Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania watoa tahadhari ya uwepo wa tishio la shambulio la kigaidi

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania watoa tahadhari ya uwepo wa tishio la shambulio la kigaidi

Au CCM itafanya tukio moja lamkigaidi ili wapate sababu ya kusitisha mikutano kwa muda usiojulikana
 
Kuna mada kama huziwezi ni bora ukakaa kimya tu. US ana inteligenc ambayo haijawahi kushuhudiwa toka ulimwengu uwepo, kasome bajet ya ulinzi wa US, Bajet ya Ulinzi pekee inaweza ikawa mara 50 ya bajet nzima ya Tanzania...
Hamna uhusiano na mikutano ya CHADEMA
Wazungu na CCM WANAJUANA KWA VILEMBA
 
Sasa kama tayari wanajua kutatokea shambulio la kigaidi, kwa nini wasiwakamate hao magaidi kabla ya kushambulia, au wao ndio wapangaji wa shambulio hilo?. Hao magaidi itakuwa wanawajua ni wa kutoka wapi na sababu za kushambulia
 
Ni vyema sana umemjibu huyi bwana kwa utu na uungwana... kuliko wenye kumshushua na kumbeza!

Mwenyezi mungu akubariki sana!

Hahaha! Gaidi sio maana yake hiyo iliyojengwa mawazoni mwako...

Gaidi ina maana yake. Soma na pekua usome kinagaubaga wa neno "terrorist" & "terrorism"

Linakuzwa kwa sababu ya chuki za kidini lakini si hao unaowaona wanajifanyia zao ibada ndo magaidi...hapana 😊
Soma! Chimbua maarifa... utapata mengi. 👍🏾
Itachukua miaka mingi kufuta hiyo kitu vichwani mwa watu wengi, tena hasa wale wavaa suruali fupi ndo hao niko jirani nao
 
Waongo mkuu kipindi cha Magufuli walizui raia wao kuja Tanzania kwasababu kuna vitisho vya ugaidi, wakasema tena Tanzania kuna ugonjwa wa Ebola, kwaiyo awa ndugu zetu Tahadhari zao ni za kitapeli, kipindi cha Magufuli walitoa tahadhali nyingi sana na hakuna tukio lolote lilotokea Dar

Usilolijua ni usiku wa giza,kaa tulia hii nchi inasiri nyingi sana.
 
Duuh aisee nilikuwa nina kijisafari cha kwenda Mlimani City kununua bidhaa flani hv wacha niingie mitini. Nisije nikakutana na wazee wa vilipuzi. Nikajikuta nakosa ugali kambale maziwa mgando na balimi ya bariidi
 
Yaani jamaa wanajuaje kwamba kuna kuna tukio la ugaidi kama si wao ndo wanalipanga..... the logic is clear
Phone tapping,
kwani hawajui kinachoendelea?

Hawana assets kwenye hivyo vikundi?

Kitachotokea ni wao watasaidiana na Polisi kukamata au kuzima shambulizi husika
 
Nakumbuka alert kama hizi kule Kenya, halafu wakashambulia supermarket ile maarufu, na chuo kikuu kimoja.

Serikali ianze kukagua maduka na ofisi zote zilizopo kwenye supermarkets kubwa. Kule Kenya walipanga kwenye supermarket, kumbe wakawa wanahifadhi humo silaha.

Serikali iombe usaidizi kwa US na Kenya maana wote wana uzoefu na mambo haya.
Pale Mlimani City panatakiwa paongezwe ulinzi zaidi, yale magari yanayoingia pale kama kuna magaidi ndani ya dakika chache wanapateka, ila uzuri wa pale exits nyingi sana
 
Labda top ten ya chama,CIA wanazo hadi top secret weapon and devices nenda uliza TISS wana nini?
Sema ukijifanya unajua wenzako/maadui nao wanabuni mbinu tofautu kabisa ambazo hukutarajia. Unakumbuka September 11. Mungu atuepushe.
 
Hao wamarekani,hebu nanda kwao,halafu toa hiyo taarifa ya tishio la ugaidi!, utakiona cha mtema kuni kwa kuleta taharuki,
 
Back
Top Bottom