Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Serikali imefungia kurasa za mitandao ya Fabebook 361, Instagram 198, Twitter 12 na vikoa 2,456 ambazo zilikuwa zinajihusisha na matangazo ya ukiukwaji wa maadili ikiwemo mapenzi ya jinsia moja.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumatatu Aprili 17, 2023 na Waziri wa Habari Nape Nauye wakati akitoa nyongeza ya majibu ya Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest ambaye amehoji mkakati upi wa Serikali kuhusu watu wanaohamasisha uvunjifu huo wa maadili.
Nape amesema serikali ilishadhibiti vitendo hivyo ikiwemo kuzuia matangazo kwenye vyombo vya habari lakini akasema kumekuwa na changamoto kwenye mitandao ya kijamii ambako nako wameanza kudhibiti.
Baada ya kuiona taarifa hiyo, kuna kitu nimekumbuka.
Zamani ilionekana Mtandao wa TWITTER ni wa watu wa hadhi fulani hivi kulinganisha na FACEBOOK.
Lakini siku hizi, TWITTER imevamiwa na wahuni wanaoutumia mtandao huo kuhamasisha ngono.
Kumekuwa na utaratibu siku hizi ikifika usiku utakutana na posti yenye kichwa kinachosema "Haya watoto wameshalala threads" halafu inasindikizwa na picha chafu.
Ukiangalia hizo reply, ni balaa zito. Utakuta video za ngono, picha za uchi, yani tafrani.