Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Ukiwa unalipwa kwa lisaa lazima upige kazi sana na ndio wanachofanya hao wenzetu.

Ni sawa na ufungue bar alafu wahudumu uwalipe kwa idadi ya vinywaji walivyouza. Hapo utagundua kila mtu ni afisa masoko

Bongo huku hatulipani kwa masaa bali mwezi na hapo ndio mchawi alipolala.
 
Jaribu kutudadavulia kwanini unaona wana moyo wa kuchapa kazi ni kitu kinawamotivate?
Je uzalendo halisi au maslahi yako vizuri?
Hakuna uzalendo wala maslahi..japo maslahi yanaweza motivate kidogo..wengi Ni motivation za ndoto zao na kutaka kucontribute to humanity
 
Mkuu kazi zipo nyingi Sana..sema ndoo hivyo..mentality zetu tayari zilijengwa kuajiliwa. Mfano hata kama umesoma Kiswahili..eg We need a lot Swahili novels, translators vitabu and any resources for Swahili speakers etc. Ni mfano,kuna mambo mengi
Issue sio kazi ni kazi zenye ujira.., Na sio ujira tu bali ujira wa kutosha..., ili watu wanunue hizo novel zako ulizotranslate (ingawa wabongo sio wasomaji) wanahitaji disposable income ya kununua kazi yako....

Kwahio hakuna infrastructure ambayo ni sustainable na hili tatizo sio la Africa tu tunapoelekea nguvu kazi haihitajiki kama zamani na dunia ambayo inaendeshwa na consumerism iwapo people can not purchase Uchumi wote will run to a standstill..., (And how can they purchase kama they are not being paid enough) ? In short the whole system needs refurbishment ili kuweza kuendana na dunia ya teknolojia na automation....

Kipindi cha hardworkers kilipitwa na wakati baada ya skills jobs kushika hatamu tunapoelekea hata skills zitakuwa sio issue kivile due to automation na machinery... Sasa hivi mtu mmoja / machines zinaweza kulisha taifa zima wakati zamani watu ishirini au mia wasingeweza kupata hata gunia 10....
 
Ni aibu kaka..huku speed ya hawa watu inatisha..unakuta kitoto miaka 16 kishafanya kaz shamban.supermaket etc..yaan
Shida siyo kufanya kazi. Shida ni teknolojia, elimu na mishahara minono.
Unafanya kazi masaa 9 au 14 halafu unapewa 10k. Hapo hapo kwenye hiyo hela unatakiwa unywe chai 1000, chakula cha mchana 1500 na usiku 1500 hapo bado haujanunua vocha. Kwenye hiyo 10k utabakiwa na shiling ngapi? Hata ufanye kazi miaka 200 huwezi kuwa na maendeleo.
Watu bado wanategemea kilimo cha mvua, jembe la mkono, mbegu za zamani n.k Eimu nursery 1yr, msingi 7yrs, sekondary 4yrs, advanced 2yrs na chuo 3yrs. Hapo shuleni unajifunza theory.
Wafrika wanafanya kazi sana ila tatizo mishahara midogo na teknolojia duni
 
Uko sahihi.

Lakini mleta mada yuko sahihi pia. Sana.

Swali la kujiuliza ni ubora na utendaji wa watu wa huko ndio umewapa Mfumo thabiti unaowalinda wote kwa usawa ule ule kiasi kwamba matokeo mwisho wa siku ni almost sawa kwa wote kwa mujibu wa hiyo willingness ya kulipa gharama yoyote ili mradi kupata wanachohitaji?…ie Maisha mazuri…etc?

Je, sisi kinachotufanya tukwame ama kwenda mwendo wa kobe katika ujenzi mzima wa maisha yetu ni Mfumo ambao tumewekewa tu hata hatujui muwekaji ni nani na madhumuni ni Yapi? Kutunyonya?

Ama sisi ndio adui zetu kwa sisi wenyewe?

Kwamba tunahusika na aina ya Mfumo unaoendesha maisha yetu kiasi kwamba tuko katika mkwamo kwa sababu hakuna wa kumfunga paka kengele?

Kuna jambo lipo hapo kati linalosababisha utofauti huu mkubwa uliopo haswa ikizingatiwa kimaumbile tu ni wazi race ipi imependelewa kwa kiasi zaidi ya zingine katika kuendana na mazingira ya Dunia hii.

Je, hilo jambo ni makusudi na uumbaji wa binaadam mwenyewe? Ama ni natural force at work?

