Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya usifumbie macho udhalilishaji huu dhidi ya viongozi waandamizi wa nchi yetu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Uzalendo wa kujipakaza usoni huku akilini kukiwa hakuna kitu ni hadaa ya kipuuzi!

Habari yako yote uliyoweka hapo haikufanyi uwe mzalendo na kujitangaza hivyo!

Sasa hapa kwa mada hiyo uliyoileta hapa sijui unataka watu wachangie kitu gani, wakubaliane na wewe ndipo waonekane ni wazalendo kwenye jambo la kipuuzi kama hili?
 
Duuuh
 
Serikali ya Kenya haiwezi kufunga websites outside their jurisdiction.
Ingekuwa inamdhalilisha Rais Uhuru Kenyatta, would you dare say such a thing kwamba "serikali ya Kenya haiwezi kufungia website outside their jurisdiction"?
 

Una uhakika Nyerere/Kikwete wanazungumziwa vizuri sana?au ni hisia zako tu?
 
Bwana mdogo hii ni awamu nyingine...

Jiwe aliwaamrisha Citizen TV kuandaaa apology kwa kusema "Ukaidi wa Magufuli" katika kupambana na Janga la UVIKO..

Sasa leo unataka jiwe atoe amri na amekwishakufa?

Pia mwisho mbona Lissu ameitwa Shoga mara kina Mbowe mbona hukutetea?
 
Bwana mdogo hii ni awamu nyingine...

Jiwe aliwaamrisha Citizen TV kuandaaa apology kwa kusema "Ukaidi wa Magufuli" katika kupambana na Janga la UVIKO..

Sasa leo unataka jiwe atoe amri na amekwishakufa?
Jiwe ndio nani mkuu?...
 
Sasa kama ni nonsense unafikiri serikali ya Kenya itapoteza muda wake kujihusisha na nonsense!
Mkuu, masuala ya sheria za Kenya na udhalilishaji wa viongozi wetu hauna uhusiano kabisa. Ni lazima tuwe wakali linapokuwa suala zima la kulinda heshima yetu kama taifa. This is nonsense.
 
Kenya ni tofauti sana na wengine katika EAC ambao wengi wao ni madikteta.
Uhuru anafanyiwa dhihaka na wananchi wake na wala hafanyi chochote.
Kwanini unaongelea uwezekano? Ina maana hauna uhakika? Kuna proof gani kama ubalozi umeganya hivyo? This is against our common EAC values. Rais sio msanii wa bongo movie wa kufanyiwa dhihaka.
 
Nani amekupa mamlaka ya kuzungumza kwa niaba ya Watanzania wote wewe unayejiita dereva wa taxi bubu?
Tunachotaka sisi ni kuwa wajue tuna msimamo mkali linapokuja suala la kulinda taswira njema ya taifa pamoja na viongozi wetu waandamizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…