TV ya Azam Sasa rasmi kutangaza pombe hadharani

Waarabu wanatupa attention sana mwisho wa mwaka huu 🤒
 
Japo maisha siyo kutesa kila siku, ila pesa ndiyo kila kitu...
 
Acha kuchanganya habari ya vitabuni na vilivyoletwa kwenye majahazi na hali halisi ya kibiashara, Acha kabisa.
 
Kwani wametangaza Kilevi au Ulevi?
 
Hiyo m-bet (simba) parimatch (Geita, nk), sportpesa (namungo, singida)

Bank NBC kwa ligi kuu (Bank ambazo zina toza riba)

Hivyo sio ajabu kuona kuna vitu kama hivi vya Pombe

Pia dini ukiimeza kama ilivyo utakuta kuwa mpira ni haramu
Umemaliza kila kitu
 
Ni vigumu sana kufanya biashara ukaepuka mambo hayo. Kwa mfano ndege za Qatar, Etihad, Emirates, Fly Dubai zote zina save pombe on board, hata ukifika kwenye hizo Airport zao pombe zinauzwa kama kawa. Wanaenda kulingana na wateja wao. Kumbuka wanafanya biashara.
 
Vipi kuhusu SportPesa na M-beti
 
Simba na yanga wanapokuwa na wadhamini wachezesha kamari kama mbet au wakishiriki ligi yenye wadhamini kama tbl inakuwaje? Huwa unashabikia hizo timu?
 
Anaetangaza apo ni simba na sio Azam mbtet sports pesa zipo lakini sio Azam anaezitangaza
 
Yupo huyo anayetuharibia kizazi Zuchi kuna kipindi alikataa shavu la kutangaza bia akasema yeye mtoto wa imani kali hafanyi ujinga huo mara ikatoka video anakata viuno nusu uchi hadharani.

Ni aina tu ya unafiki hizi kauli huwa wanazitoa wakiwa so excited kujikuta bora sana but ikija issue ya hela mezani hukunja mpunga na kuacha poyoyo zilizowaamini zikilaani huku mifukoni hawana kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…