Tetesi: Ubaguzi wa ajira kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Nyinyi ndio wale watanzania wa nyuma ya keyboard. Tanzania mliyonayo akilini ni ile ya 1985, yanayotokea Dar na kwenye miji mikubwa ndio kipimo chenu cha nchi ambayo Mungu ametujalia.

JPM atakumbukwa kwa miaka mingi ijayo, kwa sababu hashughuliki na maslahi pekee ya watu wa mijini ambao siku zote hawana shukrani.

JK anaonekana malaika baada ya kuondoka pale magogoni, huo ni ushahidi wa uwepo wa watu wengi kama wewe mkuu chabuso.
 
Dah!! Tunaelekea wapi na Tanzania yetu... Yameanza visiwani huko bara yananukia au yalishafika sema hatujashtukia... Ila malipo ya hawa wanaharamu watayapata hapa hapa duniani
 
Mwal Nyerere alishasema mkianza kuwabagua wabara mtakuja upemba na uunguja, Waache kuwabagua wabara lasivyo dhambi hii itawatafuna daima

Kama wanavyobaguliwa wachaga na wakaskazini .Hii ni sera ya Laanatullahi Nyerere na CCM yake
 

Si ndio akatujengea international airport kule Chato ili tupate watalii wengi wa kwenda kuvuta ugolo , na pia usisahau vile vi wonder vya ugolo kule Chato
 
Ubaguzi uko kwenye damu, acha kusingizia siasa....nafanya shughuli zangu Zanz nayashuhudia yote haya ila tunawaona mapoyoyo tu maana hata wakinibagua hawanipunguzii chochote ....ila kwa kujifanya watu wa dini sasaaaa!!!!!

Tatizo unatoa huduma Kwa mapadri tu
 
Si ndio akatujengea international airport kule Chato ili tupate watalii wengi wa kwenda kuvuta ugolo , na pia usisahau vile vi wonder vya ugolo kule Chato
Mkuu, viwanja vya ndege vinajengwa nchi nzima, pesa inatumika kwa faida ya wengi na sio wachache wenye mawazo ya kibinafsi kama wewe.

Endeleza kejeli za mitandaoni wakati watu wanapiga kazi ya maana kila kona ya Tanzania.

Secularism unayoipinga huwezi kuizuia, labda ufe halafu uzaliwe kwenye dunia nyingine.
 
Usilolijua ni bora ukae Kimya....
Pumbavu
 
Hii kitu ipo sana na si zanzibar hadi bara. Hata kama una vigezo vimejitosheleza.. bado watademand loyalt flan kutoka kwako either pesa au kuwa mwanachama.
Bara imekuwa iki copy mambo mengi ya dhulma kutoka Zanzibar, angalia chaguzi za hivi karibuni Bara.
 
Ubaguzi uko kwenye damu, acha kusingizia siasa....nafanya shughuli zangu Zanz nayashuhudia yote haya ila tunawaona mapoyoyo tu maana hata wakinibagua hawanipunguzii chochote ....ila kwa kujifanya watu wa dini sasaaaa!!!!!

Hata Tanganyika kumejaa ubaguzi na zarau kwa Wazanzibari.
 
Ni kweli kabisa mie rafiki zangu wengi wamepata ajira kupitia njia hyo mpka uwe na card ya ccm yaani kuna kipengele unajaza number ya card ya ccm. Hasa ajira za walimu nimeshuhudia live. Jamaa wanaigawa Zanzibar kabisa.
Umeona . Kuna wengine walitaka kupindisha taarifa hizi
 
Matatizo ya uajiri mpya yanaanzia kwenye "short lists" hii ni hatua ya mwanzo ya kuwatoa wapinzani, hatua nyengine ni "veting" ambayo hufanywa na usalama wenye maslahi na UVCCM. Mrejesho wa veting zao huwaacha watu fulani wenye asili ya maeneo fulani (hasa wapemba) na familia zenye kuhisiwa kuwa na Upinzani. Taarifa zinasema waathirika wakubwa ukiacha watu kutoka Pemba, ni watu wa kaskazini ya Unguja na watu wa majimbo yenye nguvu kubwa za upinzanio na mjini hasa watu wenye asili ya kiarabu.
 
JPM atakumbukwa kwa:-"hawa msiwavunjie wamenipigia kura,hawa wavunjiwe hawajanipigia kura,hawa wafukuze kazi vyeti vyao feki,huyu mwacheni kabila letu moja,huyu mpigeni risasi anapingana na mawazo yangu"...

