Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania watoa tahadhari ya uwepo wa tishio la shambulio la kigaidi

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania watoa tahadhari ya uwepo wa tishio la shambulio la kigaidi

Kuna mada kama huziwezi ni bora ukakaa kimya tu. US ana inteligenc ambayo haijawahi kushuhudiwa toka ulimwengu uwepo, kasome bajet ya ulinzi wa US, Bajet ya Ulinzi pekee inaweza ikawa mara 50 ya bajet nzima ya TZ.

Chukua bajet ya ulinzi ya UK, France, Russia, Italy, German n.k ukijumlisha kwa pamoja, hawafiki nusu ya bajeti ya ulinzi ya US.
Mahaba Niue haya, elewa swali!
 
Si la kupuuzia hili, hao wamarekani wakitoaga onyo ni jambo la kuchukulia serious.

Kampala walitoa onyo zikalipuliwa sehemu mbili mwaka jana.

Nahisi ngoma hii itakuwa mlimani city, masaki, oysterbay au posta.
mmeanza kazi!!
 
Ubalozi wa Marekani Nchi Tanzania umeonya juu ya kuwepo viashiria vya Shambulio la Kigaidi katika maeneo mbalimbali yanayotembelewa zaidi na Raia wa Nchi za Magharibi ikiwemo Marekani

Maeneo yaliyotajwa kuwa kwenye mipango ya kushambuliwa na Vikundi vya Ugaidi ni pamoja na Hoteli, Balozi mbalimbali, Maduka makubwa na Masoko, Vituo vya Polisi na Misikiti.

View attachment 2495591
Jukumu la ulinzi na usalama wa nchi ni la kila raia. #Kuanzia mleta taarifa, mimi, wewe na yule tuilinde kizalendo nchi yetu pendwa ya mababu na mabibi dhidi ya uadui wa ndani au nje.🙏🙏🙏
 
Maskini mimi at least sehemu tajwa huwa siingiagi!

Wakigusia Mwendokasi wamenimaliza maana ndiyo anga zangu huko.
Waongo mkuu kipindi cha Magufuli walizui raia wao kuja Tanzania kwasababu kuna vitisho vya ugaidi, wakasema tena Tanzania kuna ugonjwa wa Ebola, kwaiyo awa ndugu zetu Tahadhari zao ni za kitapeli, kipindi cha Magufuli walitoa tahadhali nyingi sana na hakuna tukio lolote lilotokea Dar
 
Yaani jamaa wanajuaje kwamba kuna kuna tukio la ugaidi kama si wao ndo wanalipanga..... the logic is clear
Wana informants huko huko Al Shabaab..... Kenya nakumbuka walikua na snipers wawili huko Al Shabaab Sasa yule informant wa CIA ndani ya Al Shabaab akawachoma. Jamaa mmoja alichinjwa Mombasa mwenzie akatwangwa risasi akiwa kwenye gari.

So tokea tukio lile litokee ndio watu wakafahamu Al Shabaab Ina mapandikizi kutoka mataifa mengi Ili kulinda maslahi Ya nchi zao. So ukiona Tanzania haijalipuliwa trust me Kuna informant kule ana divert hizo mission!!
 
Waongo mkuu kipindi cha Magufuli walizui raia wao kuja Tanzania kwasababu kuna vitisho vya ugaidi, wakasema tena Tanzania kuna ugonjwa wa Ebola, kwaiyo awa ndugu zetu Tahadhari zao ni za kitapeli, kipindi cha Magufuli walitoa tahadhali nyingi sana na hakuna tukio lolote lilotokea Dar
Mbona issue ya Garissa walionya na ikatick..... Tusipende ujuaji! wao Wana intelijensia kuliko nchi zetu maskini hizi sio sisi ikitokea mikutano ya Chadema ndio eti taarifa za intelijensia zinafanya kazi!!
 
Nakumbuka alert kama hizi kule Kenya, halafu wakashambulia supermarket ile maarufu, na chuo kikuu kimoja.

Serikali ianze kukagua maduka na ofisi zote zilizopo kwenye supermarkets kubwa. Kule Kenya walipanga kwenye supermarket, kumbe wakawa wanahifadhi humo silaha.

Serikali iombe usaidizi kwa US na Kenya maana wote wana uzoefu na mambo haya.
Umesema kweli. Na mikutano ya hadhara izuiwe. Ugaidi sio mzuri, watu wasio na hapoteza maisha
 
Tahadhari hii imetolewa leo 25/01/2023! Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umewatahadharisha wananchi au Raia wa Marekani waliopo nchini Tanzania [emoji1241] kwamba kuna viashiria vya shambulio la kigaidi kufanyika nchini, toka vikundi vya kigaidi ambavyo haikuvitaja rasmi.

Kwa maeneo waliyoyataja hapo chini;

......

By U.S. EMBASSY ,
DAR ES SALAAM
JANUARY25, 2023

SECURITY ALERT – U.S. EMBASSY DAR ES SALAAM, TANZANIA

Location: High traffic areas frequented by Westerners in Dar es Salaam and elsewhere in Tanzania

Event: Locations frequented by U.S. citizens and other Westerners in Dar es Salaam and elsewhere in Tanzania continue to be attractive targets to terrorists planning to conduct attacks. Terrorist groups could attack with little or no warning, targeting hotels, embassies, restaurants, malls and markets, police stations, mosques, and other places frequented by Westerners.

Actions to Take:

Be alert to your surroundings.Practice personal security measures.Stay alert in locations frequented by tourists/Westerners.Keep a low profile.Visit our website for Travel to High-Risk Areas .S. citizens who travel abroad should always have a contingency plan for emergency situations.  Review the Traveler’s Checklist .

Assistance:

U.S. Embassy Dar es Salaam, Tanzania
686 Old Bagamoyo Road, Msasani,
P.O. Box 9123
Dar es Salaam, Tanzania
+255 22 229 4000

drsacs@state.gov

Je, ni imetokea tu au ni mpango maalumu?
 
Zuio la mikutano linaweza likafuatia,japo siyo sehemu za mikutano si sehemu zitembelewazo na US citizenens na Westerners wengine.
Ngoja serikali iende na biti muone.
 
Back
Top Bottom