Tunaweza kulibadili na kupindua meza ama kuliondosha na kutengeneza usawa kati ya wote? Wa kule na wa huku?
Nadhani maswali yako mengi nimeyajibu kwenye vipengele vinavyofuata na mtoa mada nilimpa tu food for thought.., Hard Work does not Necessarily pay kwahio angeweza kuongelea efficiency na effectiveness lakini sio necessarily hassling... nadhani ndio maana nikasema ni vema tukaangalia uhusiano kati ya uvivu na umasikini

Suala la kupindua meza au kwanini tupo katika hii predicament nachoweza kukwambia ni Kwamba Necessity is the Mother of all Invention.... hao western tunaowasifia leo wala civilisation haikuanzia kwao na mengi wanayofanya either waliyaiga au kuwa-subjugate wengine (miji kama liverpool imejengwa na kujengeka sababu ya Utumwa) Nchi kama Belgium imejengwa kwa jasho la Congo) - Great Britain ni Kisiwa ilibidi watoke huku na kule kwenda kutafuta colonies ili waweze kuishi...; Egypt vitu kama irrigation vilianzia huko....,

Africa ingawa ukiangalia historically vitu kama pottery na ufuaji vyuma tulikuwa navyo lakini maisha ya huku mtu angeweza kuishi bila kujituma (kwanini uhitaji fridge wakati una mtungi, kwanini uhitaji AC wakati ukilala nje unapigwa Natural AC)

Kwahio huku tunapoelekea when the push comes to shove na maisha yanazidi kuwa magumu for better or for worse mambo yatabadilika (watu lazima tutapigana na kuchukiana) kwanini you might ask..., Sababu hatuna viongozi bora, tuna viongozi ambao ni walafi wanajenga kesho yetu ya matabaka na watu wenye nothing to loose..., kwahio ikifikia hapo All Hell will Break Loose.....
 
Siamini kama waafrika ni wavivu sana Kuliko race zingine.

Propaganda...............
Ngoja nikaisome Italy kiundani zaidi
 
Mwafrika hasa mtanzania anataka apige kazi masaa nane tena hayo bado anaona ni mengi,

Awahi kutoka kazini apitie baa amwagilie moyo na nyama choma huku akibishana simba na yanga.

Wanawake wanataka wawahi kutoka kazini wapitie saluni wakajirembe huku wakipiga soga na umbea.

Halafu jumapili wakajazane makanisani wakipayuka kama mbayuwayu kumuomba Mungu wapate mafanikio.

Hawa ndio waafrika..!!
We mzungu tuonyeshe mambo ya maana uliyoyafanya na yanagusa watu
 
Yaani tusijidanganye hata siku moja.

Watu weusi tunajisemaga tuko na maguvu etc..

Ila kwa jinsi hawa wenzetu ngozi nyeupe wanavyopiga kazi speed yao kama umekaa kibwegebwege utakuwa unalia kila siku

Hawa jamaa ni nuksi jamani, yaani huku kufanya kazi saa 12 + ni jambo la kawaida sana.

Halafu wako speed kama legelege lazima utapike dagaa.

Watu weusi tuko polepole sana hata kazi nchini kwetu infact ukisema u rate kwenye scale ya 10
Hawa wenzetu wako 9/10 sis tuko 1/10

Yaani hakuna kitu wakuu, nadhani hii ndio siri kubwa ya wao kutupiga gap la maana achana na kelele za ohh walikuja kuiba malighafi Afrika hizo ni kelele za kujitetea tu hawa jamaa ni watafutaji yaani wana ile spirit ya kichaga na kikinga mara 100

Ni hayo tu wadau, tupambane. sana

Na haijalishi ni me au ke hawa watu ni hatari na wanaanza michakato wadogo kabisa yaani 18yrs mtu anapiga kazi
Tena waambie watanzania wanaona kula ugali ndio kuwa na miguvu, watu wanakula pizza na burgers, na wanapiga kazi kama wendawazimu. Ila watanzania wakiona huli ugali basi sijui wankuchukuliaje
 
Hizo sio kazi mkuu ni mishemishe.
Huu uzi unaojadili, watu wanajadili huku wamelewa?
Mtu anafanya kazi kiwandani, analipwa 6000 mpaka 7000 kwa siku. Anaingia saa 1 asubuhi mpk saa 1 usiku. Chakula juu yake.
Hapo hata afanye kazi miaka 4000 hawezi kutoboa maisha.
 
Mwafrika hasa mtanzania anataka apige kazi masaa nane tena hayo bado anaona ni mengi,

Awahi kutoka kazini apitie baa amwagilie moyo na nyama choma huku akibishana simba na yanga.

Wanawake wanataka wawahi kutoka kazini wapitie saluni wakajirembe huku wakipiga soga na umbea.

Halafu jumapili wakajazane makanisani wakipayuka kama mbayuwayu kumuomba Mungu wapate mafanikio.