Kwa ufupi JPM atakumbukwa kwa kuirejesha nyuma Tanzania kidemokrasia,na kupindisha haki za msingi kwa kila mtanzania,Tanzania ya leo kila mtanzania kajiininamia kwa msongamano wa mawazo,wale wenye uwezo wameanza kukimbilia Finland kwenda kutafuta ukimbizi,wengine waliobakia wamejawa na hofu ya maisha yao..

"Raisi wa ajabu haijawahi kutokea Tanzania":-TAL
"Tanzania inaongozwa na watu washamba" :-ZZK
 
HAYA MAMBO MBONA MNAYASEMA LEO WAKATI MUANZILISHI WA MAMBO HAYO NI SHEIKH SEIF SHARIF HAMAD .
Baada ya mapinduzi kulikuwa hakuna huyu mpemba na huyu muunguja na ndiyo maana hata scholarships za elimu ya juu vijana wengi wa kipemba na unguja walinufaika. Wakati Sheikh Seif aliposhika madaraka ya kuwa Cheif Minister wa SMZ pamoja na ujumbe wa CC, Alianza mkakati wa kuhakikisha vijana toka pemba wanaajiriwa na kupewa madaraka bila kuwepo na uwiano na wenzao. Baadaye ndipo ilipojulikana kuwa bwana huyu alikuwa anatengeneza mfumo ndani ya mfumo rasmi ili kutekeleza azma yake ya kuutaka urais wa zanzibar. Sasa leo kilio hiki ni cha nini?
SIKU ZOTE DHAMBI INA MALIPO YAKE NA HAPA KAMA KWELI SUALA HILI LIPO SMZ BASI MWENYE KUBEBA ZIGO HILI NI SEIF SHARIF.
MTENDA AKITENDEWA SIKU ZOTE HUHISI KUWA ANAONEWA.
 

Si ndio hata chato mnajenga mupate kusafirisha ugolo??
 
Sasa kama Seif Sharif kayaanzisha CCM ndio wayaendeleze,sasa hapo kutakuwa na tafauti gani kati ya Seif Sharif na CCM Zanzibar!??.

Kwani mkiwakosesha ajira wapemba na Wazanzibari wasio na asili ya Kiafrika anaepata tabu nani Seif Sharif au wazanzibari na familia zao
 

Unao ushahidi wa unayoyasema??Yaan Y nyinyi mnawachukuwa wagalatia walioforge vyeti kutoka Tanganyika kwa sababu tu wapate kuwapigia kura CCM na mnawaacha ndugu zenu waislamu Kwa sababu ni wapinzani.
 

Ina maana kwanza unakiri kuwa haya yapo na ni sawa kufanywa.

Kwa hiyo haya ndio malipo ya Seif Sharif sio? halafu tunajiapiza kuwa tuna utawala bora na umoja ?

Kuna hio dhana kuwa Seif alipendelea lakini cha kushangaza tokea Baada ya Mapinduzi inajulikana ni nani waliojazwa kwenye serikali hadi leo hii. Sidhani kama hao wapinzani walipata nafasi yoyote. Hebu tuambie baada ya mapinduzi hadi leo kwenye vikosi, wizarani, mashirika, nk. nani wanaongoza kwa wingi ?.

Acheni ubaguzi kwa maslahi ya Taifa.

SMZ ijisafishe kwa ubaguzi kama upo.
 
Msameheni huyo ndio wale wale.
 
Kuna taarifa kuwa licha ya hao watu kutoka Pemba kukosa fursa ndani ya Serikali kwa takribani miongo zaidi ya mitatu (1990- 2000, 2018)na kabla ya Mapinduzi, Jamii za watu wa Pemba zina wasomi imara na wataalamu ambao hujitafutia kwa njia zao pasi kutegemea serikali.

Hapa tunazungumzia huu ubaguzi wa ajira. Kwa nini wapinzani wabaguliwe ?
 
Mkuu kuna wakati wa utawala wa Aboud Jumbe Mwinyi nusu ya mawaziri wake walikuwa wanatoka Pemba,hata Seif Sharif kutokana na maneno yake mwenyewe , Aboud Jumbe ndie aliemleta katika siasa..

Ubaguzi ni kitu kibaya,hakuna alie amilika kila mtu anafanya makosa,katika siasa,wanasasa wanafanya mambo mengi ya maamuzi kwa maslahi yao binafsi,..lakini haina maana kuwa makosa yaliyofanywa yaendelezwe au kurudiwa,ijengeni Zanzibar yenu,piganieni mnachokitaka,acheni kubaguwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…