kuna vitu vingi tu walitakiwa kuvikataa/gomea kuhusu hizo tuzo.

Nawapongeza wasanii waliozigoea hizi tuzo, waliozikataa na wale waliojaribu walau kutoa constructive criticisms waziwazi, ujue kuna muda mtu unafigt battle lako gumu halafu mtu mwingine anataka kukuhusisha kwenye ujinga ujinga wake.
Mara chache Sana naona unatoaga comment lakini ukihakutoa zinakuwa heavy kweli kweli hongera kwenye Hili tunatamani tuone ukitoa comment nyingi
 
Back
Top Bottom