Ubadhirifu wa dawa zenye thamani ya Tshs 26.7 billioni wabainika kwenye Hospitali za Rufaa za mikoa 28 Tanzania bara

Ubadhirifu wa dawa zenye thamani ya Tshs 26.7 billioni wabainika kwenye Hospitali za Rufaa za mikoa 28 Tanzania bara

Mfumo wa afya wa nchi hii lazima ubadilike kinyume na apo mtakuwa mnawaonea watumishi kila siku kuwa wanawaibia dawa....
Unatuchimba biti kwamba tushindwe kusema, Ni kweli ukienda hospital wanasema hawana dawa, na mpaka sasa hospital ni Ela mapaka kwa watoto chini ya miaka mitano na wajawazito.
 
Kwa hizo tuhuma lazima mzee baba atoke na tamko.
 
Wakati anaunda tume na kamati lukuki ajue huku mahospitali HAKUNA DAWA hata Muhimbili yenyewe
Amfikirie mtu aliyelipa tshs 1500000 kwa mwaka halafu akifika hospitali anaishia kuandikiwa dawa akanunue kwa fedha zake
Pia atoe suluhisho la kwa nini maduka ya dawa ya watu binafsi hawakubali kupokea order za NHIF (tetesi:; huwa bila mlungula hawalipwi).
Mzee nliandikiwa dawa flani hivi nlizunguka maduka yote wananiambia hakuna hiyo dawa mpaka pale nilipotoa fedha zangu binafsi na kuificha ile NHIF notice.
 
Suala la Afya Tanzania ni changamoto kubwa sana, pamoja na kwamba muda mwingine tunailaumu Serikali kwa mambo kadhaa kwenye afya ila watumishi nao wamekuwa sehemu ya hizi changamoto, wapo radhi watanzania wenzao wakose huduma na hata wafe kwa ubinafsi wao wa kuiba vifaa tiba, madawa nk.

Bila shaka wahusika watachukuliwa hatua kali wawe mfano, sitarajii hatua kali za kuhamishwa vituo vya kazi.
Mtu akitimiziwa ahadi zake atawajibika na kujituma kwenye majukumu yake unless otherwise ataona bora liende tu .miaka 5 bila nyongeza wala kupandishwa madaraja ubategemea nini?
 
Shidah kubwa serikali inayegemea mtu wa mwisho ndo apambane kuipa sifa serikali halafu huo wa mwisho nd mnyonge kwa kila kitu.
 
Suala la Afya Tanzania ni changamoto kubwa sana, pamoja na kwamba muda mwingine tunailaumu Serikali kwa mambo kadhaa kwenye afya ila watumishi nao wamekuwa sehemu ya hizi changamoto, wapo radhi watanzania wenzao wakose huduma na hata wafe kwa ubinafsi wao wa kuiba vifaa tiba, madawa nk.

Bila shaka wahusika watachukuliwa hatua kali wawe mfano, sitarajii hatua kali za kuhamishwa vituo vya kazi.
Haya mbona ni serikali nzima? Nenda ardhi, mahakama, uhamiaji uone kama kuna tofauti.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Wewe dishi lilishapoteza uelekeo kitambo sana. Yaani wewe hadi wakati wa Ku. Nya utakua unaiwaza tu Chadema. No connection at all!!

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2]
 
  • Haitoshi kufanya mabadiliko tu ya wafujaji wa mali ya umma.
  • Hawa ni sawa na wauaji
  • Hebu Tafakari wagonjwa wangapi wamepoteza uhai kwa kukosekana vifaa tiba na dawa kisa hawa wezi wameiba!
  • Duru za habari zinasema Mheshimiwa Waziri umeagiza mabadiliko ya Menejimenti 28 za hospitali hizi za rufaa kutokana na wizi huu (D/News,2021)
  • Nashauri baada ya timu yako uliyoiunda kuweka mezani ukweli, ni wazi kwamba WAHUJUMU hawa ambao sisiti kuwaita WAUAJI wachukuliwe hatua kali.
  • Hii ni white-colar crime haina tafauti na MWIZI WA KUKU huku mtaani kwetu.
  • Watu wa namna hii wasifumbiwe macho na kuendelea kuwaacha kwenye PUBLIC SERVICE ni kutoitendea haki jamii.
  • Wameiba kiasi kikubwa sana cha vifaa tiba na dawa 26.7 BILIONI sio fedha za kitoto hiyo ni hasara kubwa kwa taifa.

WITO WANGU:
Mheshimiwa Waziri hawa waliobainika wakamatwe wapandishwe Kortini kwa wizi wa kuaminiwa ni wahujumu uchumi na wauaji.

Na kwa kuwa Kamati uliyoiunda ndiyo iliyobaini madudu haya ina maana tayari ushahidi upo wa kuwapandisha kortini. WASIACHWE HAWA wamegharimu maisha ya ndugu zetu.

images.jpg
 
Hii ni kufuatia malalamiko mbalimbali nchini ya wananchi kukosa dawa ni nini kifanyike kudhibiti udokozi wa dawa!?
 
Kuna wizi mkubwa Kwenye vituo vya afya nchini.wezi wa dawa hizo ni kupitia wa pharmacia,wagonjwa wenyewe( kwa kutumia Bima za afya) .Dawa hizo haziuzwi kwenye Kwenye private hospital kama wanavyofikiria wengi bali Kwenye maduka ya dawa.

Ukisema utaenda kukagua Kwenye private hospital hutapata majibu sahihi sana .Nendeni Kwenye maduka ya dawa hapo ndipo mtakamata wengi.kuna na wengine wanauzi madawa bila kuwa na leseni za biashara.hawa ndiyo wezi wakubwa wakishirikiana na wagonjwa.
 
Subiri serikali inakuja kukagua ndipo utasema mimi nina wivu
Mmekalia majungu badala ya kufanya kazi, pharmacy zimeajiri watz wangapi? pesa zinapigwa kwenye miradi mikubwa huko hamsemi mnang'an'gana na kopo la paracetamol la shilingi elf 7 jamani!
 
Mmekalia majungu badala ya kufanya kazi, pharmacy zimeajiri watz wangapi? pesa zinapigwa kwenye miradi mikubwa huko hamsemi mnang'an'gana na kopo la paracetamol la shilingi elf 7 jamani!
Kwahiyo wizi wa dawa uendelee,serikali idili na wezi wa huko kwenye miradi,sindiyo Chief?
 
Back
Top Bottom