Hawa ndio waafrika..!!
Ufanye kazi masaa 24 halafu unalipwa shiling ngapi?
Mwalimu unayemjua anazidiwa hela na kondakta wa daladala
 
Nadhani maswali yako mengi nimeyajibu kwenye vipengele vinavyofuata na mtoa mada nilimpa tu food for thought.., Hard Work does not Necessarily pay kwahio angeweza kuongelea efficiency na effectiveness lakini sio necessarily hassling... nadhani ndio maana nikasema ni vema tukaangalia uhusiano kati ya uvivu na umasikini

Suala la kupindua meza au kwanini tupo katika hii predicament nachoweza kukwambia ni Kwamba Necessity is the Mother of all Invention.... hao western tunaowasifia leo wala civilisation haikuanzia kwao na mengi wanayofanya either waliyaiga au kuwa-subjugate wengine (miji kama liverpool imejengwa na kujengeka sababu ya Utumwa) Nchi kama Belgium imejengwa kwa jasho la Congo) - Great Britain ni Kisiwa ilibidi watoke huku na kule kwenda kutafuta colonies ili waweze kuishi...; Egypt vitu kama irrigation vilianzia huko....,

Africa ingawa ukiangalia historically vitu kama pottery na ufuaji vyuma tulikuwa navyo lakini maisha ya huku mtu angeweza kuishi bila kujituma (kwanini uhitaji fridge wakati una mtungi, kwanini uhitaji AC wakati ukilala nje unapigwa Natural AC)

Kwahio huku tunapoelekea when the push comes to shove na maisha yanazidi kuwa magumu for better or for worse mambo yatabadilika (watu lazima tutapigana na kuchukiana) kwanini you might ask..., Sababu hatuna viongozi bora, tuna viongozi ambao ni walafi wanajenga kesho yetu ya matabaka na watu wenye nothing to loose..., kwahio ikifikia hapo All Hell will Break Loose.....
Afrika hatuna mifumo kila kitu kipo shaghala bagala
Watu wamekataa tamaa kwa kiwango kikubwa sana
 
Ufanye kazi masaa 24 halafu unalipwa shiling ngapi?
Mwalimu unayemjua anazidiwa hela na kondakta wa daladala
Afrika watu walishajituma alafu wakajashtuka wanastaafu hawana kitu huku waizi wa mali za umma wakineemeka

Yaan afrika hakuna mifumo ya uzalishaji ambayo imewekwa na ambayo itanifaisha watu
Mfano scheme zote zilizopo za kilimo za umwagiliaji ni za mkoloni hakuna scheme ya maaan tumejenga sisi na ziko walizojenga wakoloni zimejifia
 
Kuna wajerumani walikuwa wanafundisha ishu za mechanical walikuwa wanapenda kuuliza "hivi nyinyi mna nchi yenu?" Yani walikuwa wanaangalia watu wenye nchi yao wenyewe kwa namna ambavyo hawako serious kabisa na hawajali kana kwamba wamekuja masomoni wakimaliza wanarudi kwao. Bullshit
 
Yaani tusijidanganye hata siku moja.

Watu weusi tunajisemaga tuko na maguvu etc..

Ila kwa jinsi hawa wenzetu ngozi nyeupe wanavyopiga kazi speed yao kama umekaa kibwegebwege utakuwa unalia kila siku

Hawa jamaa ni nuksi jamani, yaani huku kufanya kazi saa 12 + ni jambo la kawaida sana.

Halafu wako speed kama legelege lazima utapike dagaa.

Watu weusi tuko polepole sana hata kazi nchini kwetu infact ukisema u rate kwenye scale ya 10
Hawa wenzetu wako 9/10 sis tuko 1/10

Yaani hakuna kitu wakuu, nadhani hii ndio siri kubwa ya wao kutupiga gap la maana achana na kelele za ohh walikuja kuiba malighafi Afrika hizo ni kelele za kujitetea tu hawa jamaa ni watafutaji yaani wana ile spirit ya kichaga na kikinga mara 100

Ni hayo tu wadau, tupambane. sana

Na haijalishi ni me au ke hawa watu ni hatari na wanaanza michakato wadogo kabisa yaani 18yrs mtu anapiga kazi
Ni kweli....

Kazi ni kipimo cha utu
 
Bongo maisha ni rahisi ukikwama mjomba anakupiga tafu.
Huko hakuna mjomba
 
Afrika watu walishajituma alafu wakajashtuka wanastaafu hawana kitu huku waizi wa mali za umma wakineemeka

Yaan afrika hakuna mifumo ya uzalishaji ambayo imewekwa na ambayo itanifaisha watu
Mfano scheme zote zilizopo za kilimo za umwagiliaji ni za mkoloni hakuna scheme ya maaan tumejenga sisi na ziko walizojenga wakoloni zimejifia
  • Mbunge amekaa bungeni analipwa 200k km posho hapo bado mshahara ila mwalimu analipwa 500k kwa mwezi
  • Mafao analipwa akimaliza ubunge miaka 10 ila wengine wasubiri wafikishe miaka 50 halafu kuna kikokotoo
  • Huduma za afya ni changamoto
  • Elimu yenyewe unajifunza theory.
Tuna matatizo mengi sana kuliko watu wanavyofikiria na wala suala siyo kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom